Thursday, August 29, 2013

DRC: Askari wa Tanzania Wa Umoja wa Mataifa auwawa,



Habari kutoka eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika mkoa wa Kivu ya kaskazini zinasema askari mmoja wa kikosi cha kuingilia kati cha Umoja wa mataifa kutoka Tanzania, ameuwawa.

Askari wengine watano wamejeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali ya Kongo wakiungwa mkono na wale wa Umoja wa mataifa, walipokuwa wakipambana na waasi wa kundi la M23. John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Beni. Kuskiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: John Kanyunyu
Mhariri: Josephat Charo

No comments: