Sunday, December 22, 2013

TUMEFANYWA MADAMPO HADI LINI, TUJITAMBUE

Imekuwa kawaida kwa nchi zilizoendelea kuzifanya nchi maskini kama Madampo ya kutupia takataka zao. Kwanini hali hii? Siku ya jana hapa nilibahatika kupitia maeneo ya Mwanjelwa hapa jijini Mbeya na kukutana na USED BETRY (Betri zilizotumiaka) zinauzwa kama nguo za mtumba. Ukiwauliza wametoa wapi hizo used betry wanajibu tunaagiza kutoka nje.

Kweli nchi yetu ni maskini lakini sio kuwa jalala la electonic materials. Kwanini haya yanatokea? Je na sisi tukifika wakati wa kuzalisha bidhaa hizo tutakwenda kuzitupia wapi? Kwa sasa Tanzania kila kitu tunaagiza used. Nguo ni uzed, Magari used, kila kitu nused. Patafikia mahali tutaletewa vyakula used ili tule na tushibe.

Kwanini tumekuwa wavivu wa kufikiri namna hii? Jibu unalo msomaji wangu. Amakweli safari yetu bado ni changa sana, wenzetu wanakimbia sisi tunageuka nyuma na kuanza kutembea kurudi nyuma? Mwambieni Mjomba nauli kamwe haitapatikana ya kusafiria maana bado tu usingizini.

AUSI CHIWAMBO

ausichiwambor@hotmail.com

No comments: