MAKALA
YA CHIWAMBO
Katika
Makala ya Chiwambo leo inazungumzia zaidi juu ya utendaji kazi wa watumishi wa
umma, wanasiasa, na namna vyombo vya habari vinavyotumika visivyo ili kutetea
maslahi ya wachache. Hili linajitokeza kila uchaguzi hasa kuanzia Mwaka 2005,
2010, na inavyoonekana 2015 nayo ipo vivyo hivyo. Wananchi hugawanywa vipande
vipande katika makundi mbalimbali huku makundi hayo yote husimamia maslahi ya
kundi husika.
Katika
nchi yetu kwa bahati mzuri hatuna Ukabila kama kule Nchini Kenya ambapo nchi
hiyo katika kila chaguzi utawala suala la ukabila. Lakini huku kwetu Tanzania
makundi ndiyo tatizo kubwa ambayo lengo kuu ni kushika hatamu ya kuongoza nchi.
Wakati huu karibu kila chama kinazunguzia zaidi kuhusu uchaguzi 2015. Nani
atakuwa Rais ajaye sio kwa chama tawala tu bali hata chama kikuu cha upinzani
nchini Tanzania chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Viongozi
wetu inavyoelekea hasa wale wanaohitaji Urais 2015 wameanza kujisahau.
Wamesahau wapiga kura wao na kuzungumzia zaidi suala la uchaguzi mwaka 2015.
Swali la kujiuliza ni kwamba je wananchi munawatumikia kweli? Panafikia mahali
mtu unapata mashaka juu ya utendaji wao wa kazi. Magazeti wameyatawala kwa
kuandika zaidi habari zao za uchaguzi 2015 na nani atakuwa mbabe katika
uchaguzi huo.
Ukweli
ni kwamba wananchi hatupendi kuona nchi inalumbana juu ya nani atakuwa Rais
ajaye Mwaka 2015 badala yake muwatendee haki hawa Wananchi waliowafanya muingie
hapo Mjengoni. Katika tafsiri ya mwandishi wa habari inasema kwamba ni “The
voice of the voiceless” au Watch dog of the Government”. Hii inamaana kwamba
mwandishi wa habari ni mtu anayewasemea wananchi ambao hawana pa kusemea.
Wananchi
walio wengi Tanzania hasa wale wa vijijini hawana wasemaji licha ya kuwa na
wabunge ambao huwakilisha wilaya hizo na wanaonekana kwao uchaguzi hadi
uchaguzi. Sasa huyu mwandishi anatakiwa kuwa msemaji na mfichuaji wa maovu na
mazuri yote yanayofanywa na Wananchi, kikundi cha watu, pamoja na kuikosoa
serikali iliyopo madarakani kwa kuonesha kwamba hapa bwana mkuu hujafanya
vizuri na hapa umefanya vizuri.
Lakini
kwa sasa waandishi wa habari wetu wamewageuka wananchi. Na wamebadilisha maana
halisi ya Mwandishi wa habari ambapo wameifanya kuwa “Journalist is a person
who deal with the viceveser of the voice of the voiceless”. Inamaanisha
wanajadili zaidi suala la kwamba mwandishi wa habari na kazi yake ni kuweka
kinyume cha tafsili halisi ya kuwasemea wale wasio na sauti na badala yake
kusimama upande Fulani wa kundi analoliamini yeye ili kutetea maslahi ya mtu
binafsi kunyakua kiti cha uraisi 2015.
Hili
ni balaa nan i janga kwa taifa la leo na kesho. Matokeo ya vyombo vya habari
kuwa wapiga debe kwa viongozi wa aina Fulani ni bomu ambalo litakuja
kuwalipukia wenyewe hapo baadaye. Waandishi wenzangu mulio wengi mumekuwa
ndumila kuwili na watawaliwa wa fikra zenu. Inaonesha namna gani elimu
muliyonaye haisaidii Taifa letu badala yake unafuata matakwa ya wachahce wenye
fedha na wanasiasa.
Wewe
mtaaluma wa masuala ya uandishi wa Habari, iweje ufundishwe nini cha kuandika
na mtu ambaye hata taaluma yenyewe ya uandishi wa habari hana na hajawai
kuisoma. Na wengine hata tafsiri ya neon lenyewe Journalism halijui. Sasa
inakuwaje kikundi hiki cha watu kitawale sanaa ya uandishi wa habari. Kwa
msingi huu mutaendelea kununuliwa siku hadi siku, maisha hadi kiama.
Kwa
mabo kama haya munakaa vikao na kusema hatuna uhuru wa Habari nchi. Kama
unakubali kununuliwa na ukanunulika unadhani uhuru utakuwepo kweli? Tumezichoka
habari za kusikia hatuna uhuru wa vyombo vya habari nchini huku ninyi wenyewe
mkiwa mstari wa mbele kuwasaliti wananchi. Munategemea nini? Fedha za leo
zitawatawala ninyi wenyewe hapo kesho. Mara nyingi ninyi munakuwa mstari wa
mbele baadaye kusema kiongozi huyu ni mbaya, hafai na kumwangika vichwa vya
habari vya kumkejeli baada ya kupata madaraka.
Kama
mimi ningekuwa ndiye Rais wan chi hii ningemshinikiza waziri anayehusika na
masuala ya vyombo vya habari andaye mswada mpya zaidi wa kuvinyonga vyombo vya
habari ili wakose uhuru zaidi. Kwani kiasi cha uhuru uliopo wameshindwa
kukitumia. Mambo ya kuzungumzia yapo mengi ten asana kila kona. Hivi swali lenu
ni hili, je umewai kutembelea vijijini kule na kuona nyakati za mvua
wanaishije? Wanakula nini? Adha gani wanayokutana nayo?
Hivi
ni kweli vitu vya kuzungumzia kwenye vyombo vyenu vya habari (Media) vimekwisha
kabaisa? Au munataka wananchi waandamane pamoja na kuwalamba mboko ili muandike
habari zao na muwatumikie vyema? Hivi munadhani hiyo elimu yenu bila wananchi
mungeza kuipa? Utitili wa magazeti sasa unathibitisha usemi wangu kuwa
wanaripoti habari mbalimbali ili kulinda maslahi ya watu wachache badala ya
umma.
Mutazame
maeneo ya Ngorongoro watu wanavyoteseka na Njaa, Tunduru hadi leo korosho
hazinunuliwi na wananchi hawajui lini zitanunuliwa huku watu binafsi wakinunua
kangomba za korosho kwa bei ya shilingi 500 kwa kilo. Ninyi waandishi muko
wapi? Kwanini musiripoti habari kama hizi zinazooneka ni za ulanguzi. Maisha ya
wanatunduru msimu huu wa mvua yanakuwa hali tete? Chakula chao kikuu ni ugali
wa muhogo wa wa kuloweka kwenye maji na kukausha ambao hauna virutubisho
mwilini. Na mvua zinapochanganya watu hushindwa kula na wengine hushindia miogo
ya kupika au uji.
Nakumbuka
mwalimu wangu Mama Mushi wa somo la NEWS REPORTING Chuo kikuu MT. Augustine
Mwanza alinifundisha kwamba Greater The Name Greater The News, And Greater the
Event Greater the New”. Ila hili neon lisitumike visivyo ili kuweza kuwanyima
na kuwafunga midomo wananchi. Pamefikia mahari mtu unahamua kuaghahilisha
kununua Gazeti Fulani kisa linapendelea sana upande Fulani wa chama au kundi la
watu wataka Madaraka badala ya kuwazungumzia wananchi na shida zao zinazozidi
kuongezeka siku hadi siku na zitazidi kuongezeka siku hadi siku.
Inawezeka
waandishi wetu wanafanya haya kwa sababu vyombo vya habari vilivyo vingi nchini
vinamilikiwa na wenye fedha na wanasiasa hivyo wanalazimika kuandika au
kuripoti kile basi wao anachohitaji. kwa mfano kama mimi ningekuwa namiliki
vyombo vya habari basi nikilala nikiamka natoa amri kesho magazeti au media
zangu zote munilipoti kwamba nimetoa msaada huu ili nionekana nafanya mema kwa
wananchi kumbe moyoni ni danganya toto.
HivyoViongozi
wetu tunawaomba muwatumikie wananchi vilivyo ili kuweza kuleta ufanisi zaidi na
kupunguza lindi la umaskini linaloikabili nchi yetu. Masuala ya uchaguzi 2015
yasiwe ndio kikwazo kwa maendeleo ya nchi yetu Tanzania. CCM na CDM na vyama
vingine muwatumikie wananchi kwanza na sio kulumbana juu ya uchaguzi 2015 na
badala yake mufanye kama mulivoagizwa na wananchi. Je ukifika mwaka 2015
utawaeleza nini hao wananchi waliokuchagua kuwa kiongozi wao?
Makala
hii Imeandikwa na Chiwambo Ausi
TEOFILO
KISANJI UNIVERSITY (TEKU)
E-Mail:
Ausichiwambor@hotmail.com
No comments:
Post a Comment