Sunday, January 27, 2013

GESI YA MTWARA SASA YAONEKANA KAMA YALE YA LUDISM YALIYOTOKEA WIINGEREREZA


MAKALA NA CHIWAMBO
Kwa wale waliosoma kidato cha Tano na cha sita Katika History 2 wanaweza kuthibitisha hicho kichwa cha habari. Kipindi kile Nedy Ludy ilifanikiwa kuhalibu viwanda,Majumba na vingine vingi kwa sababu eti ya ugunduzi wa viwanda ambapo nchi hiyo ilipitia kipindi cha mageuzi kutoka kutegemea kilimo na kuingia mapinduzi ya viwanda.  Wananchi wengi waliona hali hile ni tete kwani hawakuweza kunufahika badala yake ni mwendo wa mateso tupu. Waliamua kuchoma moto viwanda kimya kimya.

Kwa wale waliotembelea mikoa ya kusini na wilaya zake ikiwemo Tunduru unaweza kusema kule sio Tanzania. Ni kama nchi nyingine hivi. je tUnaweza kusema viongozi waliotokea kusini wana lahana? Nakumbuka kama dishi langu halijakaa sawa basi hata Rais wa awamu ya Tatu ni wa Masasi pale Lupaso. ameifanyia nini kusini kwa miaka yote aliyokuwepo kule?

 je amechangia kuua bandari ya Mtwara? waangalie viongozi wa sasa wanavyovutia gesi iende mtwara. sasa unaweza kujiuliza kwamba hivi hawa viongozi ni wazalendo kweli? wanafanya nini huko waliko? Kusini sasa hali imekuwa kama vita. vita vinavyojulikana vita vya gesi. kila kona Tanzania wanazungumzia. sasa wavamia ofisi za umma, mahakama zinachomwa moto, nyumba za wabunge zinateketezwa. hali ni tete. ni balaa. wanakusini sasa wamechoka na mfumo uliopo?

 Nasikia eti yule kiongozi mkuu wetu bwana Mkubwa yupo nchi za wenzetu kujadili masula ya nchi za wengine na kusahau vita baridi na ya moto iliyopo Tanzania. Hadi sasa hatujasikia mataifa makubwa duniani wakisema chochote. naamini wanasubiri iongezeka nao walete mandege kama yale ya mali ili kuwauwa wanakusini? Hapo ndipo watapoamini kwamba hali imekuwa tete? kw nini tusubili waingereza au Ufaransa wakileta yale madege? mungu ibaliki Tanzania.

Tusifike huko kwani mimi ni ni Mwanakusini ambao sipo tayari kuona Tanzania ivamiwe na wakoloni wale waliotutawala kama mali. Tujiulize nani wamesababisha haya. viongozi wetu wanahusikaje juu ya hili? je kauli zao zinaleta tija kwa wanakusini? kwa upande wangu naamini kauli za viongozi zinaweza kuleta vita au la kule kusini. hata Nchini Mali ilianza wa Mvutano kati ya serikali na wananchi hasa waasi. munakumbuka Misri ilikuwaje? ni jukumu lenu viongozi kuakikisha mapatano ya maridhiano ni muhimu zaidi kuliko tunakoelekea.

 Damu inayomwagika Kusini itadumu vizazi na vizazi kama mgogoro hautatatuliwa. Kwa wale waliofuatilia uasi wa Nigeria, na Sudani zote mbili wataona au waliona namna mafuta yalivyosababisha mtafaruku wa nchi. Vita visivyo na mwisho. Sipendi kuona kusini yangu inagawanywa na kuwa nchi nyingine? je itaitwaje? hili sio jambo jema. Hili jambo ni hatari. Serikali jamani kwanini musichukue hatua ya amani kuliko vita iliyoko sasa. Kwa kawaida umma unanguvu zaidi kuliko majeshi. Kwani ukiua wote kule kusini wataishi nani? maana pakifikia mahali watu wapo tayari kufa kwa ajili ya kutetea maslahi yao ona hapo pana jambo. njia pekee ni kukaa meza moja tu.
Hakuna jipya zaidi ya hilo. serikali ikubali imeshindwa vinginevyo inaweza kutokea yale ya Ludism kule wingereza miaka ya nyuma sana. Sasa serikali itumie Wanasaikolojia na wanasosholojia ambao ni wataalamu wa jamii yao ili kutatua mgogoro huu. naamini viongozi wetu watazuia ili ofisi na majumba yasichomwe moto kama Ludism.
HALI YA USAFIRI KUSINI
Hali ya usafiri kusini ni aibu. Unaweza kusema haijawai kuwa na Rais kutoka kusini. Pia utajiuliza hawa viongozi wa kule kusini wanafanya nini? Tuna wabunge wengi kweli kweli. Tunduru peke yake inawabunge wawili akiwamo Injinia Makani na Mtutura. Je hawa watu wa kusini Hasa Tunduru, Lindi na Mwata watafaidikaje na gesi iliyopo kusini? Baraara tangia uhuru haijajengwa. Ni wimbo wa Taifa wakati wa kampeni. Kuna kupindi walikuwa wanasafiri kwa kutumia meli lakini sasa bandari ilikufa tunaendelea kupata tabu ya usafiri.
Ukiwauliza viongozi wetu wameifanyia nini kusini watakujibu Tumejenga lile daraja kubwa nchini Tanzania ya Mkapa na ile ya Msumbiji. Inawezekana hawa viongozi wanapita kwa anga tu. Uangalie chini kuna nini unafili wataweza? Hali ni mbaya. Nawaomba mujalibu kutembelea kusini ukizunguka kuanzia Namtumbo, shuka chini hadi Tunduru, kasha usikae pale Tunduru teremuka hadi Masasi kasha pandisha hadi Hotel ya Nangurukuru Mkoani Lindi.
Sasa ukianzia hapo Nangurukuru kuelekea Daraja la Mkapa utaomba kama lingekuja wingi lizoe tope zote ziwekwe pembeni ili mupite kwa amani na utulivu. Kulala nchiani ni kawaida kule kwetu. Unapaswa uwe na Biskuti, ikiwezekana pika kabisa ugali au chukua unga na dagaa wakati wa kusafiri ili usife njaa maana gari likiingia kwenye tope mbona mutakesha.
Kwa kifupi hizo barabara nilizozitaja ni mbaya mno. Tangu uhuru hazijajengwa. Na madai ya hawa wanakusini wanasema iweje bomba la gesi lijengwe miezi 18 tu wakati barabara tangu uhuru bado?

No comments: