HOTUBA
NILIYOITOA TAREHE 21 DECEMBER 2012 JIMBONI KWANGU;
Waheshimiwa, viongozi
wa darasa Bugoya Ally I, na makamu wako Sara Samwel.
Waheshimiwa,
viongozi wa TEKUBA, mabibi na mabwana.
Awali ya yote
napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kudra juu ya
maisha mema.
Pole zangu
ziwafikie wenzetu woote waliofikwa na matatizo katika kipindi choote cha nyuma
hadi tulipo sasa.
Baada ya yote
napenda kutoa shukrani zangu za dhati sana kwenu nyote kwa kutosimamisha
mgombea mwingine yeyote katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu, Hii ni kuonyesha
imani mliyonayo juu yangu na nafasi ya uwajibikaji wangu ndani ya serikali ya
wanafunzi ya chou chetu, Ni uhakika wangu kuwa hamkufanya kosa kwani
nimehakikisha ninawatumikia wananchi wangu kwa kadri ya uwezo wangu na mamlaka
yanguu ndani ya ofisi ya bunge na pia hata katika ofisi ya wizara ya mikopo.
Ndugu zangu
nilipoteuliwa kushika nafasi ya kuwa naibu waziri wa pili wa mikopo nilijisikia
vizuri kwa sababu ni nafasi adhimu si kwa Tweve bali kwa kitengo chetu cha
elimu jamii, kwa maana hiyo basi sisi kama watu wa elimu jamii tunayo adhima
kubwa ya kuwatumikia wananchi kwani vyeo tulivyonavyo ni dhamana.
Salamu zangu za
pongezi ziwaendee pia BUGOYA ALLY I na SARA kwa kuchaguliwa kuwa viongozi wapya
wa darasa letu, kwani hadi sasa uongozi wao umefana na mimi kama mbunge ninatoa
kauli yangu kuwa hakuna kiongozi anayeweza kuonekana mzuri kwa watu wote pindi
anaposhika hatamu (uongozi)
Napenda kutumia
fursa hii kipekee sana kumshukuru Mh. Chiwambo na makamu wake Mote Dorothea
ambao ni wastaafu kwa sasa, utumishi wao ni mzuri na tena umetukuka, hongereni
sana.
Ndugu zanguni,
wanafunzi wenzangu, ilihali hatuwezi kukaa na makaa ya moto yakiwa mifukoni
mwetu ni lazima tufikie hatua ya kujadili baadhi ya mambo mahususi ndani ya
letu, ni wiki chache tu nilipotoa namba yangu ili watu waweze kutuma mambo
mbali mbali yanayohusu jimbo letu.
Ifahamike
kwamba ni matarajio yangu makubwa kuwa hotuba yangu haitokuwa kichochezi cha
kuwamega wanabaso wala kuwatenga kutoka kwenye umoja uliopo hivi sasa, Bali
hotuba hii fupi inalenga kuweka msingi wa umoja endelevu, ushirikano upendo na
mshikamano;
Ndugu zangu
nilitoa fursa hii ya kunitumia mambo mbali mbali kupitia njia ya simu kwani
mtiririko wa maswali ambayo pengine sikuwa na majibu yamezidi na huku mambo
niliyonayo ni mengi sana kwa hiyo nilishindwa kuyajibu na kuamua mkutano wa
pamoja ambao tunaufanya leo. MAMBO HAYA NI:-
v Mchango wa
TEKUBA ni mkubwa kiasi cha kuathiri utayari wa watu kuchangia kwa uhakika, na
hata katika michango hiyo inaonekana dhahiri kuwa madhumuni yamejikita katika
starehe na sio katika kusaidiana sisi kwa sisi na hata hivyo ni jukumu letu
sote kushiriki katika utoaji wa maoni ya katiba ya TEKUBA.
v Michango
inayohusu kufiwa ipewe kipaubele hasa kwa pale matatizo ya kufiwa yanapokuwa ni
very sensitive kwa muhusika wa tukio la kufiwa, na ikumbukwe kuwa wananchi
wanataka ufuatiliaji wa michango ufanyike chini ya uongozi unaotambulika na
unafahamika kwa wote na hata hivyo michango ya pongezi kama vile kwa mtu aliyejifungua,
na kutuma pongezi za aina yoyote ile ifanyike chini ya uhiari wa mtu na si
kufanya ulazima na kutangaziana matangazo kwa kuhimiza ulazima wake.
v Na kwa wale
wenye mashine/computer wafanyike msaada kwa wenzao na sio kufanya mashine kuwa
chanzo cha mapato ilihali hawafanyi biashara yoyote mfano mzuri ni pale mtu
anapoamua kuwatoza wenzake hela kubwa kwa kiasi cha zaidi ya Tshs 5000 na
katika hali ya kawaida hakuna kazi inayoweza kuchapwa kwa hela hiyo na hili
linaambatana na suala la kukataa kumwandika mtu jina ilihali yupo tayari
kuchangia hela ya kuprint kazi na kueleza kile kilichomfanya asiwepo katika
mchakato wa kufanya kazi hiyo.
Mwisho kabisa kwa mapenzi ya dhati kabisa
napenda kusisitiza kitu kwenu wenzangu kuhakisha kwamba tunakuwa watu wa mbele
kutembelea blog yetu ambayo mmiliki wake yundani yetu, mimi kama mbunge
ninachukulia kama ni blog yetu sote na ninajivunia sana kwani ni kitu cha
msingi kufanywa na mwenzetu mpendwa na ninaona ni mtu kwanza pengine kufanya
kitu kama hiki ndani ya kitenngo cha elimu jamii.
Aidha mimi kama
mbunge napenda kuwahimizeni nyoote kujiunga na Asasi ya umoja wa mataifa iliyo
na tawi lake hapa chuoni kwani ni muhimu kwetu kama watu wa elimu jamii.
NAWATAKIA
SAFARI NJEMA NA SIKUKUU NJEMA ZENYE BARAKA TELE, MUNGU IBARIKI BASO, MUNGU
IBARIKI TEKU, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
NINAOMBA
KUWASILISHA.
TWEVE NEHEMIA J
(MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA MIKOPO)
P O BOX 20,
NJOMBE,
TANZANIA.
ntweve@gmail.com
+255776047873