BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR
Chiwambo Asi R.
Zanzibar
mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia machafuko makubwa sana. Ikihusisha vitendo vya uchomaji wa
makanisa, uhalibifu wa mali
za umma, na wengine kuwekwa ndani. Hili si jambo tu la kukurupuka na kuanza
kubeza sana
upande mmoja kwani kila jambo ni matokeo ya mfumo Fulani.
Taasisi
iliyoingia kashfa hiyo ni Taasisi ya UAMSHO ikiwa chini ya baadhi ya waislamu Zanzibar. Zanzibar
wanataka nchi yao iwe huru, wakati watanganyika
tunataka Zanzibar
iendelee kuwa hru. Na cha kusikitisha zaidi lile baraza la usuruhisho masuala
ya muungano ni raia wa Zanzibar.
Hakuna Mtanganyika pale.
Ofisi
inayohusika na masuala ya muungano ni ofisi ya Makamu wa rais. Na hata walio
kwenye kamati hiyo wote ni Wazanzibar.
Hivi unadhani kama ikitokea wao hawautaki
muungano unadhani kwamba wataleta majibu yaliyo sahihi? Hawa ni viongozi wetu,
tuendelee kuwaamini kwani tushike ule usemi usemao kiongozi ni kioo cha jamii.
Makundi yeyote
yanavyoanzishwa huanza na Hatua (stage)
zake. Kila hatua inajitegemea kama ifuatavyo:-
- Hatua ya kwanza ya kuunda Kikundi. (Preliminary or incipiency stage). Hapa ndipo vichwa vya watu vinapogongana kimawazo juu ya kit Fulani kwenda tofauti. Viongozi hutokea ambao si rasimi na kuanza kuonesha hisia zao.
- hatua ya pili ambayo inahsisha kuanza kutengeneza kundi na kuongeza uelewa kwa watu (Coalescence stage). Hapa panahitaji viongozi ambao wataongeza ukaribu na watu wengine. Kipindi kingine wanazungumzia mawazo yao yote hata kupitia vyombo vya habari.
- hatua ya nne ambapo kikundi kimekomaa na kufikia kilele cha kundi (Institutionalization or Bureaucratization stage). Hapa viongozi wanakuwa ni wakuchaguliwa na ufata mfumo wa taasisi Fulani (chain of command). Na viongozi hao hulipwa kiasi cha fedha.
- Anguko. (Decline stage).hapa ni sehemu ya mwisho kabisa ambapo ni anguko ku la kundi lililoundwa katika hatua ya kwanza. Hapa kundi hili usambaratika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanikiwa kwa lengo lao, au kusambaratishwa.
Hizo ndizo hatua
za makundi yanavyotokea. Hivi viongozi wetu hawakuziona hatua kama
hizi? Kama kweli tunautaka muungano kwanini
serikali iliwaachia uhamsho kuendesha mijadala yake huku wakijua kuwa wanazidi
kulikuza zaidi kundi hili? Huu ni uasi au ni nini? Kwa upande wangu naona
kwamba ni uzembe wa watu wachache ndio uliopelekea visiwa vya Zanzibar kuingia kwenye machafuko.
Kwa kiongozi
yeyote aliyesomea masuala ya uongozi au jamiii lazima amezisoma hatua kama hizi na namna ya kuyasambaratisha haya makundi.
Kwanini zisitumike ikiwemo njia za amani. Makundi haya yalipata uchungu zaidi
pale viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali walipokamatwa na jeshi la polisi
katika eneo la bunge kwa madai kuwa ni kinyume na sheria za nchi kwa kifupi
nilivyoelewa mimi ni kwamba walikuwa waasi. Ni kweli kabisa.
Lakini ilipaswa
itumike busara kutatua mgogoro huu badala ya vitisho. Hawa Wazanzibar walianza
kudai Zanzibar ijitenge kwa muda wa miaka mingi sana. Kwa wale wenye
kumbukumbu munaweza kumkumbuka yle aliyekuwa rais wa Zanzibar Ndugu Aboud Jumbe
Mwinyi alivyotangaza nia ya kutaka kuvunja muungano akiwa Dodoma kwenye vikao Fulani. Kilichompata ni
kuondolewa klatika nafasi hiyo.
Nyadhifa zake
zote za kichama na serikali alivuliwa kufumba na kufumbua macho. Hii ni kweli
kuwa uasi ulianzia muda mrefu sana.
Hapo ndipo Mwalimu Nyerere aliposema kuwa tusikubali kuvunja muungano. Hata
Nyerere wetu kumbe aliyajua haya mapema hasa pale kundi la G51 lilivyoanza
kukua nchini Tanzania.
Kwa hiyo suala
la hawa jamaa wa UAMSHO chanzo chake kimetoka mbali. Kwa hiyo kwa wakati huu
ambao nchi mbalimbali zinaonyesha namna waasi wanavyoongezeka siku hadi siku,
hasa nchi zile za kiarabu na baadhi ya nchi za Kiafrika, napendekeza serikali
bora itumie busara zaidi katika kutatua tatizo hili badala ya vitisho na nguvu
nyingi. Kweli hawa watu wapo kinyume cha sheria za nchi.
Lakini busara
muhimu zaidi kuliko nguvu zaidi. Kwanini serikali isikae nao pamoja na kanza
kusikiliza madai yao?
Kama yana msingi kwa hatima ya nchi yetu
yafanyiwe kazi. Mbona madaktari ilitumika njia kama
hii. Kwanini isitumike kule Zanzibar.
Inasikitisha kuona kila kukicha vituko Zanzibar
mara tunataka nchi yetu.
Haya yamefugwa sana na sisi wenyewe
kwani viguvugu lilipoanza hasa katika ule muswada wa maoni ya katiba mpya hawa
walichana hadharani na kupinga kujadiliwa. Wakati ule likuwa muhimu kuweza
kutafta njia mbadala za kutatua ili kuonyesha namna tunavyoujali muungano wetu.
Nalipenda sana Tanzania
hasa hili jina zuri la Tanzania.
Kwa hiyo nadhani viongozi wa serikali mutatumia wawazo haya ili kuhakikisha
tunabaki na Tanzania moja,
Imara na yenye amani na utulivu kama
aliotuachia mwalimu Nyerere.
Powered by
Chiwambo Ausi R.