Dar es Salaam. Kesi ya kupinga maazimio ya Bunge iliyokuwa
ianze kusikilizwa leo imeahirishwa hadi siku ya kufunga mwaka Desemba 31, 2014.
Wiki iliyopita za kampuni za IPTL na Pan Africa Power
Solutions (T) Limited (PAP) kwa
kushirikiana na Harbinder Sighn Sethi zilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya
Tanzania kuomba zuio la muda la utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu
akaunti ya Tegeta Escrow.
Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni
Augustina Mwarija, Gadi Mjemas na Stella Mugasha jana ilipaswa kuanza
kusikilizwa lakini iliahirishwa baada ya mawakili wa upende wa Jamhuri kuomba
ahirisho ili waweze kujipanga.
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju aliiomba
mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa madai kuwa wao walichelewa kupata
maombi ya kampuni hizo hivyo walishindwa kuyasoma na kujibu.
Hivyo aliiomba mahakama kuiaihirisha kesi hiyo jana ili waweze kusoma na leo wawasilishe majibu
yao na kama upande wa pili na wenyewe utakuwa na cha kujibu watajibu ili Desemba 31,2014 isikilizwe.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,majaji wanaoisikiliza kesi
hiyo walikubaliana na maelezo hayo na kuiahirisha hadi siku hiyo ya Desemba
31,2014.
Chanzo: Mwananchi