Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akitangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Picha na Edwin
Mjwahuzi
Dar
es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri
ambayo yamewatupa nje mawaziri watano, kuwaingiza 10 wapya, kuwapandisha
manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara
zao kwenda nyingine.
Miongoni
mwa walioachwa katika mabadiliko yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Sefue jana, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
(Mazingira), Dk Terezya Huvisa ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa
Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge.
Wengine
walioachwa na wizara zao kwenye mabano ni Manaibu Waziri, Goodlucky Ole Medeye
(Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Gregory Teu (Viwanda na Biashara),
Benedict Ole Nangoro (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Philipo Mulugo (Elimu na
Mafunzo ya Ufundi).
Mawaziri
hao wanaungana na waliokuwa mawaziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi,
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, Dk Mathayo David na Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki ambao uteuzi
wao ulitenguliwa na Rais kutokana na matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Bunge
kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Balozi
Sefue alisema kuachwa kwa mawaziri hao ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Rais
Kikwete kuimarisha utendaji serikalini. Pia alisema mabadiliko hayo yametokana
na kuwapo kwa nafasi baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao na kifo
cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
“Rais
amefanya mabadiliko kwa mujibu wa Ibara ya 55 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kutekeleza wajibu huo,” alisema Balozi
Sefue.
Sura
mpya
Sura
10 mpya zilizoingia katika Baraza hilo ni pamoja na Dk Asha Rose Migiro aliyeteuliwa
kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani ambaye
anakuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Naibu wake, Kaika Saning’o
ole Telele ambaye ni Mbunge wa Ngorongoro.
Wengine
wapya ni wale walioteuliwa kuwa Naibu Mawaziri na wizara zao kwenye mabano,
Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (Fedha), Mbunge wa Viti Maalumu,
Pindi Chana (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Mbunge wa Peramiho,
Jenister Mhagama (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).
Pia
wapo Mbunge wa Serengeti, Dk Steven Kwebwe (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa
Mbozi Magharibi, Godfrey Zambi (Kilimo, Chakula na Ushirika), Mbunge wa Mufindi
Kusini, Mahmoud Ngimwa (Maliasili na Utalii) na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma
Nkamia (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).
Waliopandishwa,
kuhamishwa
Mbali
na Dk Mahenge, Rais Kikwete pia amewapandisha manaibu waziri wengine watatu
kuwa mawaziri kamili pasipo kuwahamisha wizara walizokuwa. Hao ni Saada Nkuya
Salum anayekuwa Waziri wa Fedha, Lazaro Nyalandu (Maliasili na Utalii) na Dk
Seif Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii).
Balozi
Sefue alisema Rais Kikwete amewahamisha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria,
Mathias Chikawe kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua nafasi ya Dk
Nchimbi, wakati aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi
amerejeshwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kuchukua nafasi ya
Nahodha. Dk Mwinyi aliwahi kuongoza wizara hiyo.
Wengine
waliohamishwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Ummy Mwalimu kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,
kuchukua nafasi ya Charles Kitwanga aliyehamishiwa Wizara ya Nishati na Madini
kuendelea na wadhifa huo. Kitwanga anachukua nafasi ya George Simbachawene
ambaye amehamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima amehamishiwa Wizara ya
Fedha kuchukua nafasi ya Janeth Mbene ambaye amehamishiwa, Wizara ya Viwanda na
Biashara kuchukua nafasi ya Teu. Amos Makalla amehamishwa kutoka Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwenda Wizara ya Maji.
Sefue
alisema mawaziri na manaibu waziri wapya wataapishwa leo saa 10 jioni Ikulu.
Chanzo: Mwananchi