Saturday, December 22, 2012

HOTUBA YA MBUNGE WA BASO MH. TWEVE NEHEMIA J.


HOTUBA NILIYOITOA TAREHE 21 DECEMBER 2012 JIMBONI KWANGU;
Waheshimiwa, viongozi wa darasa Bugoya Ally I, na makamu wako Sara Samwel.
Waheshimiwa, viongozi wa TEKUBA, mabibi na mabwana.
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kudra juu ya maisha mema.
Pole zangu ziwafikie wenzetu woote waliofikwa na matatizo katika kipindi choote cha nyuma hadi tulipo sasa.
Baada ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati sana kwenu nyote kwa kutosimamisha mgombea mwingine yeyote katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu, Hii ni kuonyesha imani mliyonayo juu yangu na nafasi ya uwajibikaji wangu ndani ya serikali ya wanafunzi ya chou chetu, Ni uhakika wangu kuwa hamkufanya kosa kwani nimehakikisha ninawatumikia wananchi wangu kwa kadri ya uwezo wangu na mamlaka yanguu ndani ya ofisi ya bunge na pia hata katika ofisi ya wizara ya mikopo.
Ndugu zangu nilipoteuliwa kushika nafasi ya kuwa naibu waziri wa pili wa mikopo nilijisikia vizuri kwa sababu ni nafasi adhimu si kwa Tweve bali kwa kitengo chetu cha elimu jamii, kwa maana hiyo basi sisi kama watu wa elimu jamii tunayo adhima kubwa ya kuwatumikia wananchi kwani vyeo tulivyonavyo ni dhamana.
Salamu zangu za pongezi ziwaendee pia BUGOYA ALLY I na SARA kwa kuchaguliwa kuwa viongozi wapya wa darasa letu, kwani hadi sasa uongozi wao umefana na mimi kama mbunge ninatoa kauli yangu kuwa hakuna kiongozi anayeweza kuonekana mzuri kwa watu wote pindi anaposhika hatamu (uongozi)
Napenda kutumia fursa hii kipekee sana kumshukuru Mh. Chiwambo na makamu wake Mote Dorothea ambao ni wastaafu kwa sasa, utumishi wao ni mzuri na tena umetukuka, hongereni sana.
Ndugu zanguni, wanafunzi wenzangu, ilihali hatuwezi kukaa na makaa ya moto yakiwa mifukoni mwetu ni lazima tufikie hatua ya kujadili baadhi ya mambo mahususi ndani ya letu, ni wiki chache tu nilipotoa namba yangu ili watu waweze kutuma mambo mbali mbali yanayohusu jimbo letu.
Ifahamike kwamba ni matarajio yangu makubwa kuwa hotuba yangu haitokuwa kichochezi cha kuwamega wanabaso wala kuwatenga kutoka kwenye umoja uliopo hivi sasa, Bali hotuba hii fupi inalenga kuweka msingi wa umoja endelevu, ushirikano upendo na mshikamano;
Ndugu zangu nilitoa fursa hii ya kunitumia mambo mbali mbali kupitia njia ya simu kwani mtiririko wa maswali ambayo pengine sikuwa na majibu yamezidi na huku mambo niliyonayo ni mengi sana kwa hiyo nilishindwa kuyajibu na kuamua mkutano wa pamoja ambao tunaufanya leo. MAMBO HAYA NI:-
v Mchango wa TEKUBA ni mkubwa kiasi cha kuathiri utayari wa watu kuchangia kwa uhakika, na hata katika michango hiyo inaonekana dhahiri kuwa madhumuni yamejikita katika starehe na sio katika kusaidiana sisi kwa sisi na hata hivyo ni jukumu letu sote kushiriki katika utoaji wa maoni ya katiba ya TEKUBA.
v Michango inayohusu kufiwa ipewe kipaubele hasa kwa pale matatizo ya kufiwa yanapokuwa ni very sensitive kwa muhusika wa tukio la kufiwa, na ikumbukwe kuwa wananchi wanataka ufuatiliaji wa michango ufanyike chini ya uongozi unaotambulika na unafahamika kwa wote na hata hivyo michango ya pongezi kama vile kwa mtu aliyejifungua, na kutuma pongezi za aina yoyote ile ifanyike chini ya uhiari wa mtu na si kufanya ulazima na kutangaziana matangazo kwa kuhimiza ulazima wake.
v Na kwa wale wenye mashine/computer wafanyike msaada kwa wenzao na sio kufanya mashine kuwa chanzo cha mapato ilihali hawafanyi biashara yoyote mfano mzuri ni pale mtu anapoamua kuwatoza wenzake hela kubwa kwa kiasi cha zaidi ya Tshs 5000 na katika hali ya kawaida hakuna kazi inayoweza kuchapwa kwa hela hiyo na hili linaambatana na suala la kukataa kumwandika mtu jina ilihali yupo tayari kuchangia hela ya kuprint kazi na kueleza kile kilichomfanya asiwepo katika mchakato wa kufanya kazi hiyo.
 Mwisho kabisa kwa mapenzi ya dhati kabisa napenda kusisitiza kitu kwenu wenzangu kuhakisha kwamba tunakuwa watu wa mbele kutembelea blog yetu ambayo mmiliki wake yundani yetu, mimi kama mbunge ninachukulia kama ni blog yetu sote na ninajivunia sana kwani ni kitu cha msingi kufanywa na mwenzetu mpendwa na ninaona ni mtu kwanza pengine kufanya kitu kama hiki ndani ya kitenngo cha elimu jamii.
Aidha mimi kama mbunge napenda kuwahimizeni nyoote kujiunga na Asasi ya umoja wa mataifa iliyo na tawi lake hapa chuoni kwani ni muhimu kwetu kama watu wa elimu jamii.
NAWATAKIA SAFARI NJEMA NA SIKUKUU NJEMA ZENYE BARAKA TELE, MUNGU IBARIKI BASO, MUNGU IBARIKI TEKU, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
NINAOMBA KUWASILISHA.
 

TWEVE NEHEMIA J (MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA MIKOPO)
P O BOX 20,
NJOMBE, TANZANIA.
ntweve@gmail.com
 +255776047873