Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia
raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba
wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora.
Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani
kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa
na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa
tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga
zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye
Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya
pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union
katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba
21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na
Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon
(Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu)
kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu)
ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina
Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale
JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini
Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja
wa Majimaji.
Mechi za kundi C kesho (Septemba 21
mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza),
Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT
itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba
22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment