Wapiganaji wa Boko Haram wamewaua
watu 87 katika shambulio katika Jimbo la Borno nchini Nigeria.
Mashahidi wanasema kuwa wapiganaji
hao waliteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha mnamo Jumanne usiku.
Shambulio hili limetokea siku chache
baada ya makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Boko Haram
Wanamgambo hao waliokuwa wamevelia
magwanda ya jeshi, waliweka vizuizi barabarani nje ya mji wa Benisheik na
kuwapiga risasi wale waliokuwa wanajaribu kutoroka.
Kwa mujibu wa taarifa za mashahidi ,
wapiganaji hao waliteketeza nyumba katika shambulizi hilo la Jumanne.
Kundi la Boko Haram, ambalo
linapigania linachosema ni taifa la kiisilamu nchini Nigeria, limekuwa likifanya
mashambulizi sawa na haya kuanzia mwaka 2009.
Jeshi linadai kuwa Agosti mwaka huu, kiongozi
wa kundi hilo Abubakar Shekau na naibu wake
Momodu Bama waliuawa , ingawa hakuna taarifa za kujitegemea kuthibitisha hilo.
Mawasiliano katika jimbo la Borno,
yamekumbwa na hitilafu, tangu mwezi Mei, wakati hali ya hatari, ilipotangazwa
katika jimbo hilo
na majimbo mengine mawili.
Lakini mashambulizi yameongezeka sana hivi karibuni tangu jeshi kuanza kukabiliana na kundi
hilo katika
maeneo yaliyoathirika zaidi.
No comments:
Post a Comment