Friday, October 11, 2013

Gazeti la “Mwananchi” kuingia mtaani Leo oktoba 11



Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, wachapishaji na wauzaji wa magazeti ya MWANANCHI, MWANASPOTI, na THE CITIZEN leo imetoa ufafanuzi katika mambo mawili, kuhusiana na tukio lililotokea hivi karibu. Kwanza ni gazeti lake mama la MWANANCHI ambalo halikuchapishwa wala kuuzwa kwa takribani majuma mawili kwa agizo la serikali. Kuhusiana na hilo, wamechukua fursa na kuongelea kuhusu KUREJEA KWA UCHAPISHWAJI WA GAZETI HILO na KUUSHUKURU UMMA kwa kuwa nao bega

KUREJEA KWA UCHAPISHAJI WA GAZETI
Kwa mujibu wa agizo la Serikali, kutochapishwa kwa gazeti la Mwananchi kunakwisha leo, na kuanzia kesho tarehe 11.10.2013 gazeti litakuwa mitaani kama kawaida. Kwa hiyo kuanzia kesho wasomaji wa gazeti hilo maarufu wataendelea kupata gazeti lenye habari za uhakika zinazojikita kwenye umahiri, uhuru, na weledi wa uandishi na uhariri.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw Tido Mhando, magazeti hayou yataendelea kusambazwa nchi nzima na kufika mapema kabisa kote, kupitia kwa mawakala na wauzaji wake walioenea kote Tanzania.

Kwa wapenzi wa gazeti la Mwananchi waliopo jijini Dar es Salaam, kesho watauziwa magazeti na waandishi wa gazeti hilo ambao kuanzia asubuhi watakuwa mtaani wakisherehekea uhuru wao kwa kukutana na wasomaji wao moja kwa moja.

PROMOSHENI YA CHOMOKA NA MWANANCHI
Kutochapishwa kwa gazeti la MWANANCHI kwa majuma mawili kulisababisha ile promosheni ya CHOMOKA NA MWANANCHI isimame kwa muda huo huo. Tido alichukua Fursa kuwajulisha wasomaji wake kwamba promosheni hii sasa inarudi tena na inaendelea kuanzia ilipokuwa imekomea.

Zawadi za shilingi milioni moja kila siku, na zawadi za magari mapya, zitaendelea kushindaniwa na kutolewa ili kutimiza ile ahadi yetu ya kutoa zawadi zenye thamani ya jumla ya shilingi 250,000,000/=.



PICHANI JUU:Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited(MCL)Tido Mhando akizungumza na waandishi wa habari jijini kuhusu kuanza uchapishaji leo wa gazeti la Mwananchi lililokuwa limefungiwa kwa wiki mbili.

Mkurugenzi wa Mwananchi, Tido Mhando akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kuanza kwa uchapishwaji wa gazeti hilo.
 

Thursday, October 10, 2013

TIDO MHANDO; Mwananchi haitarudi nyuma katika utendaji wake, Litaendelea kusimamia haki sheria na ukweli daima.

                                  
Tido Mhando


Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuchapisha magazeti ya mwananchi Bw Tido Mhando amesema licha ya kufunguiwa na serikali kwa kipindi cha wiki mbili haitarudi nyuma katika utendaji wake na kuahidi kuendelea kusimamia haki sheria na ukweli daima.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akiwa kaambatana na mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi Bw Denis Msaki ambapo amesema kwa kipindi cha majuma mawili wamepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 400.
Chanzo: ITV DAIMA

Chuji awekewa ulinzi wa kutisha Bukoba



BENCHI la Ufundi la Kagera Sugar, limeweka wazi kuwa limemwandalia ulinzi mkali kiungo wa Yanga, Athuman Iddi ‘Chuji’ wakati timu hizo zitakapocheza Jumamosi mjini Bukoba.

Yanga ambayo inasafiri leo Alhamisi kuelekea Bukoba ikiwa na kiungo wake Haruna Niyonzima aliyeunguliwa na nyumba yake hivi karibuni, imecheza mechi mbili nje ya Dar es Salaam dhidi ya Mbeya City na Prisons. Zote ilitoka sare ya bao 1-1.

Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mlage Kabange, aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Tahadhari yetu kubwa ambayo tutaingia nayo kwenye mchezo huo ni kuhakikisha Chuji (Athuman) hatembei.

“Kuna vijana watatu wameandaliwa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo ya kumwekea ulinzi mkali na kuhakikisha hapati nafasi ya kupiga zile pasi zake kwa (Mrisho) Ngassa wala (Simon) Msuva.

“Tunaamini kwa kufanya hivyo Yanga hawatatembea kabisa. Chuji amekuwa akitumika sana kuwachezesha Ngassa na Msuva, hata ukiangalia mechi walizoshinda mipira mingi imekuwa ikianzia kwake.”

Alifafanua kuwa wameifuatilia Yanga na kugundua inatengeza mashambulizi yake kupitia winga za kulia na kushoto ikiwatumia Ngassa na Msuva.
“Hata ukifuatilia matokeo yao katika ushindi wa mechi mbili zilizopita dhidi ya Ruvu na Mtibwa utabaini hilo. Chuji amekuwa akiwachezesha vizuri Ngassa na Msuva, lengo letu kumwekea Chuji ulinzi wachezaji watatu ni kwamba Ngassa pamoja na Msuva wasipate mipira, nafikiri tukifanikiwa kwa hilo tutakuwa tumewamaliza kabisa.”

Hata hivyo, Kabange amegoma kuweka hadharani majina ya wachezaji walioandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo.
“Hatuwezi kuwataja majina, nafikiri hii ni kama vita, huwezi kumpa mpinzani wako mbinu zako,” alisema.

Yanga itakuwa ikicheza kwenye Uwanja wa Kaitaba huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza msimu uliopita ingawa ilisawazisha makosa hayo na kulipa kisasi kwenye mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.
Bao la Kagera likifungwa na Themi Felix wakati Nizar Khalfan akifunga la Yanga.
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

CHICHARITO ATAJA SABABU KWA NINI ATAONDOKA MAN U



MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amesema anaweza kuondoka ManchesterUnited ili kusaka timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza. 


Mshambuliaji huyo anayefahamika kama Chicharito hapewi nafasi kubwa katika klabu ingawa mwezi uliopita aliifungia timu hiyo bao la ushindi katika Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One dhidi ya Liverpool na zaidi ya mechi hiyo alianza katika mechi nyingine moja tu, United ikifungwa nyumbani na West Brom.

Hernandez amesema kwamba wakati akiwa ana furaha kuchezea klabu kubwa kama hiyo, pia anataka nafasi zaidi za kucheza na anaamini anaweza kuwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza iwe Old Trafford au katika klabu yoyote.

"Nasotea hiyo [kuanza katika mechi zaidi],"alisema Hernandez akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Mexico, Deportes Telemundo.
"Nafanyia kazi hilo- kupata nafasi kikosi cha kwanza. Nafahamu kwamba kiwango changu uwanjani kitaniruhusu kutimiza lengo hilo siku fulani, aidha hapa [Manchester] au popote katika klabu yoyote.

"Naelekea kutimiza miaka minne hapa [Manchester United] na kweli, kama ambavyo wakati wote nimesema, nina furaha kuwa tayari nimechezea moja ya klabu bora duniani, nafanya vizuri kila siku kutafuta muda zaidi uwanjani,".

"Nahitaji kupewa nafasi zaidi kuonyesha uwezo wangu, kwa sababu kati yetu sote tunataka kutoa mchango wetu ili hii timu ishinde ubingwa,".
Hernandez amekuwa akisotea namba kikosi cha kwanza United kutokana na kuzidiwa kete na akina Wayne Rooney, Robin van Persie na Danny Welbeck, lakini Mmexico huyo amesema hiyo inaweza kuwa nzuri kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu England.

"Ushindani ndani ya timu wakati wote umekuwa mkubwa na ninafikiri hiyo inaisaidia timu kwa kiasi kikubwa, kwa sababu kuna wachezaji wengi bora ambao kila mmoja kati yao anataka nafasi kikosi cha kwanza,".

"Mazoezi na mechi zinazokuja zitatulazimisha kusimama imara kuisaidia timu kuimarika kwa vyote, kwa uchezaji binafsi na kitimu kwa ujumla,".
Chanzo: sportmail

BERGKAMP ATAKA KUREJEA ARSENAL KUPIGA KAZI



GWIJI wa Arsenal, Dennis Bergkamp ameelezea nia yake ya kujiunga na dawati la makocha la timu ya Arsene Wenger.


Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 44 alunga mabao 87 katika miaka yake 11 ya kuchezea Arsenal na amesema klabu hiyo ina nafasi maalum moyoni mwake.
Robert Pires amekuwa akisaidia kuendesha mazoezi katika Uwanja wa Gunners, London Colney na Bergkamp, ambaye aliichezea timu hiyo kuanzia mwaka 1995 hadi2006, anaweza kuungana naye.

"Hisia alizonazo Johan Cruyff kwa Barcelona, nami ninazo hizo hizo kwa Arsenal," Bergkamp aliiambia Telegraph.
"Nikiwa Arsenal ilikuwa babu kubwa. Wakati wote nafurahia. Sijawahi kuwa na siku mbaya humo. Ipo katika fikra zangu wakati wote. Ni sehemu ya malengo yangu kurejea huko.

"Naona kama naweza kuwa sehemu ya makocha. Nafurahia hiyo kazi, hususan kufundisha vitu binafasi kwa washambuliaji,".
Bergkamp alijipatia sifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka, ubunifu na maarifa ya kisoka alipokuwa Arsenal.

Mchezaji mpya ghali wa Arsenal, Mesut Ozil amekuwa akifananishwa na Mholanzi huyo, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi amesema kila mchezaji ni wa kipekee.
Sasa akiwa kocha Msaidizi wa Ajax, Bergkamp amevutiwa na mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu na kusema Ozil ni kipaji maalum.

"Pamoja na heshima zangu zote kwa wachezaji wengine wote wa Arsenal, nafikiri ni mmoja ambaye anaweza kutengeneza tofauti,"alisema.
"Wachezaji wengine ni wazuri katika kiungo. Lakini unahitaji mtu mmoja fulani wa kiwango cha juu ambaye anaweza kuhaha Uwanja mzima,". 
Chanzo: binzubeiry



Obama ataka suluhisho la bajeti haraka



 Rais Obama amesema yuko tayari kuzungumza na wajumbe wa chama cha Republican kuhusu kitu chochote, lakini baraza la wawakilishi linatakiwa kwanza lipitishe mswaada kuzifungua tena shughuli za serikali.


Rais wa Marekani, Barack Obama, ameonya kwamba viongozi wa dunia wana wasiwasi wabunge wa chama cha Republican nchini humo huenda wakauvuruga kabisa uchumi wa taifa na kuapa kutotetereka katika msimamo wake wa kutaka kiwango cha fedha Marekani inazoweza kukopa kulipa madeni yake kiongezwe bila masharti yoyote.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ikulu yake mjini Washington hapo jana, rais Obama amewataka wabunge wa chama cha Republican waache vitisho na waupigie kura muswaada wa sheria kuidhinisha fedha kwa ajili ya serikali, ambao ikiwezekana huenda ukapitishwa leo.

"Baraza la wawakilishi linatakiwa kupiga kura leo. Kama wanasiasa wa chama cha Republican na spika Boehner wanasema hakuna kura za kutosha. Basi wanatakiwa wathibitishe. Acha muswada upigiwe kura halafu tuone kitakachotokea. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba kuna kura za kutosha."

Boehner akataa kujisalimisha bila masharti
Spika wa bunge la Marekani, John Boehner, amesisitiza hakutakuwa na 'kujisalimisha bila masharti' kwa chama cha Republican. Boehner amesema bunge litairuhusu Marekani ikope fedha zaidi kama rais Obama atakubali kubana matumizi. Hata hivyo kulikuwa na ishara ya matumaini ya kuutanzua mgogoro mkali wa bajeti ambao umesababisha baadhi ya shughuli za serikali kufungwa kwa zaidi ya wiki moja na hivyo kuibua hofu kwamba Marekani huenda ikashindwa kulipa madeni yake kama kiwango hicho hakitaongezwa kufikia tarehe 17 mwezi huu.

Obama amesema kukiwa na haja atakubali makubaliano ya muda mfupi kuongeza kiwango cha fedha serikali inazoweka kukopa na kufungua tena shughuli zilizofungwa, hatua ambayo itauahirisha mkwamo huo kwa wiki kadhaa. Wakati huo huo, rais Obama amewashutumu wabunge wa chama cha Republican kwa kuutumia mkwamo wa bajeti kama chombo cha shinikizo kwa lengo la kuyahujumu mageuzi ya bima ya afya.

Wachambuzi wanasema hiyo ni mbinu mpya ya chama cha Republican kumbana Obama. Mwanauchumi Steven Ricciuto anasema, "Nadhani huo utakuwa mkakati wa chama cha Republican ambao kwa kiwango fulani unaweza kukubalika na Wamarekani; kwamba hupaswi kushindwa kulipa madeni. Lakini katika miswaada yote ya bajeti huenda kuna masharti yaliyofungamanishwa, ambayo huenda yakauendeleaza mkwamo uliopo."

Lakini rais Obama ameshikilia msimamo wake kwamba katu hatokubali makubaliano yoyote kuhusu kukakataa kuzikubali nadharia za chama cha Republican ili apate mamlaka zaidi kukopa fedha kugharamia kifedha majukumu ya Marekani. 

Obama amesema bunge lina kazi mbili za msingi - kupitisha bajeti na kuhakikisha Marekani inalipa madeni yake. Ameonya kwamba wabunge hawakudai walipwe fidia na kusisitiza msimamo wake kuwa atafanya mazungumzo na Warepublican mara tu kiwango cha fedha kitakapoongezwa na shughuli za serikali zilizofungwa zitakapofunguliwa.

Spika Boehner alijitokeza kwenye televisheni muda mfupi baada ya Obama kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari na kusema mazungumzo yatafanyika. Spika huyo pia ameukosoa msimamo wa Obama akisema sivyo serikali ya Marekani inavyofanya kazi. Obama ambaye alizungumza na Boehner hapo kabla kwa njia ya simu, anahoji kuongeza kima cha fedha serikali inazoweza kukopa ni muhimu kwa uaminifu wa taifa hilo kuweza kukopa fedha na hakupaswi kuvurugwa na wasiwasi wa kisiasa.

Mwanamke wa kwanza kuingoza benki kuu ya Marekani
Wakati mzozo wa bajeti ukiendelea, rais Obama leo atamteua Janet Yellen kama mwanamke wa kwanza kuiongoza benki kuu ya Marekani. Obama atampendekeza Yellen kwa awamu ya miaka minne kuchukua mikoba kutoka kwa Ben Bernanke, ambaye sera zake za miaka minane zilihusishwa na kukabiliana na mzozo wa kiuchumi ulioikabili dunia na kutafuta njia za kuufufua uchumi.

Afisa wa Marekani amesema tangazo hilo litafanywa katika ikulu ya Marekani leo usiku katika tukio litakalohudhuriwa na Bernanke, na hivyo kufungua mlango kwa mchakato wa kuthibitishwa katika nafasi hiyo. Yellen, mwenye umri wa miaka 67, amekuwa akishikilia nafasi ya pili ya uongozi wa benki hiyo.

Yellen alizaliwa New York na ameolewa na mshindi wa tuzo ya uchumi ya Nobel, profesa George Akerlof na ni mama wa profesa wa uchumi, Robert Akerlof. Alisomea uchumi katika chuo kikuu cha Brown na baadaye katika chuo kikuu cha Yale, ambako alipata shahada yake ya uzamili. Yellen amekuwa profesa katika chuo kikuu cha Havard na hivi karibuni katika chuo kikuu cha California, Berkeley, ambako mume wake pia hufundisha na kufanya utafiti.

Mwandishi: Josephat Charo



Rais Morsi kufunguliwa mashtaka Novemba



Aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Morsi aliyeng'olewa mamlakani atafunguliwa mashtaka mwezi Novemba tarehe nne.
Bw Morsi atashatakiwa kwa kosa la uchochezi na mauaji pamoja na wanachama kumi na wanne wa kundi Muslim Brotherhood.

Mashtaka hayo yanahusiana na mauaji ya waandamanaji saba wakati wa vurugu kati ya wafuasi wa upinzani na wafuasi wa Muslim Brotherhood nje ya ikulu ya rais mjini Cairo mwaka uliopita.

Kupinduliwa kwa bwana Morsi kumesababisha maandamano ya kupinga na kumuunga mkono kutoka kwa wafuasi na wapinzani na wafuasi wake na baadhi wameuawa na vikosi vya kijeshi.

Morsi atashtakiwa na viongozi wengine kumi na wanne wa vuguvugu la Brotherhood.
Amekuwa akizuiliwa katika eneo lisilojulikana tangu alipoondolewa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.

Mamia ya watu wanataka arejeshwe mamlakani na wengi wao wakiwa wafuasi wa vuguvugu la Brotherhood. Wengi wa wafuasi hao wameuawa kwenye makabiliano na vikosi vya usalama tangu Morsi alipong'olewa madarakani.

Zaidi ya watu hamsini walifariki kutokana na ghasia hizo siku ya Jumapili.
Mahakama ya rufaa mjini Cairo iliamua kuwa Morsi na wenzake 14 akiwemo Mohammed al-Beltagi na Essam al-Erian, wanaweza kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya uhalifu.

Wendesha mashtaka walitangaza kuwa mwezi jana walifunguliwa mashtaka ya uchochezi kuhusiana na ghasia nje ya ikulu ya Rais mjini Cairo.

 


Speech by Dr Slaa at The University of Samford, USA





Mr. President, the faculty, staff, students, invited guests and the public at large. Allow me to express my gratitude, for the cordial welcome at your lovely campus. It is one of a kind, and If I could, I would have stayed much longer to learn more on your success that I could take back to our young people. The environment and the surroundings are as beautiful as the people themselves. Along the way, I have met great people with great hearts, and I thank you for that

Likewise, receive greetings from the people of Tanzania. I was quite impressed with your level of research, and the homework you have done trying to know Tanzania, I was also particularly touched by some of you in the audience that knew the geography of my country; and even trying to challenge me . Mrs. Macquire, "People of Mto wa Mbu" are definitely proud of you for being such a good Ambassador. 
We thank you, and Tanzania needs more of you that will help in exposing it to the people of America

The Samford community, my journey has been long and tedious; I have travelled through hills and valleys of trials and tribulations. However, due to the need and challenges we face as a nation, physical fatigue of travel would not stop me from marching forward. I am determined to work with my countrymen to see our nation of Tanzania reach the Promised Land.

Tanzania is a great and rich country, with rich culture and rich people at heart. Her people have sent me on a study tour. They have sent me to learn the secrets of your success as a society

Tanzania is one of the most blessed countries on the face of the earth. It has abundance of natural wealth, and for those who understand the world history, know that the best game parks are in Tanzania. It is the place believed to be the cradle of mankind.
Tanzania is the home of Mt. Kilimanjaro, Serengeti national park, Ngorongoro crater, and Olduvai Gorge where the first man is believed to have lived. We have some of the world best beaches; our people are very hospitable and extremely welcoming. I welcome all of you to Tanzania

For a long time, Africa has been known as a dark continent infested with disease, poverty, starvation, illiteracy and never endings wars. This might have been created in your minds with the images in your televisions. I can't blame you, because this is the truth you know

However, this is far from the reality. Africa and Tanzania in particular is the new frontier. Tanzania is a country rich in natural resources and only lacks human capital. It is a country with rich land and plenty of water bodies
Many African leaders are believed to come to Washington and other western capitals begging for handouts known as foreign aid. This has created a notion in the minds of many that Africans are poor and lazy.

This is not the case.
Africa is transitioning from mismanagement, dictatorship and corruption that have plagued the continent. Corruption is the main vice depriving Tanzanians and other Africans a chance to a better education, better healthcare and economic prosperity.

Well, I am not here to beg, because my country is rich. I know clearly well that, foreign aid does not come cheaply. It comes with a condition of signing up our sovereignty
I am not here for foreign aid, and CHADEMA party which I represent does not believe on foreign AID. 

This is my party's philosophy, and any sane human being would not want to live off handouts, or going around begging because foreign aid is only needed as short term relief for countries coming out of calamities. Rwanda needed help to so it could emerge out of the ruins of genocide. Once it did, it became less interested on the foreign aid now a success economic story in Africa

Foreign aid is a form of slavery which creates a false sense of entitlement. It confines a beggar into a psychological and mental prison of his own creation, becoming incapable to make any meaningful decision of his own. He does not think on how to get out of his difficulties as long as he knows that, someone somewhere will help him.

CHADEMA party believes that all too often, foreign aid creates dependency by the receiving country onto the giving country and winds up in the pockets of corrupt rulers.
Foreign aid money are your taxes, your sweat which should work for your benefit not for people sitting on their wealth. More important than your dollars, are your brain trust, investments and technological advantage. This is what we need to utilize our resources and also in planning for years beyond our non-renewable resources

Our country rich in resources is being exploited by foreign entities, while our President is busy trotting the world begging for mosquito nets. With our resources, we can make our own mosquito nets without them being donated to us. Chadema party which I represent is poised to changed that, and the most important tool we need is the development of human capital

We need our resources to benefit our people. We need to create jobs for our people, we need to improve our health care, we need to improve our education, our infrastructures, communication and economy as a whole. And this is only possible if can with the wealth that we have all we need is better education for our people
We are currently having inequitable trade, where far eastern countries are exporting their poor populations to compete for jobs with our citizens. 

They are even exporting to us their prisoners to work on our roads yet millions of our young men have no jobs. This is not possible in any civilize society, unfortunately, because our rulers have signed contacts shrouded in secrecy whose contents are only known to them

Some of these individuals have turn to insult us as a nation. They are now interfering on our sovereignty, publicly aligning themselves with political parties. A whole ambassador standing on a political platform to address a political rally, and has ignored the public call for him to leave the country!

This is not the kind of trade we are looking for. We are looking for partners that will work with us to develop our resources in order to benefit our people; Partners that will bring to our country new skills, and also create jobs for our graduates. We need your expertise so we can turn our country into a bread basket of Africa. America is the world's land of milk and honey where everyone wants to be, that's the model we want to learn from

Well, we have come to realize, that if you feed us today with your milk and honey, our meals for tomorrow may not be guaranteed. We instead want to know how you made your country into a land of milk and honey so we can be able to feed ourselves for unforeseeable future and also feed the rest of the world. We have the potential but lack the expertise, and the know how is what we need

Tanzania is not an island; it is part of the global community where all humans have the liberty to visit whenever they want. Our boarders are open for all, as long as our laws and culture are respected. All we need is trade partnership that will guarantee fifty-fifty trade, in which the country benefits equally with the investor.

The younger American generation, I am inviting you to visit Tanzania; I am talking to you as the investors of tomorrow. Come and explore the endless possibilities my country has for you. We need investors that will bring into our country, a set of skills and creativity to turn our hardwood into high quality, made in Tanzania products, as opposed to bringing cheap furniture made of plywood while hauling away our valuable timber

Chadema party believes on the free market economic philosophy in which individual creativity is rewarded. We need your partnership in fostering individual innovation within our people. We don't need your tax money; neither do we need your mosquito net donations, we need your skills.

We don't need shoe boxes, we need to know how to make our own shoes. We need your technological know how
CHADEMA party's priority number one is education! Priority number two is education and so is the priority number three.

We believe on education to be the only way for Tanzania to rise from the abject poverty it is in today. We have no alternative but train our young people who will in turn, employ their intellectual creativity into full practice to enable Tanzania become an economic giant in a continent long forgotten

Samford is one of the American's finest educational institutions. It is producing some of the world finest, from school teachers to the finest lawyers. It is my hope that we see your institution open its doors to our support and in preparing Tanzania's aspiring scientists, teachers, and accountants to become innovators.

In our effort to make our country a unique success story, I am challenging you the young people to go out to the world, and open new trails for others to follow. Tanzania has its doors open for you

Thank you all for listening.
Source: http://www.wavuti.com

Asilimia 50 ya marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi hapa nchini, ni wa kigeni.




Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesema ajira ya marubani wazalendo ipo mashakani kwa sababu ndege nyingi nchini, zinaongozwa na wageni.TCAA imesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa na kampuni zinazotoa huduma hizo nchini, kutumia ndege nyingi za kukodi zinazofanya kazi chini ya masharti yanayotoa nafasi kubwa ya kuongozwa na marubani wa kigeni.

"Ndege ni ghali sana na wengi walioko kwenye sekta hii wanakopeshwa na kupewa masharti,"alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhili Manongi, alipokuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti hili.

Alisema karibu asilimia 50 ya marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi hapa nchini, ni wa kigeni.
Manongi alisema ingawa mikataba kuwabana, kigezo cha uzoefu pia ni kikwazo kwa marubani wengi wazalendo.

"Wengine wanashindwa kupata ajira kutokana na kutokuwa na saa zinazohitajika ili mtu aweze kurusha ndege za biashara," alisema.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa sasa Tanzania ina marubani 500 na katika miaka mitatu ijayo watafikia 700.

Alisema kwa jumla sekta ya usafiri wa anga ina upungufu wa wataalamu kama wahandisi na marubani lakini shida kubwa inawahusu zaidi marubani.

Manongi alisema kwa kuzingatia hali hiyo, TCAA ipo kwenye mikakati ya kuboresha sekta ya marubaini nchini ili pamoja na mafunzo, pia wapate uzoefu utakaowawezesha kutoa ushindani kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA






Na Gladness Theonest
Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo,wakati akizungumza na wanafunzi waliokosa mikopo ambapo kwa takriban wiki nzima wamepiga kambi wizarani hapo.

"Kasungura kadogo na mkumbuke kuwa mkopo ni kuomba kuna kupata na kukosa...hivyo wale waliokosa na walikuwa na vigezo watafute watu wengine wenye uwezo wawasomeshe kwa mwaka mmoja na unaofuata watume tena maombi," alisema.
Alisema kilio chao amekisikia na leo atazungumza na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusiana na malalamiko yao ambapo suala hilo litapelekwa Bungeni ili kujadiliwa.

"Kama Bunge litaamua kupunguza fedha kutoka kwenye bajeti zingine ili kusomesha wanafunzi hao. Bunge litaamua kwani Serikali ina nia nzuri sana kwani hadi sasa imetoa trilioni 1.5, lakini ndugu zenu hawarudishi," alisema.

Alitaja sababu nyingine ya wanafunzi kukosa mikopo ni Serikali kuangalia uhitaji, kwani kuna masomo maalumu walilenga hasa fani zenye upungufu wa wataalamu.
Alitaja fani hizo kuwa ni ualimu, udaktari na wahandisi. Alitaja sababu nyingine za wanafunzi kukosa mikopo hiyo ni waombaji kukosea majina na vitu vingine vidogo vidogo na walipotangaziwa kwenye vyombo vya habari warudi kurekebisha fomu zao hawakufanya hivyo.

Alisema waliokosea kujaza fomu hizo walikuwa 6,000 lakini waliorudi kufanya marekebisho walikuwa ni 3,000 na wengine 2,000 walikuwa na vigezo lakini wamekosa kutokana na sungura kuwa mdogo (bajeti).

Wanafunzi waliokosa mikopo walisema kama wenzao wameweza kupata mikopo kwa asilimia 100 basi waangalie namna ya kugawana ili wote waweze kupata


Share on facebook:CHANZO MAJIRA

 


TAZARA YAPATA VICHWA SITA VYA TRENI




Madereva na Mafundi wa Treni za TAZARA wakiwa katika moja ya vichwa sita vipya vya Treni ambavyo vimeletwa Tanzania na wapo katika mafunzo ya jinsi ya kuvitumia. (HM)

SHIRIKA la reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) limepata vichwa sita vya Treni vipya kutoka nchini China vyenye uwezo wa kubeba tani 1800 kila kimoja.
Kufuatia kutolewa kwa vichwa hivyo vya Treni vipya, madereva 160 na mafundi 80 wa karakana ya Treni Iyunga mkoani Mbeya wanapatiwa mafunzo yakakayo wawezesha kufanya kazi kwa umakini katika vichwa hivyo.

Akitoa maelezo ya ujio wa vyicho hivyo Mhandisi Mwandamizi katika karakana na Iyunga Eng. Davie Tembo alisema kuwa vichwa hivyo vya treni vyenye uwezzo wa kubeba Tani 1800 vimeletwa Juzi katika karakana hiyo.

Alisema kuwa vimetoka nchini china na ni toleo jipya ambalo linahitaji madereva na mafundi kujifunza kabla ya kuanza kutumia kwani linatumia mfumo mpya.
Tembo alisema kuwa kampuni ya CSR Qishuyan ya nchini China ndio iliyo tengeneza vichwa hivyo na inatoa mafunzo kwa madereva na mafundi jinsi ya kuvimudu vichwa hivyo.

Alisema kuwa wamevijaribu vichwa hivyo na kuviona vinafaa kwa matumizi na havina shida yoyote.
Awali akifungua mafunzo kwa madereva hao Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA, Said Sauko alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga kwa Wafanyakazi wa TAZARA watakao kuwa katika makundi saba ambapo kila kundi litakuwa na watu wasio pungua 40.

Alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa mwezi mmoja na yamelenga kwa wafanyakazi kutoka Tanzania na Zambia. Chanzo: Furahia Eliab, Mbeya

SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI.

Na. Aron Msigwa, Iringa


Wakati maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa yakiingia siku ya tatu mkoani Iringa Serikali imewahakikishia vijana kuwa itaendelea na mkakati wake wa kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha na kuondokana na umasikini.

Akizungumza na Vijana wanaoshiriki maadhimisho hayo mkoani Iringa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makala amesema kuwa serikali katika kuhakikisha inatimiza lengo hilo kwa kuanzia imetenga kiasi cha shilingi bilioni 6.1 katika bajeti ya mwaka 2013/2014 ili kuwawezesha vijana kote nchini.

"Jambo hili la kuwawezesha vijana tunalipa uzito mkubwa na kwa kuanzia katika bajeti ya mwaka huu tumetenga kiasi cha shilingi bilioni 6.1 kuwawezesha vijana, ni mwanzo mzuri pamoja na kuwa tunahitaji kufanya zaidi" amesema

Amefafanua kuwa kiasi hicho cha fedha kitatolewa kwa vijana walioamua kujishughulisha na wenye mawazo ya kujikwamua kiuchumi na kuwataka vijana kote nchini kutumia fursa ya mikopo wanayopata kuitumia katika kufanya shughuli za maendeleo.

"Nawaomba vijana muepuke kutumia fedha hizo katika anasa na mambo mengine yasiyokusudiwa yanayowafanya mjikute mmeingia katika matatizo ya madeni na kuendelea kuwa maskini" amefafanua

Hata hivyo amesema serikali kwa kuliona jambo hilo imeandaa mpango wa kuwapatia elimu vijana ili waweze kuzitumia ipasavyo fursa za maendeleo zilizopo na waweze kujiandaa kunufaika na kiasi hicho cha fedha zilizotengwa pia inafanya jitihada za kuboresha vyuo vya vijana pamoja na kuongeza idadi ya walimu wa vyuo hivyo.

"Nataka niwahakikishie kuwa serikali inaendelea kuviboresha vyuo vyetu vya ndani ikiwa ni pamoja na kushirikiana na nchi marafiki ambapo kwa kushirikiana na Afrika ya Kusini tunaandaa utaratibu wa kupeleka walimu wetu ili waweze kusoma huko na kuja kufundisha vijana katika vyuo vyetu" amesema.

Mh. Makala ameongeza kuwa tayari serikali katika kushughulikia tatizo la ajira hasa kwa vijana wanaohitimu masomo ya elimu ya juu kwa kuzungumza na baadhi ya taasisi za fedha zikiwemo benki za NMB, EXIM Bank na CRDB ili ziweze kutoa mikopo kwa vijana hao kwa dhamana ya vyeti vyao na kubainisha kuwa tayari baadhi ya benki zimekwisha anza zoezi la kuwakopesha vijana kwa kutumia dhamana ya vyeti vyao.

Aidha kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Vijana kitaifa amesema kuwa inatokana na uamuzi waserikali uliofanyika mwaka 1999 mjini Dodoma wa kuhakikisha kuwa kila mwaka vijana wanapata fursa ya kujumuika pamoja katika maadhimisho hayo.

Aidha amewashukuru viongozi wa mkoa wa Iringa kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya ya kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara ya Habari Vijana , Utamaduni na Michezo kuhakikisha kuwa shughuli za Wiki ya Vijana na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru tarehe 14/10/2013 zinafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

"Sisi kama viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tunawashukuru sana viongozi wa Iringa kwa ushirikiano mlioutoa katika kufanikisha shughuli hizi za Wiki ya Vijana kitaifa, na ni matumaini yetu kuwa tarehe 14 mwezi huu wananchi wengi zaidi watajitokeza katika kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2013" amesema Mh. Makala.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwafanya vijana kujitambua na kuwakumbusha kuzitumia fursa za kimaendeleo zilizo katika maeneo yao kujiletea maendeleo.

Amesema katika maadhimisho ya mwaka huu licha ya kuwepo kwa maonyesho ya bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini vijana watapata fursa ya kujadili mada mbalimbali katika midahalo ikiwemo mada ya kuujua mkoa wa Iringa na fursa za kimaendeleo na ajira zilizopo katika mkoa wa Iringa, pia huduma za hifadhi ya jamiii na maendeleo ya vijana,nafasi ya vijana wa Tanzania katika kutunza amani na upimaji wa hiari wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma amesema kuwa mkoa wa Iringa utaendelea kutoa msukumo kwa vijana ili waweze kujiletea maendeleo kutokana na fursa zilizopo ndani ya mkoa huo.

Ameongeza kuwa mkoa huo kwa muda mrefu umekuwa na jukumu la kuwaandaa vijana kuwa watu wanaojitegemea, kuwa viongozi na watoa maamuzi sahihi, wajasiriamali na wazazi wanaowajibika na kuongeza kuwa serikali ya mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kutoa elimu kwa vijana kuhusu uzazi salama, ujasiriamali na kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

Dkt. Ishengoma ameeleza kuwa mkoa wa Iringa umeanzisha mfuko wa kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mikopo na mitaji ya kuendesha miradi midogo midogo ya kiuchumi na kuondoa tatizo za utegemezi na tayari vikundi vipatavyo 70 katika halimashauri za mkoa wa Iringa katika mwaka 2012/2013 vimepatiwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 116.

Waziri mkuu wa Libya Zaidan aachiliwa



Waziri mkuu wa Libya ameachiliwa saa chache baada ya kutekwa nyara na watu wanaominika kuwa wapiganaji wa kiisilamu. Hii ni kwa mujibu wa serikali ya Libya.
Ali Zeidan alitekwa nyara na kundi la waasi waliokuwa na uhusiano na serikali kwa jina Revolutionaries Operations Room.

Walisema walimteka nyara kwa maagizo ya mwendesha mkuu wa mashtka ingawa wizara ya sheria imekanusha madai hayo.
Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi ya wapiganaji walioghadhabishwa na hatua ya makomandao wa Marekani kumkamata Anas Al-Liby mshukiwa wa kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Wengi walitaja hatua ya Marekani kama ya kuingilia uhuru wa taifa hilo na kata kutaka maelezo kutoka kwa balozi wa Marekani nchini humo.
Mwandishi wa BBC mjini humo anasema Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.

Serikali imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kali baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa al-Qaeda Anas al-Liby nchini Libya.
Bwana Liby alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.

Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.
Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.

Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.

Taylor kutumikia kifungo Uingereza



Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor atatumikia kifungo chake cha miaka 50 jela nchini Uingereza baada ya kupatikana na hatia ya uhalifu wa kivita.
Haya ameyasema waziri wa sheria nchini Uingereza Jeremy Wright.

Sweden na Rwanda pia zilikuwa zimeomba kumfunga jela Taylor katika ardhi yao baada ya rufaa yake kukataliwa na mahakama mwezi jana.
Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sierra Leone, mjini Hague.

Iliamua kuwa makosa dhidi yake yalithibtishwa bila tashwishi.
Alihukumiwa jela mwaka 2012 kwa kuwasidia waasi waliofanya maasi makubwa dhidi ya watu wa Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Taylor, mwenye umri wa miaka 65, alipatikana na hatia ya kuwapa waasi wa Revolutionary United Front silaha na wao wakimpa almasi kutoka Sierra Leone.

MAGAZETINI LEO ALHAMISI 10-10-2013 NA Chiwambo's Blog