Saturday, September 21, 2013

Mbeya City Timu Inayong'aa waambiwa Karibu Dar es Salaam


 

UKIWA unapita Barabara ya Morogoro, labda unatoka Arusha, Morogoro, Iringa au Mbeya, ukishaumaliza Mkoa wa Pwani, utakutana na bango kubwa barabarani limeandikwa ‘Karibu Dar es Salaam’.

 Kama hiyo haitoshi utakutana na mabango mengine madogo madogo yakisomeka “Sasa umeingia Dar es Salaam’.
Baada ya Mbeya City kuwa vidume katika Mkoa wa Mbeya na hata kuikomalia Yanga, sasa si vibaya kama tukiikaribisha timu hiyo jijini Dar es Salaam kwa kusema “Karibu Dar es Salaam’.

Mbeya City wameingia Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu waanze Ligi Kuu Bara.
Kila kona ya Dar es Salaam na Tanzania wanaizungumzia mechi yao dhidi ya Simba leo Jumamosi itakayopigwa Uwanja wa Taifa.

Licha ya kuwa imeshacheza mechi nne za awali, mashabiki wanaamini kuwa wikiendi hii ndiyo Mbeya City wanaanza ligi kwa kucheza mechi ya kwanza ngumu zaidi nje ya mkoa wake na ndani ya Dar es Salaam tena dhidi ya timu ngumu ya Simba.
Mbeya City ilishangaza wengi kwa kutoka sare ya bao 1-1 na mabingwa watetezi Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine, wikiendi iliyopita mjini Mbeya kabla ya kulazimisha suluhu dhidi ya Mtibwa mjini Morogoro Jumatano wiki hii.

Mambo hayo yameongeza mvuto na hamasa kwa mashabiki kwenye mechi dhidi ya Simba, ambayo imebatizwa jina la ‘Karibu Dar es Salaam’.
Mbeya City iliingia Mkoa wa Pwani juzi Alhamisi na kupiga kambi ya muda kabla ya jana Ijumaa mashushushu wake kuanza kutua Dar es Salaam na baadaye wakafuatiwa na timu yenyewe.

Kocha Juma Mwambusi amesisitiza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini amewatengeneza kisaikolojia wachezaji wake kukabiliana na presha ndani na nje ya uwanja na wanaamini watapata matokeo mazuri.

Straika msomi na hatari wa Mbeya City aliyemfunga Ally Mustapha ‘Barthez’, Mwagane Yeya amepania kumtungua, kipa wa Simba, Abel Dhaira na kuandika historia katika Ligi Kuu Bara. Kiungo wa Mbeya City, Steven Mazanda amesema lazima wawafanye kitu mbaya Wekundu hao wa Msimbazi.

Mbali na tambo hizo za wachezaji, mashabiki wa Mbeya City kutoka Mbeya, wamesema watafurika kwa wingi Uwanja wa Taifa kuishangilia timu yao.
Yeya, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Iduda Uyole, aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Mbeya City ni vijana wa kazi, kwetu matokeo ni jambo la mwisho. Lakini malengo yangu ni kuhakikisha napigana, kama niliweza kumfunga, Barthez hata Dhaira (Abel) atafungika tu.”

Straika wa Simba, Tambwe Amisi amesisitiza kuwa ameshazitambua klabu za Tanzania na sasa inamuwia rahisi kukabiliana na mabeki.
Mchezaji huyo amesisitiza kuwa haijui Mbeya City lakini anaamini hakuna timu ambayo haifungiki huku kocha wake msaidizi, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ akisema; “Simba imekamilika, vijana wako fiti sana na ni vipigo tu, hatuangalii jina la timu wala ushabiki sisi tunataka pointi tu.”

HOFU YA KIPIGO
Wachezaji wa Mbeya City wamekuwa na hofu kubwa huenda mashabiki wa Yanga wakawafanyizia kulipa kisasi cha basi lao kuvunjwa kioo wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Lakini hofu yao nyingine ni kucheza kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa, ambao una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 tena na timu ambayo imeshinda mabao 6-0, Jumatano.

JEZI ZA MBEYA CITY
Kwa wauzaji wa jezi ni kwamba, jezi za Mbeya City ni dili kubwa jijini Mbeya na watu wanazishambulia kuliko za Simba na Yanga. Mbeya City klabu mpya, imejizolea wapenzi wengi wa soka na robo tatu ya watu wa Mbeya wanaishabikia klabu hiyo mpya ya Ligi Kuu Bara.

Mwanaspoti ilipita katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya na kujionea uuzwaji wake. Mmiliki wa duka la vifaa la Mbaspo, Salum Haroun alisema: “Jezi za Mbeya City hapa ni dili kubwa. Hapa dukani kwangu zimeisha na watu wanaziulizia sana, ukileta tu hazikai.”

Naye mchuuzi wa barabarani, Jastine Kisongi alisema: “Asikwambie mtu, kwa sasa jezi za Mbeya City ndiyo zina dili hapa Mbeya, ukiwa nazo una uhakika wa kuuza tofauti na hizi za Simba na Yanga.”

MECHI ZA LEO JUMAMOSI
Mgambo vs Rhino
Prisons vs Mtibwa
Kagera vs Ashanti
Simba vs Mbeya City
Chanzo: Mwanaspoti

87 wauawa na Boko Haram Nigeria




Wapiganaji wa Boko Haram wamewaua watu 87 katika shambulio katika Jimbo la Borno nchini Nigeria.
Mashahidi wanasema kuwa wapiganaji hao waliteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha mnamo Jumanne usiku.

Shambulio hili limetokea siku chache baada ya makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Boko Haram
Wanamgambo hao waliokuwa wamevelia magwanda ya jeshi, waliweka vizuizi barabarani nje ya mji wa Benisheik na kuwapiga risasi wale waliokuwa wanajaribu kutoroka.

Kwa mujibu wa taarifa za mashahidi , wapiganaji hao waliteketeza nyumba katika shambulizi hilo la Jumanne.

Kundi la Boko Haram, ambalo linapigania linachosema ni taifa la kiisilamu nchini Nigeria, limekuwa likifanya mashambulizi sawa na haya kuanzia mwaka 2009.
Jeshi linadai kuwa Agosti mwaka huu, kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau na naibu wake Momodu Bama waliuawa , ingawa hakuna taarifa za kujitegemea kuthibitisha hilo.

Mawasiliano katika jimbo la Borno, yamekumbwa na hitilafu, tangu mwezi Mei, wakati hali ya hatari, ilipotangazwa katika jimbo hilo na majimbo mengine mawili.
Lakini mashambulizi yameongezeka sana hivi karibuni tangu jeshi kuanza kukabiliana na kundi hilo katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Friday, September 20, 2013

VINARA SIMBA KUWAKABILI MBEYA CITY VPL



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).

Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.

Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

 

VINARA SIMBA KUWAKABILI MBEYA CITY VPL



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).

Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.

Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

 

Jaji Mutungi aiumbua CCM



HATIMAYE Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameanza kuonyesha makali, baada ya kukipa onyo kali Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukitaka kuacha mara moja kutumia viongozi wa kidiplomasia kwenye shughuli za kisiasa.

Hatua ya Jaji Mutungi, imekuja siku chache baada ya CCM kumtumia Balozi wa China, Dk. Lu Youping katika shughuli za kisiasa mkoani Shinyanga wiki iliyopita.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana, ilisema suala la ushiriki wa raia wa kigeni ikijumuisha wanadiplomasia katika shughuli za kisiasa nchini, halikubaliki.

Alisema ofisi yake, inaunga mkono kwa dhati hatua iliyochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kukemea jambo hilo.

"Tamko la Serikali limezingatia sheria na wajibu wa wanadiplomasia, wakati wa uwepo wao hapa nchini, mimi nikiwa mlezi wa vyama vya siasa, ninakemea kitendo cha CCM kumshirikisha Balozi wa China katika shughuli za kisiasa," alisema Jaji Mutungi.

Alisema katika tukio hilo, CCM kuruhusu raia wa kigeni kutumia jukwaa lake ni dhahiri limezua hali ya taharuki kwa wananchi, japo sheria ya vyama vya siasa kwa upande wake iko kimya katika suala hilo.

"Naviasa vyama vya siasa kwa ujumla wake, kuzingatia na kufuata sheria na taratibu stahiki katika utekelezaji wa shughuli zao za kisiasa.

"Napenda kuujulisha umma kwamba, ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa wakati huu ipo kwenye mchakato wa marekebisho ya sheria husika ya vyama vya siasa, ambayo imebainika kuwa na upungufu....lengo ni kukabiliana na changamoto zilizopo likiwemo suala hili," alisema Msajili, Jaji Mutungi katika taarifa yake aliongeza sasa hivi ofisi yake inaendelea kukusanya maoni ya wadau katika jitihada za kufanikisha marekebisho ya sheria hiyo.

Suala la CCM kumshirikisha Balozi wa China katika masuala ya kisiasa, lilizua mjadala mkubwa hali iliyosababisha CHADEMA kutoa tamko na kuandika barua ya malalamiko UN wakitaka aondolewe kwa kupoteza sifa za kuwa balozi, baada ya kuvunja mkataba wa Umoja wa Mataifa wa 1961 unaosimamia nchi na nchi.

CHADEMA waliandika barua nyingine kwenda Serikali ya China na Tanzania, wakitaka msimamo na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya balozi huyo kuvunja mkataba huo ibara ya 41(1-3), kinachokataza balozi kujihusisha na siasa katika Taifa ambalo yuko.

Chadema imesema inalaani kitendo hicho na itachukua hatua kwenda Umoja wa Mataifa na pia kupata maelezo toka Serikali ya China kama imemtuma balozi huyo kujihusisha na mambo ya siasa za ndani za vyama au kuiwakilisha nchi.

Akijibu tuhuma hizo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema alichofanya balozi huyo ni kitendo cha kuungwa mkono, maana alikuwepo kwa nia ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa zao la Pamba katika Mkoa wa Shinyanga.

Alisema uwekezaji kutoka China, utasaidia kuondoa tatizo sugu la ajira, kupanda kwa bei ya zao la pamba ambacho kimekuwa kilio kikubwa cha wakulima pamoja na ujengwaji wa viwanda vya nguo na kuchuja mafuta.

Hivyo ni vema kumpongeza balozi huyo na kuunga juhudi za CCM za kuwatafuta wawekezaji wa nje, badala ya kusingizia uvunjaji wa Mkataba wa Vienna ili kupata umaarufu wa kisiasa:
chanzo mtanzania

MAGAZETINI LEO IJUMAA TAREHE 20-09-2013






HATIMAYE Tanzania imewekwa kando rasmi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)



HATIMAYE Tanzania imewekwa kando rasmi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika kuunda Shirikisho la Kisiasa litakaloziongoza nchi hizo. (HM)

Tayari marais wa nchi hizo, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamekwishafikia makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC, bila kuishirikisha Tanzania.

Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki, yalifikiwa Septemba 12 mwaka huu, mjini Kampala na marais wa Rwanda, Kenya na Uganda na hivi karibuni Rais wa Burundi ambaye alialikwa katika mkutano huo na kushindwa kuhudhuria, naye sasa amethibitisha ushirika wake katika shirikisho hilo jipya.

Gazeti la The Sunday Times la Rwanda, limemnukuu Waziri Musoni kuwa marais wa nchi hizo wamekubaliana kukamilisha rasimu hiyo ndani ya muda mfupi.

Musoni ambaye alikiri kushiriki katika mkutano wa marais hao ulioshirikisha pia maofisa waandamizi wa nchi hizo isipokuwa Tanzania, alisema uamuzi uliofikiwa katika mkutano huo ambao ni wa pili kufanyika, ni moja ya maagizo ya uamuzi uliofikiwa kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika pia mjini Kampala.

"Tumekubaliana juu ya kanuni za kisheria na mpango mzima utakaotuongoza ili kupata Rasimu ya Katiba itakayoliongoza shirikisho hilo la kisiasa," alikaririwa Musoni.

Alieleza kuundwa kwa kikosi kazi maalumu kitakachojulikana kwa jina la High Level Task Force (HLTF), ambacho kitajumuisha wataalamu wa nyanja mbalimbali watakaoandika Rasimu hiyo kwa namna ile ile ya ulivyoandaliwa mpango wa Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Musoni alisema mawaziri wa nchi wanachama waliopangiwa kushughulikia shirikisho hilo, wanatarajiwa kuelezea mwelekeo wa mafanikio ya mpango huo katika mkutano mwingine uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba huko Kigali Rwanda.

Kwa mara ya kwanza, marais Kagame, Museveni na Kenyatta walikutana kufikia makubaliano ya kuharakisha uundwaji wa shirikisho la kisiasa kwa nchi zao kwa kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuweka hati ya vitambulisho vya pamoja na ushirikiano wa kibiashara sambamba na kuzindua mradi wa ujenzi wa gati ya Bandari ya Mombasa.

Waziri Sitta ashangaa
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, alipoulizwa kuhusu hatua ya nchi hizo kuanza kuitenga Tanzania kuelekea kwenye Shirikisho la Kisiasa, alisema Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ibara ya 7 (e) ya mkataba inaruhusu nchi wanachama kufanya jambo la haraka kama nchi nyingine zinachelewa kufanya hivyo.

Sitta alilieleza Jumatano kuwa, taratibu za Tanzania haziruhusu kibali cha utambulisho kutumika katika nchi zote wanachama, kwa sababu lazima raia wa nchi wanachama anapoingia Tanzania kufuata taratibu za uhamiaji.

Alisema licha ya hatua zinazochukuliwa na nchi wanachama wa EAC za kuitenga Tanzania katika baadhi ya mambo, itabakia na msimamo wake na haitakubaliana kuingia kwenye Shirikisho la Kisiasa huku masuala ya ushuru wa forodha, soko la pamoja na sarafu moja, hayajatengamaa.

"Huo ndio msimamo wa Tanzania, hivi vitu vinne vilikuwa bado havijakamilika, matumizi yake hayajaenda sawasawa na makubaliano ya kila nchi sasa wanaharakisha Shirikisho la Kisiasa, waache waende kwa sababu Katiba inawaruhusu na wana ajenda zao za siri.

"Hatuoni suluhisho katika suala hilo, ni vigumu kuanza kusuluhisha matatizo ya jumuiya kwa sasa kama ilivyo vigumu kusuluhisha matatizo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Ukitazama sasa tunapambana kuendeleza Muungano na Zanzibar, hili la nchi zote nne litakuwaje? Mali zinatoka nchi nyingine, vivyo hivyo kwa upande wa bidhaa, kwa maana hiyo hatuwezi kufika kwenye shirikisho kabla hatujamaliza vikwazo hivi vingine," alisema Sitta.

Tanzania yailima barua EAC
Waziri Sitta pia alieleza kuwa Tanzania imeiandikia barua sekretarieti ya baraza la mawaziri wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki, ikilalamikia baadhi ya mambo yanayoendeshwa kwa usiri na baadhi ya nchi katika jumuiya hiyo.

Alisema barua alikabidhiwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika Agosti 28 mwaka huu, mkoani Arusha, ikitaka wahusika kuweka wazi mambo yanayoendelea ndani ya jumuiya kwa kuzishirikisha nchi zote.

Aidha, Sitta alieleza kuwa wakati barua hiyo ikiwa imekwishawasilishwa kwa Sekretarieti, viongozi ambao wamekubaliana kuanza mchakato wa kuandika Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa, wanapaswa kutambua kuwa Katiba itakayopatikana itakuwa batili kwa sababu haikuamuliwa na wananchi wa nchi husika bali watawala. Chanzo: Mtanzania

TBS yadai ‘oil’ ya magari haifai



Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Agness Mneney amebainisha kuwa asilimia 90 ya mafuta ya kulainisha mitambo (oil) ya magari yamechakachuliwa au kutengenezwa chini ya kiwango, hivyo kuhatarisha usalama wa magari hayo na watumiaji kwa jumla.

Hayo yameelezwa jana na Naibu Mkurugenzi huyo alipokuwa akifungua mkutano wa watengenezaji na wafanyabiashara wa mafuta hayo, uliofanyika kwenye ofisi za TBS makao makuu Dar es Salaam.

Mneney alisema, tatizo hilo limebainika kutokana na utafiti ulifanywa na TBS katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, wakizingatia vigezo vya msingi vinavyopendekezwa na Chuo cha Utafiti cha Petroli cha Amerika (API).

“Hata hivyo utekelezaji wa kiwango ndiyo changamoto inayotukabili. Sisi wote ni mashahidi wa mafuta yaliyopo chini ya kiwango katika soko hapa nchini. Katika utafiti ilibainika bayana kuwa kuna mahitaji yanayopaswa kuainishwa katika utendaji,” alisema Mneney.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Starpeco, Grantian Nshekanabo aliitaka TBS ichukue hatua za kiutendaji ili kuhakikisha mafuta yanayoingizwa sokoni yanakidhi viwango vinavyotakiwa ili kuepusha hasara wanayoipata watumiaji hasa wamiliki wa magari.
“TBS ihakikishe kikosi chake kinaondoa mafuta yasiyo na viwango ambayo hununuliwa kutokana na bei kuwa chini na injini za magari kuharibika.”

Msanii Masogange, mwenzake wapata dhamana Afrika Kusini


Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa

Johannesburg. Watanzania Agness Masogange na Melisa Edward waliokamatwa kwa kutuhumiwa kubeba dawa za kulevya huko Afrika Kusini wameachiwa kwa dhamana.
Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni aliithibitishia Mwananchi jana kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana,lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.

Mangaleni alisema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg.

Hata hivyo, Kamishna Mangaleni alisema hawezi kuzungumzia zaidi kuhusu kesi hiyo kwa sababu hataki kuharibu uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya Watanzania hao, ambao ni wasanii.

Marafiki wa karibu wa Masogange wanaoishi maeneo ya Midland Johannesburg ambao walikataa kunukuliwa majina yao, walithibitisha kuwa wanawake hao wameachiwa kwa dhamana.

“Ni kweli wameachiwa leo asubuhi. Lakini hatuwezi kuongelea kwa kina habari hizi kwa sababu hatutaki matatizo na polisi. Hii kesi bado inaendelea na wataendelea kubaki hapa hadi kesi yao itakapomalizika,” alisema mmoja wa marafiki zake.

Naye Masogange aliandika kwenye mtandao wa ‘Facebook’.
“Namshukuru Mungu nimeamini wewe ulikuwa pamoja na mimi katika maombi yangu na nashukuru kwa wote mliokuwa mkiniombea Mungu kapokea maombi yenu.”
Masogange na Melissa walikamatwa Julai 2 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa wana mabegi sita makubwa ya dawa zinazoaminika kuwa ni `Crystal Methyl Amphetamine’.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia Mwananchi jijini Dar es Salaam kuwa alikuwa amepata taarifa za kuachiwa kwa wasichana hao, lakini alikuwa anawasiliana na watu wa Afrika Kusini ili kupata uhakika.

Nzowa, hata hivyo alilidokeza gazeti hili juzi kuwa kuna uwezekano wanawake hao wangepata dhamana au kufungwa kifungo chepesi kwani dawa walizokamatwa nazo ni kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za aina tofauti kwa matumizi ya binadamu ingawa pia na dawa za kulevya.

Mamlaka yapinga uamuzi wa Mahakama
Msemaji wa Mamlaka za Huduma za Mapato Afrika Kusini(SARS), Marika Muller alisema wana uhakika asilimia 100 kuwa akina Masogange walikamatwa na dawa za kulevya.

“Timu yetu ilifanya kazi vizuri na ilitambua kuwa mzigo huo ulikuwa wa dawa za kulevya ila tunaiachia mahakama kuendelea na uchunguzi wake,” aliongeza Muller.
Chanzo: Mwananchi

Chikawe amwomba JK asaini muswada kuepusha vurugu


Wenyeviti wa vyama vya Upinzani,Freeman Mbowe wa Chadema(Kulia) na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF(wapili kulia)wakiagana na viongozi wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu jijini Dar es Salaam jana baada ya mazungumzo kuhusu kupinga Rais kusaini Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba.Picha na Fidelis Felix 

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, atamshangaa Rais Kikwete ikiwa atasikiliza kelele za wapinzani kwa sababu walishirikishwa kupitia kamati na hata bungeni kabla ya kupitishwa kwake.

“Nitamshangaa sana Rais Kikwete kama atashindwa kusaini muswada huo kwa sababu ya kelele za wapinzani. Tuliwashirikisha katika kila mchakato kabla na baada ya kuuwasilisha bungeni,” alisema Chikawe.

Alisema kitendo cha wapinzani hao kujiunga pamoja na kuanzisha kampeni za kuwahamasisha wananchi ili waukatae muswada hakisaidii lolote, kwa sababu sheria zote zinatungwa bungeni na siyo kwenye Viwanja vya Jangwani wala Ikulu.

Vyama vyampinga JK
Wakati Chikawe akisema hayo, viongozi wa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi wameshikilia msimamo wao kwamba wataendelea kupinga muswada huo uliopitishwa na Bunge, Septemba 6, mwaka huu.

Wakizungumza Dar es Salaam jana walipokutana na Shura ya Maimamu ikiwa ni mwendelezo wao wa kukutana na asasi za kiraia, viongozi wakuu wa vyama hivyo, walisema kamwe kasi yao ya kutaka kutosainiwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba haiwezi kupunguzwa kwa namna yoyote kwa kuwa wanatetea masilahi ya Watanzania na siyo mtu binafsi.

Kauli yao imekuja siku moja baada ya Rais Kikwete kusema kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakisema uongo kuhusu mchakato wa Katiba unavyokwenda.
Wanasiasa pia hao wamepinga matumizi ya kauli za kibabe kwenye mchakato huo na kuonya kuwa nguvu ya dola haiwezi kushindana na nguvu ya umma.

Mbali na hayo, wanasiasa hao walisisitiza kwamba hawatapiga magoti kuomba Katiba Mpya, kwani ni ya Watanzania wote na si mali ya wanasiasa, chama cha siasa wala wabunge.

Rais Kikwete alikaririwa na magazeti mbalimbali jana akipinga madai ya wapinzani kuwa hakuzingatia maoni yao wakati wa uteuzi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Nafahamu kwamba tunaambiwa tunasema uongo, lakini ni vizuri ifahamike wazi kuwa hatuwezi kupunguzwa nguvu na kauli hizo alizozitoa Rais Kikwete, kwani msimamo tulionao ni kuendelea kutetea Watanzania,” alisema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Mbowe alimshauri Rais Kikwete atumie busara kwa kutosaini mkataba huo ili mchakato uende vizuri.

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema mikutano wanayoifanya na asasi za kiraia imebainisha kwamba uteuzi wa Tume ya Katiba ulifanyika kwa ubaguzi.
“Tunafahamu kwamba Rais ana nguvu ya kuteua wajumbe wa tume hiyo kwa mujibu wa sheria, lakini kuna taasisi zimekosa wawakilishi kwenye tume, mfano hai ni Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu (Shivyawata), walitakiwa wapeleke majina ya watu watatu, lakini hakuna hata mtu mmoja kati yao aliyeteuliwa,” alisema Profesa Lipumba.

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alisema viongozi wa Shivyawata waliwaeleza wazi kuwa hawana mwakilishi kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Wanasiasa hao leo wanatarajia kukutana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tec).

Nape alonga
Akizungumzia madai hayo ya upinzani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kama wanataka waaminike, watoe ushahidi kuthibitisha wanachokidai.
“Hawa watu ni vigeugeu. Kwanza, Rais alipoteua wajumbe wa Tume, Chadema walijitokeza hadharani na kupongeza. Baadaye haohao waliibuka na kuanza kuishutumu Tume wakisema kuwa imekosa weledi.

“Wakati wa mchakato wa kukusanya maoni, Chadema haohao, ambao waliiona Tume haina weledi, wakapeleka maoni yao hukohuko. Ukifuatilia haya mtu unashindwa kuelewa msimamo wa watu hawa ni upi hasa,” alisema Nape mkoani Simiyu.
Imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Aidan Mhando na Rachel Shempemba.
Chanzo: Mwananchi

Thursday, September 19, 2013

Mwana wa Gaddafi afikishwa mahakamani


Seif al-Islam Gaddafi

Mtoto wa kiume wa dikteta wa Libya aliyeuwawa Moamer Gaddafi Alhamisi (19.09.2013) amefikishwa mahakamani katika mji wa Zintan kwa mashtaka ya kuvuruga usalama na kesi yake imeahirishwa hadi tarehe 12 mwezi wa Disemba.

Seif al-Islam pia alikuwa anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Tripoli kwa ajili ya kutajwa kwa kesi yake ya mashtaka ya usalama kuhusiana na uasi wa mwaka 2011 uliompinduwa baba yake lakini kuna wasi wasi iwapo waasi wa zamani waliomteka na kumshikilia huko Zintan watakubali kumpeleka Tripoli.

Mwendesha mashtaka wa Libya Abdulqader Radwan hapo Jumatano aliamuru Seif al -Islam ahamishiwe katika mahakama ya Tripoli kutoka ya Zintan ilioko kilomita 180 kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Mrithi huyo wa zamani wa uongozi wa Gaddafi na washtakiwa wengine zaidi ya 30 akiwemo kiongozi wa zamani wa ujasusi Abdullah al Senussi wanashtakiwa kwa madai ya uhalifu waliofanya wakati wa uasi wa mwaka 2011 uliomn'gowa madarakani Gaddafi.

Kesi muhimu katika historia ya Libya
Baghdadi al -Mahmudi waziri mkuu wa mwisho katika kipindi cha Gaddafi na Mansur Daw ambaye alikuwa akiiongoza Kikosi cha Ulinzi cha Wananchi pia ni miongoni mwa washtakiwa katika mojawapo ya kesi muhimu kabisa ya kisheria katika histroria ya Libya.

Mwendesha mashtaka wa Libya Radwan ameuambia mkutano wa wandishi wa habari kwamba wametuma agizo la kuhamisha kesi hiyo katika mahakama ya Tripoli kwa mamlaka zinazoshugulikia watu

wanaohusishwa na kesi nambari 630 akiwemo Sef al-Islam.Inaripotiwa kwamba mazungumzo yalifanyika hadi usiku wa manane hapo jana kwa ajili ya kumhamisha Seif mjini Tripoli kwa masaa kadhaa.Duru zilizo karibu na kesi hiyo zimesema suala hilo litategemea zaidi hali ya usalama.

Mashtaka makuu yanayowakabili watuhumiwa ni pamoja na mauaji yaliofanyika wakati serikali ilipokuwa ikipambana na uasi ambao ulizuka katika mji wa mashariki wa Benghazi hapo mwezi wa Februari mwaka 2011.

Seif al-Islam yuko mikononi mwa serikali
Gaddafi alitekwa na kuuwawa na waasi katika mji alikozaliwa wa Sirte mwezi wa Oktoba mwaka huo.

Mtoto wake huyo wa kiume alitekwa mwezi uliofuatia na kundi la waasi wa zamani kutoka eneo la milimani la Zintan na amekuwa akishikiliwa huko tokea wakati huo.Serikali ya sasa ya nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ilijaribu mara kadhaa kutaka kuhamishiwa Tripoli kwa mtoto huyo wa Gaddafi bila ya mafanikio.

Hata hivyo serikali hiyo imekuwa ikisisitiza kwamba Seif al-Islam anashikiliwa na serikali.

Wakati huo huo shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu Amnesty International limetaka kukabidhiwa haraka kwa Seif al Islam na Senussi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Shirika hilo limesema mfumo wa mahakama nchini Libya unatakiwa kufanyiwa mageuzi makubwa na kuna wasi wasi mkubwa juu ya uwezo wa serikali kuhakikisha kesi zinafanyika kwa haki kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya usalama nchini humo.

Jumla ya nyaraka 40,000 na kurasa 4,000 za maelezo ya usaili zitazingatiwa na mahakama ambayo itasikiliza kesi hiyo katika eneo la siri katika mji mkuu wa Libya.
Iwapo watuhumiwa watapatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Mwandishi : Mohamed Dahman/AFP
Mhariri: Josephat Charo
Chanza: DW

KATUNI NDANI YA Chiwambo's blog


JK: Tutakabiliana na wauza ‘unga’ kwa nguvu zote


California/Johannesburg. Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema Serikali yake haitawatetea Watanzania wanaokamatwa wakijishughulisha na biashara ya dawa za kulevya, Watanzania wawili Agnes Masongange na mwenzake, Melisa Edward jana walinyimwa dhamana na Mahakama Kuu ya North Gauteng katika kesi ya dawa ya kukamatwa na dawa hizo.

Rais Kikwete alisema Serikali yake itakabiliana na biashara hiyo kwa nguvu zote kwa kuwa ni haramu na ni kinyume na sheria za nchi.

Alisema hayo juzi usiku alipokutana na Watanzania wanaoishi katika Jimbo la California, Marekani...“Serikali yangu haitawatetea watu wanaojishughulisha na ubebaji wa dawa za kulevya na kusafirisha nje ya nchi. Hii ni biashara haramu na inavunja sheria za nchi yetu.”

Masogange na Melisa walikamatwa Julai 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh6 bilioni.

Aidha, amesema hayo siku chache baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa ya kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Paundi za Uingereza 50 milioni (Sh125 bilioni).

Pia, Agosti 31, mwaka huu, mshambuliaji nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Bole, Addis Ababa walipokuwa wakijiandaa kwenda Paris, Ufaransa wakituhumiwa kubeba dawa za kulevya.

Juzi, Rais Kikwete alisema ni wajibu wa Watanzania wanaoishi ughaibuni kuwa raia wema, kufuata na kuheshimu sheria katika nchi wanazoishi kwa sababu wakizivunja, Serikali yake haitawatetea.

“Ukikamatwa na dawa za kulevya hatukutetei kwa sababu hata sheria za nchi yetu zinazuia biashara hiyo. Sisi hatuwezi kuendelea kuwa na sifa ya kufanya biashara za ovyoovyo kiasi hicho. Serikali itawatetea Watanzania wanaoishi nchi za nje ikiwa wataonewa. Lakini ukifanya biashara ya dawa ya kulevya au kubaka watu hatukutetei kamwe,” alisema.

Masogange, Melisa wakwama dhamana
Masogange na mwenzake Melisa jana walikosa dhamana baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu ya North Gauteng, Afrika Kusini kujibu mashtaka ya kusafirisha dawa zinazodaiwa kutumika kutengenezea dawa aina ya amphetamine (maarufu kama tik).

Taarifa kutoka Mahakama hiyo zinaeleza kuwa, Masogange na Melissa walirudishwa rumande na kesi yao itasikilizwa tena Novemba mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya cha Polisi nchini, Kamanda Godfrey Nzowa alithibitisha kuwa watuhumiwa hao walipanda kizimbani jana kujibu mashtaka yanayowakabili ya kusafirisha dawa za kulevya na kwamba wamerudishwa rumande hadi Novemba.

Awahoji akina Masogange
Nzowa alisema alikwenda Afrika Kusini kuwahoji Melisa na Masogange kabla ya kupandishwa kizimbani lakini alisema hawakumpa ushirikiano.

Kamanda huyo alisema imebainika kuwa mzigo walioubeba wasichana hao haukuwa dawa halisi za kulevya, bali kemikali zinazotumika kutengeneza dawa zinazoitwa amphetamine. Kutokana na madai hayo, Nzowa alisema wanaweza kupewa dhamana na kesi yao kuendelea kusikilizwa nchini baada ya yeye (Nzowa) kushauriana na Kitengo cha Dawa za Kulevya cha Afrika Kusini.

Alisema, inawezekana watuhumiwa wakapewa hukumu nyepesi kidogo kutokana na kosa hilo.
Chanzo: Mwananchi

Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani


Dar es Salaam. Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini.

Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette alikuwa amemaliza muda wake nchini Kenya na alitakiwa kuja kuiwakilisha nchi yake Tanzania.
Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na Gazeti la Standard la Kenya akieleza kuwa anajipanga kurudi kwao baada ya kukataliwa na Serikali ya Tanzania.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ndio wanaoshughulika na hayo mambo, waulizeni.”

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema wizara yake haijapata taarifa za kukataliwa kwa balozi huyo.

“Suala hilo linahusu ofisi ya Rais, mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa na hata kama ingekuwapo hiyo taarifa siyo ya `public’.
“Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.

“Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine,” alisema Mkumbwa.

Alikariri Kifungu cha Nne cha Azimio la Vienna ambacho kinaruhusu nchi kukataa balozi wa nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
“Nchi inayopeleka balozi katika nchi nyingine inatakiwa kutoa jina mapema kwa nchi nyingine. Hata hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa kumkubali au kukataa uteuzi,” kinaelekeza kifungu hicho.

Balozi Mjerumani alonga
Gazeti hilo la The Standard, lilimkariri Balozi Hellwig-Boette akisema kuwa amekataliwa kuja Tanzania bila ya kuelezwa sababu.
“Ndiyo, Tanzania imekataa uteuzi wangu. Kwa mujibu wa itifaki za kidiplomasia, nchi husika ina haki ya kumkataa mtu aliyeteuliwa kwenda kuwakilisha nchi yake au kumkubali.

Tanzania imenikataa lakini haijatoa sababu yoyote ya kufanya hivyo.
“Nitaondoka Nairobi kurudi Berlin Alhamisi (leo) asubuhi ili nikapangiwe sehemu nyingine,” lilieleza gazeti hilo.

Hivi karibuni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga aliandaa chakula cha jioni, lengo likiwa ni kumuaga balozi huyo baada ya kumaliza kipindi cha miaka minne akiwa anaiwakilisha Ujerumani nchini Kenya.

Misimamo yake imemponza
Gazeti hilo limesema Hellwig-Botte ambaye alikuwa Balozi wa Ujerumani nchini Kenya tangu mwaka 2009, alikuwa anajulikana kutokana na misimamo yake na hasa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na mara nyingine kuunga mkono vyama vya upinzani.

Anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Serikali ya Kenya kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kushtakiwa kwenye Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa huko The Hague, Uholanzi kutokana na kuhusishwa na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Chanzo: Mwananchi