Saturday, March 15, 2014

Jasusi wa zamani Rwanda jela miaka 25

                       Simbikangwa alikuwa mkuu wa ujasusi wa Rwanda wakati wa mauaji ya Kimbari
Mahakama nchini Ufaransa, imemhukumu kifungo cha miaka 25 jela jasusi mkuu za zamani wa Rwanda Pascal Simbikangwa kwa kuhusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Simbikangwa alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji hayo na kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.

Alikabiliwa na makosa ya kuchochea , kupanga na kusaidia katika juhudi za mauaji ya watutsi hasa kwa kuwapa silaha wapiganaji wa kihutu waliokuwa wanalinda vizuizi vya barabarani na kuwaua wanaume wa kabila la Tutsi, wanawake na watoto.
Simbikangwa alikanusha madai hayo.

Haijuikani kama mawakili wa Simbikangwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Simbikangwa,mwenye umri wa miaka 54, anatumia viti vya magurudumu baada ya kuhusika na ajali mwaka 2008 alipokuwa anaishi katika kisiwa cha Mayotte.


Maelfu ya watutsi na wahutu waliuawa mwaka 1994
Ni mwanamume wa kwanza kuhukumiwa nchini Ufaransa kuhusiana na mauaji ya Kimbari Rwanda miaka 20 iliyopita.
Upande wa mashitaka uliitaka mahakama kumfunga jela maisha Simbikangwa, baada ya kumtaja kuwa mtu mkatili na ambaye anaweza kufanya mambo mabaya zaidi ya aliyofanya.

Mawakili wake hata hivyo walisema kuwa kesi hiyo ilishinikizwa zaidi kisiasa na kuwataja mashahidi kama wasioweza kuaminika na ambao walikuwa na chuki wakati wakitoa ushahidi wao.

Takriban watu 800,000 wengi wao wa kabila la Tutsi , waliuawa katika kipindi cha siku miamoja.
Chanzo: BBC Swahili

MALAYSIA: JUHUDI ZA KUISAKA NDEGE ZASHIKA KASI

Wiki moja tangu ndege ya Malaysia iliyokuwa imewabeba abiria 239 kutoweka, juhudi za kimataifa kuisaka ndege hiyo bado zinaendelea.
Mataifa kumi na mbili sasa yamejiunga pamoja kuisaidia serikali ya Malaysia na msako huo, juhudi zenyewe zikijikita zaidi Magharibi mwa rasi ya Malaysia.

Marekani imesema kuwa inatuma manowari zake za kivita, pamoja na ndege maalum ya uchunguzi katika maeneo ya Bengal, Bahari ya Andaman na sehemu za Bahari hindi.
Mnamo Ijumaa taarifa ziliibuka kuwa ndege hiyo ilituma mawasiliano katika kituo cha trafiki ya ndege kwa karibu saa tano baada ya taarifa ya kupotea kwake kutolewa.

Taarifa zinasema kuwa mawasiliano hayo yanaweza kusaidia katika kujua iliko ndege hiyo na ndio maana Marekani ikaamua kutuma meli zake za kivita katika Bahari Hindi.

CHANZO BBC

Friday, March 14, 2014

KATUNI YA WIKI NA KIPANYA


KWANINI YANGA WAENDELEZA MSIMAMO WA KUANDAMANA?

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imeomba kibali cha kufanya maandamano hadi ikulu kuushinikiza uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kutoa majibu ya maombi yao heka 11 kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Kaunda.

Katibu wa Yanga, Benno Njovu aliiambia Mwananchi jana kuwa ameliandikia barua Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuomba kibali hicho baada ya juhudi zao za kufuatilia maombi yao kwenye mamlaka za mkoa kushindikana.
Yanga, klabu kongwe kuliko zote nchini, ina mpango wa kujenga uwanja wa kisasa utakaojulikana kama Jangwani Complex, lakini ina ardhi ndogo kwenye maeneo ya Jangwani isiyokidhi mahitaji ya uwanja huo wa kisasa.

Njovu alisema wameliomba Polisi ili liwaruhusu kufanya maandamano hayo Machi 17 mwaka huu.

Naye mwanachama anayejulikana kama, Ibrahim Akilimali, ambaye amekuwa akitambulisha kama katibu wa Baraza la wazee, alidai jana kuwa maandamano yao yanatokana na kuzungushwa kwa kipindi kirefu tangu Juni mwaka jana walipoomba ongezeko la eneo hilo licha ya kufikisha ombi lao kwa kufuata taratbu.


Naye Kamanda wa Polisi wa Dar es Salaam, Suleiman Kova aliiambia Mwananchi jana kuwa hajaiona barua hiyo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi eneo ili tujue moja. 
Chanzo: Mwananchi

SHANGAZI WA KENYATTA ATEKWA NA KUIBIWA NAIROBI

Shangazi wa Rais Uhuru Kenyatta amekuwa moja wapo wa waathiriwa wa wizi wa magari kwa kutumia nguvu nchini Kenya, baada ya kushambuliwa na kuibiwa gari lake akiwa katika msongamano wa magari kwenye njia kuu ya Uhuru.

Watu watatu walokuwa na bunduki walingia kwa nguvu ndani ya gari la Bi. Njeri Muhoho, mwenye umri wa miaka 56, na kumzungusha katika jiji la Nairobi kwa karibu saa mbili kabla ya kumshusha karibu na shule moja ya kimataifa katika mtaa wa kaskazini wa Gigiri.

Bi. Muhoho, ambae ni mke wa mkuu wa zaamani wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya, George Muhoho, aliwambia polisi kwamba alikua garini pamoja na mwanamume mwenye umri wa miaka 25 wakati gengi la watu watatu walipowashambulia Jumanne, saa mbili na nusu usiku.

Polisi wanaeleza kwamba walishambuliwa wakiwa wanasubiri taa ya kuongoza magari kubadilika kuwa kijani, na aliibiwa Sh 20,000 za Kenya, pamoja na kadi yake ya benki ATM, na leseni ya kuendesha gari.

Mkuu wa polisi mjini Nairobi Benson Kibue anasema baada ya kuwashusha, wezi hao watatu walelekea mahala isipojulikana na gari lao la aina ya Nissan. Msako unafanyika kutafuta gengi la watu hao.

Chanzo: VOA Swahili

UFAFANUZI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA JIMBO LA KALENGA

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva akiongea na vyombo vya Habari leo Mkoani Iringa akifafanua juu ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura Jimbo la Kalenga.(Picha na Martha Magessa)

Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukutana na Viongozi wa Siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Kalenga mnamo tarehe 12 mach 2014, na kutoa taarifa kuhusu maadalizi ya Uchaguzi katika jimbo hilo.

Vyama vya Siasa katika mkutano huo viliarifu kama ilivyokuwa katika chaguzi ndugo zilizopita, daftari la kudumu la wapiga kura litakalo tumika katika uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kalenga ni lile lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Kutokana na hoja hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Kalenga utakaofanyika 16 mach 2014.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva amesema kuwa, Tume kwa mamlaka iliyopew na Sheria na Kanuni za Uchaguzi imekuwa ikipitia na kuhakiki Daftari la kudumu la Wapiga kura lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa dhumuni la kuondoa kasoro ndogo ndogo zilizokuwepo katka daftari hilo.

Jaji St.Lubuva amesema, Kasoro hizo ni kuwaondoa wapiga kura ambao taarifa zao zinatokea kwenye daftari zaidi ya mara moja pamoja na kuweka majina ya kupiga kura ambao walijiandikisha hapo awali na wana kadi za kupiga kura ambapo kwasababu mbalimbali za kimfumo, majina yao hayakutokea kwenye daftari lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Ameongeza kuwa, kilichofanyika ni uhakiki wa daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi na kuhakikisha kila aliyeandikishwa awali na kupewa kadi ya kupiga kura anatumia haki yake ya kupiga kura, ili kuondokana na malalamiko ya kushindwa kupiga kura kwa sababau ya kukosekana jina la mpiga kura katika kaftari hilo.
Aidha amesema, idadi ya wapiga kura ni 71,957 pamoja na vituo vya kupiga kura 216 vilivyopo katika jimbo la Kalenga.

Jaji St.Lubuva ametoaonyo rai wa vyama vya siasa kufuata taratibu na sheria walizowekewa ili kuchaguzi ufanyike kwa hali ya utulivu na haki pasipo uvunjifu wa amani.


Hata hivyo, amesema uchaguzi mgogo wa ubunge utafanyika tarehe 16 machi 2014 katika Jimbo la kalenga na kuagiza vyama vya siasa kutii agizo la kukoma kwa kampeni zao ifikapo tarehe 15 machi 2014 majira ya saa 12 jioni.

Mamia washambuliwa nchini Nigeria

Taarifa za hivi punde zinasema kuwa kumetokea mashambulizi makali ya ufyatulianaji risasi mjini Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wakazi wa mji huo wanasema kuwa walisikia ufyatuaji wa risasi na milipuko kwa karibu saa mbili nyakati za Asubuhi.

Inaarifiwa tukio hili limejiri wakati, wa kile kinachoshukiwa kuwa shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi lililofanywa na wapiganaji wa Boko Haram.
Kuna taarifa za mamia ya wapiganaji kuvamia mji huo asubuhi na mapema na kushambulia kambi mbili rasmi za jeshi ili kuwaachilia wapiganaji waliokamatwa na kuzuiliwa.

Wakazi walisema kuwa waliona ndege mbili za jeshi zikipaa katika eneo hilo.
Pia kumekuwa na taarifa ya milipuko kusikika ndani ya nyumba za wakazi pamoja na katika chuo kikuu cha Maiduguri.
Afisaa mkuu wa haki za binadamu katika umoja wa Mataifa Navi Pillay -- ambaye yuko nchini humo, alisema kuwa ukatili unaotendwa na wanajeshi ni sababu ya kundi la Boko Haram kuendeleza mashambulizi.

Maelfu ya watu wameuawa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka mitano tangu kundi la Boko Haram lilipoanza vita.

Ghasia hizi zimekithiri katika miezi michache iliyopita, licha ya juhudi za maafisa wa usalama kuzidhibiti usalama na kutangazwa kwa hali ya tahadhari katika majimbo matatu.
Chanzo: BBC Swahil

Samuel Sitta: Kura ya siri

Dodoma. Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta amezungumzia uwezekano wa kutumia kura ya siri katika kuamua ibara nyeti katika Rasimu ya Katiba.

Sitta aliyechaguliwa juzi kushika wadhifa huo, alisema atashirikiana na kamati ya uongozi itakayoundwa ya wenyeviti wa Kamati 15 za Bunge hilo na kamati ya ushauriano kupata jawabu la suala hilo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu nyumbani kwake mjini Dodoma juzi, Sitta alisema: “Unajua kuna baadhi ya vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba ni vizuri vipigiwe kura ya wazi na vingine ambavyo ni nyeti zaidi vipigiwe kura ya siri.”

Alisema si vizuri vifungu vyote vipigiwe kura sawa, yaani si lazima zote ziwe za siri au ziwe za wazi.

Alitoa mfano wa ibara inayosema kutakuwa na Mahakama Kuu ya Tanzania na kusema: “Hatuwezi kushindana katika suala la kuwapo kwa Mahakama na ni wazi kuwa jambo hilo mnaweza kupiga kura ya wazi. Nasema hivyo kwa sababu Katiba yoyote lazima ionyeshe mihimili yote ambayo ni Bunge, Serikali na Mahakama.”

Sitta ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alishinda kiti hicho katika uchaguzi uliofanyika juzi kwa kura 487 kati ya 563 (sawa na asilimia 85).

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki ambaye kaulimbiu yake ni ‘kasi na viwango’, alisema vifungu na ibara za Rasimu ya Katiba vinavyoweka misingi ya Katiba, ni vizuri vikapigiwa kura ya siri.

“Unajua tuna viongozi wa dini na halitakuwa jambo la busara kama tukizijua hisia zao. Kama wewe uko karibu na imamu au askofu halafu anapiga kura ya wazi ya kutaka Serikali tatu wakati wewe muumini unataka Serikali mbili ni wazi kuwa jambo hilo linaweza kuleta hisia tofauti na kuwanyima watu haki na uhuru wa kuamua,” alisema Sitta.

Alitoa mfano wa Sura ya Sita ya Rasimu ya Katiba inayozungumzia Serikali na muundo wa madaraka katika Jamhuri ya Muungano na kufafanua kuwa katika sura hiyo atapendekeza ipigiwe kura ya siri.

Kuhusu suala hilo la muundo wa Serikali alisema: “Kikubwa ni wajumbe kujenga hoja, hatuwezi kwenda na misimamo isiyobadilika kwa sababu tunataka maridhiano. Nitatenda haki na nitatoa muda mrefu zaidi kwa wajumbe kujadili sura ya kwanza na ya sita ambazo zina uzito mkubwa kuliko sura nyingine ambazo ni za maelezo tu. Mfano suala la haki za binadamu ambazo wote tunakubaliana nazo.”

Alisema wakati wa kujadili muundo wa Serikali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukifika, ataishauri kamati ya uongozi, kutenga muda wa ziada katika suala hilo na mengine yenye utata.

Mwenyekiti huyo alisema suala la upigaji kura linatakiwa kuamuliwa kwa busara na atatumia hekima zake na za wajumbe wa Bunge hilo, kutatua mgogoro wa kura ya siri au ya wazi.

Wakati wa kujadili rasimu ya kanuni za Bunge hilo, kulizuka mvutano mkali katika vifungu vya 37 na 38 vinavyozungumzia aina ya kura itakayopigwa wakati wa kufanya uamuzi na kulazimika kuviweka kando. CCM kimekuwa kikinadi kura ya wazi kikisema ni ya haki huku wapinzani wakitaka kura ya siri.

Hata hivyo, kamati ya muda iliyoandaa kanuni za Bunge hilo, ilipendekeza kuwa Bunge Maalumu ndilo litakaloamua aina ya kura itakayopigwa.

Akizungumzia suala hilo Sitta alisema: “Pamoja na kuwapo kwa hali hiyo, lazima ifikie wakati tuamue. Hatuwezi kuwa na kanuni ambazo hazielekezi namna ya kupiga kura kwa sababu upigaji wa kura unaweza kuanza kufanyika wiki ya kwanza tu baada ya kuanza kujadili Rasimu ya Katiba.”

Samia Makamu Mwenyekiti

Wakati huohuo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan jana alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo baada ya kumshinda mpinzani wake, Amina Abdallah Amour.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa Uchaguzi, Dk Thomas Kashililah alisema kati ya kura 523 zilizopigwa, Suluhu alipata kura 390 sawa na asilimia 74.6, Amina kura 126 sawa na asilimia 24.1. Kura saba ziliharibika.

Kukamilika kwa uchaguzi huo kunafungua milango kwa Yahya Hamad Hamis kuapishwa kuwa Katibu wa Bunge la Katika na Dk Thomas Kashililah kuwa Naibu Katibu kwa mujibu wa sheria.

Makatibu hao wataapishwa leo saa nne asubuhi na Rais Jakaya Kikwete katika Ikulu ndogo ya Dodoma. Baada ya kuapishwa, Katibu atawaapisha Sitta na Samia katika Ukumbi wa Bunge kuanzia saa 10 jioni leo.

Awali wakati wakijieleza Amina alizua gumzo baada ya kueleza kuwa licha ya kuwa na watoto watano, ameachika na kwa sasa hana mume.

“Mimi ni mama wa watoto watano, nina shahada ya uzamili ya masuala ya fedha, nina stashahada ya sheria na nimefanya kazi katika Benki ya Biashara kwa miaka 23 ila kwa bahati mbaya nimeachika,” alisema na kusababisha wajumbe kuangua kicheko.

Baada ya kuchaguliwa, Suluhu alisema: “Nitafanya naye (Sitta) kazi kwa ushirikiano na uadilifu mkubwa. Pia ninawaahidi wajumbe wote kuwa nitawapa ushirikiano.”

Mbowe amuonya Sitta
Wakati huohuo; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtumia salamu za pongezi Sitta huku akimtaka kuachana na masilahi ya chama chake.

“Ningependa kutuma salamu kwa Samuel Sitta ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, nataka aelewe kuwa alichokabidhiwa ni majukumu si cheo,” alisema na kuongeza:

“Mamilioni ya Watanzania watakuwa wanamfuatilia na kumtazama kwa makini mno... maana wananchi kwa sasa wanajua mchakato wa Katiba Mpya umebeba matumaini ya Taifa lao kwa miaka 50 hadi 100 ijayo.

 Chanzo: Mwananchi

Serikali yaingilia kati ada vyuo vikuu

                                           Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.PICHA|MAKTABA
 Dar es Salaam. Serikali imekunjua makucha yake katika kudhibiti ada zinazotozwa katika vyombo vya utoaji elimu chini.

Jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa alizindua rasmi mfumo mpya wa ulipaji ada katika vyuo vya elimu ya juu, huku akisema utasaidia kudhibiti viwango vya ada vinavyotozwa kwa wanafunzi.

Akizindua mfumo huo jijini Dar es Salaam, Dk. Kawambwa alisema Serikali imeanzisha mfumo huo unaotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu katika vyuo vyote, kwa lengo la kudhibiti ada kulingana na fani zinazotolewa.

“Sasa natarajia nitapata usingizi wa kueleweka maana kelele za viwango vya ada zilikuwa ni kubwa, kila chuo kilikuwa na ada yake. Niliulizwa vigezo vinavyotumika kupanga sikuwa na jibu, lakini sasa nitakuwa na majibu tena yanayoeleweka,” alisema.

Suala la viwango vya ada katika shule na vyuo binafsi liliwahi kuzungumziwa kwa kina siku za nyuma, huku Rais Jakaya Kikwete na Waziri Kawambwa wakinukuliwa kwa nyakati tofauti kutaka taasisi za elimu kupunguza viwango vya elimu. Aprili 2013 akifungua Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyokuwa vya Serikali (Tamongsco) uliofanyika mkoani Mbeya, Rais Kikwete alisema: “Elimu ni huduma muhimu na haki kwa mtoto. Siyo vyema kugeuzwa kuwa biashara ya kuleta faida kubwa.’’

Aliongeza kuwa Serikali ilikuwa katika mchakato wa kutathmini ada zinazotozwa vyuoni na sekondari ili kupendekeza viwango halisi vinavyopaswa kutozwa.

Kwa sasa udadisi wa gazeti hili umebaini kuwa wanafunzi walioanza masomo katika mwaka wa fedha 2013/2014 wanatozwa ada kuanzia Sh360,000 kwa mwaka hadi Sh9,900,000.

Kwa mujibu wa Dk. Kawambwa, mfumo huu ambao baadaye utaendelea hadi shule za sekondari na msingi, umepatikana kupitia kikosi kazi cha wataalamu ambacho pamoja na majukumu mengine kilipewa kazi ya kutathmini gharama.

Dk. Kawambwa alisema moja ya faida ya utaratibu huo mpya ni kudhibiti taasisi zinazotoza ada kubwa kwa sababu za binafsi ikiwamo biashara.

Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini Makumira cha Dar es Salaam (Tudarco), Profesa Uswege Minga alisema endapo gharama hizo zitakuwa sawa, vyuo binafsi vitaathirika kwa sababu ni gharama kubwa kuendesha chuo kikuu.
Chanzo: Mwananchi

Zaidi ya raia milioni 9 wa Syria hawana makaazi

Shirika la kushughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limesema mzozo wa Syria umesababisha mzozo mkubwa zaidi duniani wa wakimbizi kwani umesababisha zaidi ya raia milioni 9 wa Syria kuachwa bila makaazi.

Kamishna mkuu wa shirika hilo la UNHCR Antonio Guterres amesema asilimia 40 ya wasyria wameyatoroka makaazi yao huku zaidi ya milioni 6.5 kati yao wakitafuta hifadhi salama ndani ya Syria kwenyewe na wengine milioni 2.6 wakitorokea nchi jirani.

Guterres amesema ni jambo lisiloingia akilini ni vipi janga kubwa la kibinadamu la kiwango cha namna hiyo linajiri machoni mwa walimwengu bila ya hatua zozote za maana kuchukuliwa kuzuia umwagikaji mkubwa wa damu unaoendela Syria.
UNHCR imesema wengi wa wakimbizi wa Syria wamepata hifadhi katika nchi zisizo na utajiri mkubwa kama Misri,Iraq,Jordan,Lebanon,Uturuki na hivyo imeathiri pakubwa uchumi na miundo mbinu ya nchi hizo.

Chini ya asilimia nne ya wakimbizi wa Syria wako Ulaya
Ni kiasi kidogo cha wakimbizi wa Syria wameweza kutafuta hifadhi katika nchi za Ulaya kutokana na hatari ya kuzifika nchi hizo kupitia safari za majini na pia kukumbwa na hata hatari kubwa zaidi iwapo watanusirika ya kukataliwa na nchi hizo.

Guterres amesisitiza kutumika kwa kila juhudi kutafuta amani Syria ili kupunguza dhiki na mateso ya raia wasio na hatia waliojikuta katika mzozo huo na kulazimika kuyatoroka makaazi yao,jamii zao,kazi zao na maisha yao ya kawaida.

Vita hivyo vya Syria ambavyo vilianza mwezi Machi mwaka 2011 kama wimbi la uasi la kutaka kumg'oa madarakani Rais Bashar Al Assad limesababisha vifo vya zaidi ya watu 140,000 na kuziathiri pia nchi za kanda hiyo kutokana na mzigo wa kuwapokea wakimbizi.

Nchini Lebanon pekee idadi ya wakimbizi wa Syria inaelekea kufika milioni moja huku ikitarajiwa kuongezeka hadi milioni 1.6 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
UNHCR imezitaka nchi za Ulaya,Amerika ya Kaskazini na Asia kutoa nafasi kwa wakimbizi wa Syria.

Bunge la Syria laidhinisha sheria mpya za uchaguzi

Huku janga hilo la kibinadaamu likiendelea,bunge la Syria leo limeidhinisha sheria mpya za uchaguzi ambazo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo mingi inaruhusu wagombea kadhaa kuwania urais.

Sheria hiyo imeidhinishwa miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu.Hata hivyo sheria hiyo inawazuia viongozi wa upinzani walio uhamishoni kugombea dhidi ya Assad kwani sheria hiyo inataka wagombea wawe wameishi Syria kwa miaka kumi mfululizo.
Rais Assad anatarajiwa kugombea muhula mwingine wa miaka saba.Uchaguzi sharti ufanywe kati siku sitni na tisini kabla ya muhula wake kukamilika tarehe 17 mwezi Julai mwaka huu.

Upande wa upinzani na wapatanishi wa kimataifa wamepinga kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu huku bado mazungumzo ya kuvimaliza vita hivyo yakiwa bado yanaendelea.
Mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa na nchi za kiarabu kuhusu Syria Lakhdhar Brahimi akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana amesema anahofia kuwa iwapo kutakuwa na uchaguzi,upinzani hautakuwa na nia ya kufanya mazungumzo na serikali.

Mwandishi:Caro Robi/afp/dpa
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Chanzo: Dwswahil.com 

Thursday, March 13, 2014

NJIA 7 ZA KUONGEZA WASOMAJI WA BLOG YAKO

Katika ulimwengu wa leo neno blog siyo kitu kigeni, leo hii karibu kila mtumiaji wa internet anayo blog yake. Blogu hizi kuna zile zinazotembelewa na watu wengi na kuna zile zinazopata watembeleaji kwa mdondo.Je umewahi kujiuliza kwanini watu hawatembelei blog yako kama wanavofanya kwa blog fulanifulani? Ingawa kuna sababu nyingi kama umri wa blog, umarufu wa mmiliki wa blog nk lakini kuna kuna vitu ambavyo unaweza kuvifanya na vikakuongezea idadi ya watembeleaji.
Hivyo kwenye makala ya leo tutaangalia ni vitu gani vya msingi kuzingatia ili blog yako ivutie wasomaji wengi zaidi.

1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.
Kama umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule. Ingawa ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi (blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi, ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.
Siyo tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.

Hivyo, jambo la muhimu ni kuchagua uelekeo unaoupenda na kuuweza, mara nyingi kazi ya kublog huwa rahisi kama unablogu kitu unachokipenda, mfano, binafsi nikiwa ninaandika makala zenye uelekeo wa IT kwenye Blog ya Dudumizi, kwakuwa ninapenda IT na ndiyo maisha yangu ya kila siku hivyo kwangu kuandika makala za IT ni sehemu ya maisha yangu, na jinsi kazi inavyokuwa rahisi ndivyo utakavyoweza kuandika makala nyingi zaidi na zenye mvuto zaidi, hivyo huvutia wengi zaidi.

Pia jinsi unavyokuwa wa kipekee, ndivyo unavyopata watemebeleaji wengi zaidi, mfano, badala ya kukimbilia kwenye blogu za habari na michapo, kwanini usijikite kwenye blogu za yanayoendelea vyuoni na kuonesha maisha ya wanafunzi, kwanini isiwe blogu ya hadha ya usafiri na foleni nk.

Wana blogu wanatakiwa kuwa wabunifu, wawe watu wanaofikisha maono yao juu ya mambo ya kijamii kwa kutumia intaneti, na wao ndiyo wataisaidia jamii yetu.
Kumbuka; Unapochagua uelekeo,itakusaidia kujua nani mlengwa wako, na vitu gani muhimu huyo mlengwa wako vinamuhusisha, hapa utaangalia mambo kama elimu, upeo wa uelewaji na hata vitu wanavyopenda kusoma. Kwa kujua vitu hivi itakusaidia kuandika makala zinazosomwa na zenye kueleweka na wahusika. Kumbuka, haublogu ili usome wewe mwenyewe bali ni kwa ajili ya watemebeleaji wako. Hivyo kuwafahamu wao ni moja ya hatua muhimu itakayowawezesha kusoma na kuzipenda makala zako.

2. Tumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ni kitu cha lazima kama unataka kuongeza watemebeleaji wa blogu yako. Mitandao hii ni vijiwe vya mamilioni ya watemebeleaji ambao pia ni watemebeleaji wa blogu yako pia, hivyo ni lazima uhakikishe unatumia vyema mitandao hii.
Hakikisha kila makala ya blogu yako inaenda moja kwa moja kwenye mitandao jamii, pia hakikisha kwenye kila makala kuna kitufe cha share, like, g+ nk mbavyo vitawawezesha muingiliano na mitandao jamii.

Ingawa mitandao jamii ni muhimu, lakini, epuka matumizi yaliyozidi na hata kuwachukiza watembeleaji, kuna baadhi ya blogu kila unapofungua unakutana na kidirisha cha
kulike ambacho hukuzuia kufanya lolote mpaka ulike kurasa ya Facebook. Hi inaweza kuwa kero kwa watembeleaji wa blogu yako. Kitu cha muhimu hapa ni, usiwalazimishe
watu kulike au kushare makala zako, bali washawishi kwa ubora wa makala.

3. Blogu yako iwe na spidi ya haraka
Je ni watu wangapi wapo tayari kusubiria dakika tano mpaka blogu yako ikawa tayari kufunguka? Kama wewe blogu yako ni mpya, ni dhahiri kuwa hakuna atakayesubiri, na kama wewe blogu yako ni maarufu, basi watasubiri kwakuwa hakuna mbadala na pindi watakapopata mbadala basi wataanza kupungua siku hadi siku.

Blogu kuchelewa kufunguka kunaweza kusababishwa na mambo mnegi kama uwingi wa makala, teknolojia iliyotumika na hata mrundikano wa vitu; mfano, kwenye blogu nyingi za Tanzania, kumekuwa na rundo la matangazo kabla ya kuanza kwa makala, na matangazo haya ni picha kubwa ambazo kila moja inachukua ujazo tosha na kuifanya blogu iwe taratibu sana.

Kuna njia nyingi za kuonesha makala na matangazo idadi sawa kwa mtindo ambao hautoathiri spidi ya blogu yako ambayo nimeielezea kwenye kipengele cha muonekano.

4. Fikiria jina kamili
Blogu kama ilivyo Website, inaweza kuwa na jina, leo hii kuna blogu nyingi sana maarufu zina majina, kama www.mjengwablog.com, www.8020fashionsblog.com nk, kuwa na jina kamili la blog yako kutasaidia kukumbukika na pia itakusaidia kwenye mitandao ya utafutaji. Si hayo tu, pia itakusaidia pindi unapotaka kuhamia kwenye website kamili kwani hautatakiwa kuwataarifu watembeleaji tena.

Nimewahi kuandika mambo ya kuzingatia pindi uchaguapo majina ya website  / blog
Kwa wale wanaotumia Blogspot, unaweza kununua jina (domain) halafu ukalielekeza kwenye blogspot na watu wakatumia jina kamili kufungua blog yako na sio .blogspot.com tena ila wewe utaendelea kuichunga kwenye blogspot kama kawaida.
Gharama ya jina haizidi elfu 20 ya kitanzania, unaweza nunua kwa kwenda hapa

5. Muonekano bora ni kitu cha lazima
Kwenye falsafa ya watumiaji wa mitandao tunasema; mtembeleaji wa wavuti hutumia sekunde zisizozidi tatu kutafuta anachokitaka na kama atashindwa kukipata, basi kutimka, hivyo blogu yako ni lazima iwe na uwezo wa kufikisha ujumbe na kumvutia somaji ndani ya sekunde tatu.

Blogu isiyovutia haiwezi kuwa na watembeleaji wengi, na hata kama wengi wanakuja, basi hutimka (baunce) bila kusoma chochote. Leo hii kuna makampuni mengi sana yanayoweza kukusaidia kutengeneza blogu au website kwa gharama nafuu kabisa, unaweza kutafuta kwa kuandika website design in tanzania kwenye google na kuangalia makampuni yanayoweza kukusaidia.

Ingawa mitandao ya blog kama Bloggers ni mizuri kwa kuanzia, ila jinsi blog yako inavyozidi kukua, ndivyo umuhimu wa kuwa na blog inayojitegema unavyoongezeka.

Gharama za kutengeneza blog isiyo ya blogspot.com si ghali na hi itakupa uwanja mpana wa kuchunga na kuiboresha blog yako.

6. Takwimu ni muhimu pia
Ingawa mada ni jinsi ya kuongeza wasomaji wa blog yako, lakini hatuwezi kuacha kuongelea umuhimu wa takwimu. Kuna usemi unaosema, kama usipoipima, basi hautoweza kuiboresha. Hivyo kwa kuwa na takwimu ya watembeleaji wa blog yako, siyo tu itakuwezesha kujua mtiririko wa wasomaji, bali wanapotoka, wanatumia muda gani kwenye blog yako nk.

Takwimu zitakusaidia kupanga mikakati ya kujitanua na kujitangaza zaidi, pia zitakuwezesha kuthaminisha harakati zako za ukuaji. Na takwimu hizi zinapatikana kwa kwenda Google Analytics.

7. Usisahau watumiaji wa simu
Takwimu zinaonesha, watumiaji wa intanet wengi hutumia simu za mkononi kufungulia website, na idadi hii huongezeka siku hadi siku. Hivyo, kama wewe ni mmiliki wa Blog, hakikisha blog yako inaonekana vyema kwa watumiaji wa simu.
Kama website yako haifunguki kwenye simu, basi jua kwamba unapoteza mamia ya watembeleaji siku hadi siku. Hivyo wakati ndiyo huu, nenda kisimusimu zaidi.

Makala zaidi za IT, tembelea

Web: www.dudumizi.com   Facebook: www.facebook.com/dudumizi

SAMWEL SITTA ASHINDA KUWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mh.samweli sitta ameshinda nafasi ya mwenyekiti wa bunge la katiba kwa kura 487 na hashim rungwe kapata69 walio piga kura jumla ni566 kula zilizo alibika ni 7.

UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA


KATUNI YA WIKI


Tuesday, January 21, 2014

JK atema wengine watano, wapya ni 10

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akitangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Picha na Edwin Mjwahuzi

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambayo yamewatupa nje mawaziri watano, kuwaingiza 10 wapya, kuwapandisha manaibu wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha wengine wanane kutoka wizara zao kwenda nyingine.

Miongoni mwa walioachwa katika mabadiliko yaliyotangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue jana, ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji, Dk Binilith Mahenge.

Wengine walioachwa na wizara zao kwenye mabano ni Manaibu Waziri, Goodlucky Ole Medeye (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Gregory Teu (Viwanda na Biashara), Benedict Ole Nangoro (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Philipo Mulugo (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).

Mawaziri hao wanaungana na waliokuwa mawaziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais kutokana na matokeo ya uchunguzi wa Kamati ya Bunge kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Balozi Sefue alisema kuachwa kwa mawaziri hao ni moja ya hatua zilizochukuliwa na Rais Kikwete kuimarisha utendaji serikalini. Pia alisema mabadiliko hayo yametokana na kuwapo kwa nafasi baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.

“Rais amefanya mabadiliko kwa mujibu wa Ibara ya 55 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayompa mamlaka ya kutekeleza wajibu huo,” alisema Balozi Sefue.

Sura mpya

Sura 10 mpya zilizoingia katika Baraza hilo ni pamoja na Dk Asha Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani ambaye anakuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Naibu wake, Kaika Saning’o ole Telele ambaye ni Mbunge wa Ngorongoro.

Wengine wapya ni wale walioteuliwa kuwa Naibu Mawaziri na wizara zao kwenye mabano, Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (Fedha), Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (Elimu na Mafunzo ya Ufundi).

Pia wapo Mbunge wa Serengeti, Dk Steven Kwebwe (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Mbozi Magharibi, Godfrey Zambi (Kilimo, Chakula na Ushirika), Mbunge wa Mufindi Kusini, Mahmoud Ngimwa (Maliasili na Utalii) na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).

Waliopandishwa, kuhamishwa

Mbali na Dk Mahenge, Rais Kikwete pia amewapandisha manaibu waziri wengine watatu kuwa mawaziri kamili pasipo kuwahamisha wizara walizokuwa. Hao ni Saada Nkuya Salum anayekuwa Waziri wa Fedha, Lazaro Nyalandu (Maliasili na Utalii) na Dk Seif Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii).

Balozi Sefue alisema Rais Kikwete amewahamisha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukua nafasi ya Dk Nchimbi, wakati aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi amerejeshwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kuchukua nafasi ya Nahodha. Dk Mwinyi aliwahi kuongoza wizara hiyo.

Wengine waliohamishwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, kuchukua nafasi ya Charles Kitwanga aliyehamishiwa Wizara ya Nishati na Madini kuendelea na wadhifa huo. Kitwanga anachukua nafasi ya George Simbachawene ambaye amehamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima amehamishiwa Wizara ya Fedha kuchukua nafasi ya Janeth Mbene ambaye amehamishiwa, Wizara ya Viwanda na Biashara kuchukua nafasi ya Teu. Amos Makalla amehamishwa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwenda Wizara ya Maji.


Sefue alisema mawaziri na manaibu waziri wapya wataapishwa leo saa 10 jioni Ikulu.
Chanzo: Mwananchi