Tuesday, November 12, 2013

Uhusiano kati ya Zimbabwe na China wanoga



Serikali ya Zimbabwe, imetia saini mkataba na benki ya serikali ya China kuinua hadhi ya mradi wake wa kuzalisha kawi ya maji katika bwawa la maji la Kariba.
Waziri wa fedha wa Zimbabwe, Patrick Chinamasa, alisema kuwa benki hiyo hutoa mkopo wa takriban dola milioni tatu hadi ishirini kwa mradi huo ambao utasaidia kumaliza tatizo la uhaba wa umeme huku serikali ya China nayo ikitoa ufadhili wa ziada.
Zimbabwe imekuwa ikiimarisha uhusiano wake na China hasa baada ya Marekani na Ulaya kuiwekea nchi hiyo vikwazo.

Waziri Chinamasa alisema kuwa mkopo huo utalipwa na Zimbabwe pamopja na riba ya asilimia mbili kila mwaka kwa miaka ya kwanza tano na kisha kulipa mkopo utakaosalia kwa miaka 20.
Pesa hizo zitatumiwa kuongeza uwezo wa bwawa la kuzalisha kawi ya maji kwa megawati 300.
Zimbabwe huzalisha kawi yenye megawati 1,200 kwa kawaida kila siku ikilinganishwa na mahitaji ya megawati 2,100 kila siku.

Ili kukabiliana na uhaba wa umeme wakati mahitaji ni makubwa, baadhi ya sehemu za mji husalia bila umeme kwa hadi masaa kumi hususan katika miji mikubwa.
Zimbabwe imeendelea kuimarisha uhusiano wake na China baada ya kutofautiana na nchi za Magharibi.

Marekani na Ulaya ziliiwekea nchi hiyo vikwazo, ikiwemo vya usafiri pamoja na kupiga tanji mali zake Rais Robert Mugabe na washirika wake baada ya uchaguzi wa mwaka 2002, ambao waangalizi wa Ulaya walisema ulikumbwa na visa vya wizi wa kura na kwamba Mugabe hakushinda kwa njia halali.

Wanawake wananyanyaswa zaidi Misri



Misri inasemekana kuwa nchi yenye rekodi mbaya zaidi ya haki za wanawake katika mataifa ya kiarabu. Hii ni kwa mujibu wa kura ya maoni iliyofanywa na wataalamu wa maswala ya kijinsia.

Utafiti huo uligundua kuwa wanawake wanadhulumiwa sana kingono, visa vingi vya ukeketaji wa wasichana na ongezeko la makundi ya watu wenye itikadi kali kuwa baadhi ya mambo yanayochangia dhuluma dhidi ya wanawake.
Visiwa vya Comoros vilishikilia nafasi ya kwanza katika utafiti huo uliofanywa na wakfu wa Thomson Reuters.

Zaidi ya wataalamu 330 wa maswala ya jinsia walihojiwa katika nchi 21 za kiarabu ikiwemo Syria.
Huu ni utafiti wa tatu wa aina hii kufanywa na wakfu huo uliolenga hasa haki za wanawake tangu harakati za mapinduzi kuanza kushuhudiwa katika nchi za kiarabu mwaka 2011.

'unyanyasaji kila siku'
Iraq ilishikilia nafasi ya pili baada ya Misri ikifuatiwa na Saudi Arabia, Syria na Yemen kuwa miongoni mwa nchi zenye rekodi mbovu kuhusu haki za wanawake.
Nchini Comoros ambako wanawake wanashikilia asilimia 20 ya nyadhifa za mawaziri, inafuatiwa na Oman, Kuwait, Jordan na Qatar.

Kura ya maoni iliwataka wataalamu kutathmini maswala kama dhulumua dhidi ya wanawake, haki za afya ya uzazi , ambavyo wanawake wanatendewa katika familia na jukumu la wanawake katika siasa na uchumi.
Sheria zinazochochea ubaguzi dhidi ya wanawake pamoja na biashara haramu ya binadamu ndizo sababu zilizochangia Misri kuwa na rekodi mbaya zaidi katika ambavyo wanawake wanatendewa katika nchi 22 za kiarabu.

Nchini Misri kuna sehemu ambazo shughuli za kiuchumi na biashara zinazingatia sana biashara haramu ya kuwauza wanawake na kuwafanyisha ndoa za lazima.
Hata hivyo dhuluma za kingono ndio changamoto kubwa zaidi dhidi ya wanawake.
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Aprili ilisema kuwa asilimia 99.3 ya wanawake wamedhulumiwa kingono.

Wakati huo huo, Iraq imesemekana kuwa mahala hatari sana kwa wanawake kuishi kuliko ilivyokuwa chini ya utawala wa hayati Saddam Hussein..
Chanzo: BBCSwahili

PAC: Makinda, Ndugai wanatumika kutuingilia



na Betty Kangonga
MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Deo Filikunjombe, amewataka Spika wa Bunge, Anne Makinda, na naibu wake, Job Ndugai, kuacha kutumiwa na serikali kuingilia kamati za Bunge wakati zikitimiza majukumu yake.

Akizungumza jana wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za PAC na ile ya serikali za mitaa (LAAC), Filikunjombe alisema mara nyingi kama kamati wamekuwa wakipokea simu kutoka kwa viongozi hao zinazolalamikia utendaji wao.
Filikunjombe alisema kuwa hatua ya kuruhusu vyombo vya habari kuingia wakati wa kuhoji mashirika na taasisi mbalimbali za umma imesababisha tatizo hadi kufikia viongozi hao kuwapigia simu na kuwataka kutofanya hivyo.

Alisema kuwa hatua hiyo inasababisha kukosa uwajibikaji na uwazi katika masuala ya fedha za umma.
“Tunawaita watendaji waje kujieleza mbele ya kamati juu ya matumizi ya fedha lakini cha kushangaza utaona unapigiwa simu mara na Spika au naibu wake; sasa hii inaondoa dhana nzima ya uwajibikaji,” alisema.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Ludewa (CCM), taasisi hizo zinapoomba fedha zinafanya hivyo mbele ya umma sasa inashangaza kuhofu kuhojiwa wakati vyombo vya habari vikiwepo.
Alisema kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kuziamini kamati na kuziacha zifanye kazi zake kwa umakini ili kuwa na uwajibikaji.

“Tunaomba pia kuepuka kuzivunja kamati hizi mbili, ni vyema zikaachwa ili zidumu kwa kipindi chote kuliko kuzivunja kwa kuwa zina umuhimu zaidi katika usimamizi wa fedha za umma,” alisema.

Naye Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alisema kuwa ni muhimu Makinda akaona umuhimu wa kuleta kamati nyingine ili kuwezesha shughuli zilizokuwa zikifanywa na kamati ya POAC zikaweza kuendelezwa.
“Tunafahamu umuhimu wa kamati hiyo, leo tunaona umuhimu wa kazi zilizokuwa zikifanywa na kamati zilizovunjwa, hivyo Bunge linapaswa kuzingatia uamuzi unaofanywa,” alisema.

Utouh aliongeza kuwa ni vyema Bunge likaona umuhimu wa kamati hizo ikiwa ni pamoja na kuziwezesha ili zifanye kazi zao kwa umakini.
Naye Mwenyekiti wa LAAC, Rajab Mbarouk Mohamed, alisema kuwa kamati hiyo inasikitishwa na kitendo kinachofanywa na ofisi ya Bunge kwa miaka miwili kushindwa kuwapa fedha ili kuweza kukagua miradi ya maendeleo.

Alisema kuwa hivi sasa kamati zimechoka kuwa washauri tu badala yake zimetaka kupewa meno ili ziweze kutembea na askari polisi pindi zinapokwenda kufanya ukaguzi mbalimbali.
“Ili nidhamu irudi katika halmashauri zetu tuna haja ya kupewa meno na kukabidhiwa polisi ili tunapokamata watendaji wabadhirifu tuweze kuwakabidhi kwa vyombo vya dola na wakawekwa ndani ili waogope,” alisema.

Akijibu hoja hizo, Ndugai alikiri kuwa huko nyuma sheria za Bunge zilikuwa haziruhusu vyombo vya habari kuingia wakati idara mbalimbali zinahojiwa kuhusu matumizi.
Ndugai alisema kuwa kuanzia sasa wanajaribu kuangalia namna ya kuweka uwazi katika suala hilo ili kuviruhusu vyombo vya habari kupata taarifa za matumizi ya fedha za umma.

“Juu ya suala la Utouh, nimelipokea; ninaahidi kulifikisha Bungeni na tutatoa majibu muda si mrefu,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima

Kiongozi wa Msafara wa Rais akutwa na zaidi ya kilo 297 za dawa za kulevya



KASHFA NZITO LIBERIA: Msafara wa Rais Ellen Johnson Sirleaf wakutwa na zaidi ya kilo 297 za bangi. Watu 4 akiwemo kiongozi wa msafara washikiliwa kwa mahojiano.

== Liberia's Drug Enforcement Agency has arrested the head of the presidential motorcade for allegedly using an official vehicle to smuggle 297 kilograms (654 pounds) of marijuana into Liberia from neighboring Sierra Leone, officials said Monday.

The motorcade commander, Perry Dolo, was arrested over the weekend along with three other men after crossing from Sierra Leone via the town of Bo Waterside, said DEA Director Anthony Souh. The other three men were a Liberian official, a Guinean and a Sierra Leonean believed to be a member of the armed forces, Souh said. He did not provide further details about the men.
The vehicle used in the operation is known as "Escort 1," the jeep that normally leads the president's convoy, Souh said.

"He took the car during his day off to go do this thing. He was not on duty, but he used the official car," Souh said of Dolo.
Journalists were denied access to the suspects because they were still being interrogated at the DEA after their arrest by a joint force that included members of the Emergency Response Unit.

"They are still with me going through the process," Souh said. "We want to speedily send them to court as soon as possible because the case is too high. Using a presidential car? It's too big."
Liberia's DEA has in recent years tried to combat marijuana farming in Liberia's interior counties, which is primarily done for local sale and consumption. However, weak drug laws have made the practice difficult to curtail.

According to the 2012 World Drug Report from the United Nations Office on Drugs and Crime, 9 percent of Liberian high school students use cannabis.
———
abc News

Utata wa amani kati ya M23 na DRC, Mkataba wa amani washindikana




Shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu , iligonga mwamba.
Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.

Mpatanishi wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.
Hata hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi za upatanishi.

Kundi la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na Uganda.
Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.

Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo yatasainiwa. Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.

Serikali ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.
Duru zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.