Ulimwengu
unahuzunika kutokana na kifo cha Nelson Mandela,kiongozi mashuhuri aliyeingia
katika madaftari ya historia ya karne ya 20 kama "chimbuko la kuwapa watu
moyo wa kuthamini maadili,kusamehe na kusikilizana.
Nelson
Madiba Mandela
Msiba umetanda kote ulimwenguni
tangu zilipotangazwa habari za kifo cha Nelson Mandela.Bendera zimeshushwa nusu
milingoti katika kila pembe ya dunia.Na Siku hadi tatu za maombolezi kutangazwa
katika nchi nyingi duniani.Viongozi wa kimataifa wameelezea masikitiko yao na
kusifu mchango wa Madiba kama mtu aliyekuwa akipigania haki,uhuru na usawa
ulimwenguni.Rais Barack Obama wa Marekani anasema kwa kufariki dunia Nelson
Mandela,ulimwengu umempoteza mmojawapo wa binaadam mwenye ushawishi mkubwa
kabisa,mwenye moyo wa kijasiri kupita kiasi na mwenye imani kupita kiasi.Rais
Obama ameungama maisha yake yasingekuwa kama yalivyo ingekuwa dunia haijakuwa
na mpinzani wa zamani wa Afrika kusini aliyetumikia miaka 27 jela.
Rais Barak
Obama amenukuu yale yaliyosemwa na Madiba alipofikishwa
mahakamani mwaka 1964
"Nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa waupe na nimepigana dhidi ya
utawala wa kimabavu wa watu weusi.Nnapigania maadili ya kuwepo jamii huru na ya
kidemokrasia ambapo watu wote wataishi pamoja kwa furaha na kuwa na fursa sawa.Ni
Maadili nnayotaraji kuyaendeleza maishani mwangu na ikihitajika basi pi niko
tayari kufa kwaajili ya maadili hayo."
Hikma,Busara na moyo wa imani
ndizo sifa zake
Matamshi
kama hayo yaetolewa pia na kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliyesema jina la
Nelson Mandela daima litafungamanishwa na mapambano ya wananchi wa Afrika
kusini dhidi ya unyonyaji na kupinduliwa utawala wa ubaguzi wa rangi na
mtengano Apartheid.Miongo zaidi ya miwili jela haikumbadilisha Nelson wala
haikumtia chuki moyoni.Afrika kusini mpya imeibuka kutokana na wito wake wa
suluhu."Amesema kansela wa Ujerumani Angela Merkel.
Katibu
mkuu wa Umoja wa mataifa amemtaja Nelson Mandela kuwa ""Mtu asiyekuwa
na mfano katika kupigania haki.Hakuwa na kinyongo.Ameonyesha kinachowezekana
kutendeka katika dunia na katika kila mmoja wetu anasema katibu mkuu wa Umoja
wa mataifa Ban Ki Moon,aliyetoa nasaha watu wawe na imani na kushirikiana
kwaajili ya kupigania haki na utu.
Amerika
kusini rais wa Brazil Dilma Roussel amemtaja Nelson Mandela kuwa "mtu
mashuhuri mwenye ushawishi mkubwa kabisa wa karne ya 20.Amesema Nelson Mandela
ameongoza utaratibu wa maendeleo katika historia ya binaadam kwa busara na
mapenzi-utaratibu uliopelekea kumalizika enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano.
Malkia
Eliabeth wa pili wa Uingereza pia ameelezea masikito yake kutokana na kifo cha
Nelson mandela akisifu juhudi zake .Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza
anasema tunanukuu:"Juhudi zake ndizo zilizopelekea kuwepo Afrika kusini
yenye amani hii leo.
Na
waziri mkuu wa Uingereza David Cameroun anasema:"Nelson Mandela hakuwa
shujaa wa wakati mmoja tu ni shujaa wa enzi zote."
Amefuata
nyayo za Gandhi
Waziri
mkuu wa India ,Manmohan Singh amemtaja Nelson Mandela kuwa kiongozi aliyefuata
kweli nyayo za Mahatma Gandhi.
Sifa
na maombolezi yametolewa pia na viongozi wa Ufaransa,Australia,Mashariki ya
kati na Latin Amerika kusifu mchango wa Nelson Mandela nchini mwake na
ulimwenguni.
Mwandishi:Hamidou
Oummilkheir/Rduters/AFP
Mhariri:
Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment