Imekuwa
kawaida kwa nchi zilizoendelea kuzifanya nchi maskini kama Madampo ya kutupia
takataka zao. Kwanini hali hii? Siku ya jana hapa nilibahatika kupitia maeneo
ya Mwanjelwa hapa jijini Mbeya na kukutana na USED BETRY (Betri zilizotumiaka)
zinauzwa kama nguo za mtumba. Ukiwauliza wametoa wapi hizo used betry wanajibu
tunaagiza kutoka nje.
Kweli
nchi yetu ni maskini lakini sio kuwa jalala la electonic materials. Kwanini
haya yanatokea? Je na sisi tukifika wakati wa kuzalisha bidhaa hizo tutakwenda
kuzitupia wapi? Kwa sasa Tanzania kila kitu tunaagiza used. Nguo ni uzed,
Magari used, kila kitu nused. Patafikia mahali tutaletewa vyakula used ili tule
na tushibe.
Kwanini
tumekuwa wavivu wa kufikiri namna hii? Jibu unalo msomaji wangu. Amakweli
safari yetu bado ni changa sana, wenzetu wanakimbia sisi tunageuka nyuma na
kuanza kutembea kurudi nyuma? Mwambieni Mjomba nauli kamwe haitapatikana ya
kusafiria maana bado tu usingizini.
AUSI
CHIWAMBO
ausichiwambor@hotmail.com
No comments:
Post a Comment