Friday, August 9, 2013

PICHA ZA BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE HAPA MKOANI MBEYA. PALIVUTIA SANA

Hili ndilo jengo la Halmashauri ya Wilaya ya tunduru hapa mkoani Mbeya ndani ya majengo ya Nane nane.
 Wanatunduru pia Waliweza kutengeneza Ghala la kihifadhia mahindi, Nyugu, Karanga na Vnginevyo kama   unavyoliona kwa kiruga tunaita "CHIKUTI" katika picha tatu kushuka chini



 Hapa Chini ni picha ya friji ya Asili iliyoandaliwa na Wenyeji wa Wilaya ya Tunduru huko Mkoani Ruvuma katika maonesho ya Nane nane. Humu Ndani unaweza kuhifadhi Maji, Soda, Juice, Nyama na Vile vingine unavyoone vinafaa kuwekwa kwenye friji. Friji hii imetengenezwa na Mkaa wa miti

 Hii ni Bustani mfuko Ambapo mfuko huwekwa Samadi na Mchanga na kupandikiza mboga mboga.


                                                              Bustani ndani ya Tenga
                                   Mwonekano Halisi wa ustani ya Mfuko baada ya kupandwa vitunguu.



 Hii ni Bustani mlima kama inavyoonekana Hapo. Hicho ni kichuguu au mlima uliotengenezwa na kupanda chochote kile upendacho. Amakweli Palivutia

 Hapa chini ni Majengo ya Kufugia ng'ombe kama yanavyojieleza. Anayeonekana ni Rafiki yangu Bwana Sunh Emmanuel akiangalia technologia ya Tunduru









                                    Hapa chini ni Mabanda ya kufugia kuku yaliyojengwa kisasa






 Wananchi Mbalimbali Wakipata somo namna ya utengenezaji mbolea ya Asili inayozalishwa Tunduru yetu
                               Huu ni mfano wa tanuli lililotengenezwa kupata mbolea ya Asili
ELIMU HII UNAWEZA KUIPATA KUPITIA NAMBA YA BLOGU HII YA MATANGAZO

KATIKA SAFARI YANGU YA TUNDURU NILIKUTANA NA SHIDA YA MAJI KATIKA BAADHI YA VIJIJI.

 Hii ni Picha ya milima katika bonde la magemani lililopo Kijiji Cha Azimio kata Ya Mtina Wilayani Tunduru. Umbali wa Kutokea makao makuu ya Wilaya hadi hapo ni Maili 10. Huko chini ndiko yanakopatikana maji ya kunywa katika kijiji hicho.
 Hii ni Njia ndefu kulelekea yanakopatikana Maji. Maji hapa kijijini yanapatikana Umbali wa kilomita 2.5 kutoka mahali kijiji kilipo.
 Zile chini sio nyumba za Kuishi binadamu bali ni mashimo ya maji yanayotumiwa na Wananchi wa Kijiji Hicho cha Azimio
                                           Huu ni mwonekano wa Mbali yanakopatikana maji
 hii ni hali halisi yanakopatikana maji. Foleni za kuzidi. Hapa Neti zimegeuzwa na kuweza kusaidia kufunika visima vya maji ili takataka na Wadudu wasinywe maji na kuchafua nyakati za usiku
                                         Weusi wa jengo la miti ndilo shimo la maji yenyewe
                           Hili ni Shimo Halisi Na juu ni Ndoo ya Kutekea maji. na maji hapa ni foleni

 Foleni ya ndoo za maji zikisubili kupata maji katika bonde hili ili kukidhi haja ya majumbani




                        Baadhi ya Wakazi wa kijiji hicho waliokutwa wakifua karibu na mashimo ya Maji

 Huyu Ni mwnafunzi Wa shule ya Msingi Azimio akiwa amebeba maji kichwani ndoo mbili za maji
PICHA HIZI ZIMEPIGWA NA Ausi Chiwambo Wiki Nnne zilizopita baada ya kutembelea Huko Tunduru na kujionea Mengi aliyojionea


NA CHIWAMBO AUSI
Katika kijiji Hicho cha Azimio tatizo la maji ni la kihistoria. Kwa miaka mingi sana maji yamekuwa tatizo kupindukia huku hali ya majengo ya shule nayo ni ya kusikitisha. Kwa mara ya kwanza maji ya Visima vya DANIDA vilichimbwa miaka ya 1990-1993, ilifuata TASAF miaka ya 2000.

Asili ya eneo hili lipo juu ya mlima mkubwa na kipo juu ya mlima na aina ya udongo au mchanga unaopatikana hapo ni mwepesi na hufukia visima vya maji au mashimo ya maji. Maji hapa yanauzwa ndogo Sh 300 Tsh. Kule yanakotoka pia yananunuliwa. Idadi ya Mabomba ya kuchimbwa yanayofanya kazi ni machahce sana na hayana uwezo wa kudumu wiki Tatu bila ya kuhalibika. Mabomba au Visima viko vinne vyenye uchakavu wa vifaa.

Serikali ichukuwe tahadhari mapema kabla hali haijawa kubwa zaidi. Umbali kutoka mto mkuwa wa Msinjewe unaomwaga maji Mto Ruvuma kutoka kijiji hicho ni kilomita tatu.

KARIBUNI MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI SONGEA UJIONEE YALIYOTOKEA ENZI HIZO ZA VITA VYA MAJIMAJI NA HISTORIA YAKE

                                    Hili ni lango la kuingilia ndani ya Makumbusho ya Majimaji

 Huyo ni Ausi Chiwambo mmiliki wa Chiwambo's Blog baada ya kutoka ndani ya Makumbusho ya Majimaji

       Huyu ni Evance Silinu Rafiki yangu na nimemaliza Shule ya Sekondari Masonya miaka mingi iliyopita
 Huu ni Mnara wa waliokufa vita vya Majimaji. Juu ya Mnara huu kuna Sanamu ya Askari wa Kitanzania ambao ni Wananchi waliojitolea harakati za kuondoa utawala wa kikoloni Miaka kwa miaka iliyopita.




 Humu ni ndani ya majengo ya Makumbusho ya Vita vya majimaji na Nyuma ya majengo hayo upande wa kushoto kuna makaburi ya Wahanga Wa Vita Vya Majimaji iliyotokea miaka Mingi iliyopita katika historia.

Karibuni sana  Wadau Wangu Huko Songea kujionea Makumbusho ya vita vya Majimaji, Pia Tembelea mbuga za Wanyama, milima ya Mawe isiyokuwa na michanga au udongo, mapango ya milima, Misitu minene, Mito mikubwa inayotililisha maji mwaka Mzima ikiwemo mto Ruvuma. 

JENGO LA GHOROFA LA UDONGO KWA KUTUMIA NGUZO POLI HUKO WILAYANI TUNDURU, VIJIJINI

                       PICHA HII IMECHUKULIWA KOTOKA facebook Profile ya Hassan Namlia

Kwa Mara ya Mwisho Jengo kama hili nililiona Tunduru kijiji cha Angalia. Pia Azimio lilikuwepo miaka mingi iliyopita katika tarafa ya Lukumbule. Hii ni technologia ya Watu Wa kusini hasa maeneo ya wilaya ya Tunduru. Usalama wa hizi nyumba ni mdogo sana kwani hujengwa kwa kutumia miti poli ambayo uwezo wake wa kudumu haifiki kumi. Kama unavyoliona hilo jengo na miti yake kama nguzo za nyumba.

Hizi nyumba kwa maonyesho zinafaa lakini si kwa ajili ya kuweka makazi ya kudumu kwa sababu hazina vigezo vya kitaalamu katika ujenzi wake na ni rahisi sana kuporomoka kuto pale mvua zinapoongezeka na matokeo yake ni kuathiri maisha ya binadamu.