Friday, August 9, 2013

HISTORIA YA MJI WA KILWA PAMOJA NA MAJENGO YA KALE



Mwanzo wa Kilwa umekadiriwa ulikuwa mnamo 800 BK. Kuna kumbukumbu ya kimdomo inayosema: Watu wa kwanza waliojenga Kilwa Kisiwani ndio Watakata, halafu watu wa Jasi wa kabila la Waranga. Badaaye akaja Mrimba na watu wake. Halafu akaja Sultan Ali bin Selimani Mshirazi yaani Mwajemi. Akaja na jahazi zake akaleta bidhaa na watoto wake. Mtoto mmoja aliitwa Fatima binti Sultan Ali. Hatujui majina ya watoto wengine. Walikuja na Musa bin Amrani Albedu. (kutoka BBC: The Story of Africa - The Swahili).





Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu ya biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 BK Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.





Katika karne ya 14 -kati ya 1330 na 1340 BK- mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji. ajengo makubwa yalijengwa ikiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti kuu, nyumba ya kifalme ya Husuni Kubwa na mengi mengine.

Kuja kwa Wareno katika Karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne za 18. na 19. ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hii ulimaliza utajiri wa Kilwa.
 

 Sehemu ya jengo ambalo lilikuwa na ukumbi mkubwa wa kunadi bidhaa zikiwemo watumwa,pembe za ndovu,simbi,mbao na vyombo vya kufinyangwa kutoka bara la Arabu na Ghuba ya uajemi,kisha kuingiza kwenye ngarawa tayari kwa kusafirisha (Maelezo haya ni kwa ajili ya picha ya hapo juu). 

Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani la Afrika ya Mashariki wakati wa karne za 12-15 BK. Kwa hivyo, Kilwa ilikuwa mji mkuu Afrika mashariki kabla ya wazungu hawajafika kwenye bahari kuu la Hindi.

Kwa mujibu wa tariki ya Kilwa ambayo ni miongoni mwa matini ya kizamani sana yanayotoa historia fupi kuhusu sehemu hii ya Tanzania, Kilwa ni mji ulioanzishwa na kusimamishwa na wahamiaji kutoka Shiraz, huko Uajemi kwa siku za leo. Ni dhahiri kwamba matini haya ambayo jina la mtunzi wake limepotea ni aina ya masimulizi ya kusisimua akili ya msomaji kwa kuwa na hadithi ya kibuni.

Kwa hivyo, ingawa yana maudhui ya kuvutia sana kutokana na ushuhudio wake muhimu sana, tariki hizi hazisomeki kama insha ya kisayansi ambayo itakuwa imeandikwa kufuatana na nadharia tete yenye uthabiti. Mintarafu asili ya wahamiaji wa kwanza ambao walifika Kilwa, hatuna uhakika kwamba walikuwa wanatoka Uajemi, kama inavyodaiwa na tariki hii. Hapo tuwe makini sana.

 Kwa mujibu ya tariki hizi, inasemekana kwamba Sultani mmoja aliyeitwa Hassan bin Ali kutoka Shirazi ndiye aliyehama kule kwao wakati wa kuibuka aina ya mgogoro kati ya watu wake. Sultani huyo akaamua kuondoka na watoto wake sita. Kuondoka kwao huko kwenye bandari ya Siraf, walisafiri kwa jahazi saba kuelekea Afrika mashariki. Hapo inaaminika kuwa kila wakipita kwenye bandari ya kanda ya pwani, mmojawapo alivunja safari yake huku akiaamua kuweka misingi ya mji wake.



Ndiyo asili ya miji saba ambayo tunayo mpaka leo kwenye kanda ya pwani ya afrika mashariki : Mandakha, Shaughu, Yanba, Mombasa, Pemba, Kilwa na Hanzuân. Sultani mwenyewe alikuwa wa mwisho katika kusalia katika msafara huu, naye akakaa kisiwa cha Hanzuani ambacho kipo Ungazija. Mikasa hii na tukio hilo limejitokeza katika miaka kuanzia 957 mpaka 985 baada ya K. Inaaminika kwamba Kilwa wakati ule kilikuwa kisiwa kilichomilikiwa na wenyeji waitwao wamuli.

Kwa kuwa walikuwa hawana nguvu nyingi, walikubali kukiuza kisiwa chao kwa kukubali kupewa vipande vya ntandio. Hapo ndipo Ali bin Hussein alipochukua kisiwa hiki kwa ajili ya kukaa ikiwa ni pamoja na kujenga majumba ya kujitetea dhidi ya watu wa bara na miji mingine ya pwani.

 Kati ya mwaka 957 hadi 1131, Kilwa uliwahi kupambana na mji jirani uliokuwa unaitwa, kwa enzi zile, Shagh. Ghasia zile zikakolea, zikawa zikageukia zikawa vita kwa ajili ya kutawala himaya kubwa. Kilwa ukawa na sifa za fahari katika pande zote za Afrika mashariki kutokana na nguvu zake na mali yake ambayo ilikuwa inatoka bara la Afrika, pahala panapoitwa Sofala. Dhahabu ya Sofala, ambayo ilikuwa ni baadhi ya madini iliyopatikana kwa wingi wakati ule, ilikwenda kuchukuliwa na kuletwa Kilwa kwa njia ya kutembea kwa miguu. Misafara hii ilikuwa changamoto kubwa sana katika kutajirisha himaya ya Kilwa.




Hapo si kiwanja ila ni ukumbi amabo mnada ulikuwa ukifanyika,au sherehe zao watawala hao wa kiarabu walikuwa wakifanyia humo,kwa mbele kuna maji ni bahari ambapo kuna ngazi za kuteremshia bidhaa kuingiza kwenye ngarawa zao.fika ukajionee ni utalii nafuu zana wa kuona kisiwa cha kihistoria Tanzania. (Maelezo haya ni picha ya juu).
Hapo yupo mwandishi mwingine katika lugha ya kiarabu, Al-Mutahar bin Tahir al Makdisi, ambaye vile vile anatoa ushahidi mzuri wa kwamba nchi ya zenj – ambayo ni sehemu hii ya kanda ya pwani kwa enzi hizo – ilichangia sana katika usafirishaji wa dhahabu kutoka Kilwa kwenda Uarabuni kuanzia karne hii ya 10.

Kwa kifupi, wataalamu wa historia wamekubali kusema kwamba kilele cha Kilwa katika kujifaharisha kilianza karne 12 ikadumu hadi karne 15. Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.

Baharia maarufu ambaye pia alikuwa ni mwana historia hodari sana, Ibn Battuta, anathibitisha vilevile kwamba dhahabu ilikuwa inapatikana pia katika eneo lililoitwa Yufi, nchini mwa Limi (nchi ya kiajabu ambayo wataalamu wengine wanakisia ni pengine Nigeria). Zama zile zilikuwa za kudhabiti utawala wa Kilwa ambao ulipanua mpaka Mafia, Zanzibar na Pemba. Sultani Suleiman bin al-Hassan (1170-1189) aliwahi kukarabati majengo makubwa ya Kilwa kisiwani. Anajulikana sana kwa ujenzi aliouanzisha chini ya utawala wake ambao unaitwa Husuni mdogo. 

Enzi hii bado ilikuwepo chini ya nasaba (dynastie) ya Shirazi mpaka mwaka 1277, ambapo ni kipindi cha awamu nyingine iliyojitokezea katika nasaba ya Mahdaliya ambayo ilitoka Hadramau, Yemen. Karne 14 na mwanzoni mwa karne 15 zilikuwa nyenzi za fahari kubwa sana kwa sababu ya kufaidi na kujiimarisha kipindi kile cha nyuma ambacho Sultani Al Hassan bin Suleiman II (1331-1332) alipopata nafasi ya kuongeza nafasi ya kuswalisha swalat al ijumaa ikiwa ni pamoja na kujenga kasri inayojulikana kwa jina la Husuni Kubwa. 

                                                       Hii Ndiyo Ramani ya Kilwa
 Hicho ni kiberenge kilitumiwa na mmoja wa mwanaakolojia ambaye akikuwa akichimba ili aone masalia ya vyombo vilivyo kuwa zikitumika wakati huo na washirazi kisiwani hao wakati huo.aliyeshika kiberenge ni Bw.samweli mtembeza wattalii.

ZANZIBAR NA HISTORIA YA DINI YA KRISTO




WARENO 1500 – 1800

Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno.  Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.

Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar.  Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao.  Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba.  Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman.  Jeshi hili la Oman inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.

Baada ya miongo ya vita na maangamizo ambayo yaliyoshuhudi  kuwaka moto mji wa Mombasa, Wareno walirudi nyuma, na kurejea kuendea kusini, mbali na mafikio ya mashambulizi ya moja kwa moja ambayo yaliyotokana na pepo za miongo za jahazi (waarabu).
 

 PICHA ZA WATUMWA MJINI ZANZIBAR


OASISI YA UVUMILIVU (OASIS OF TOLERANCE)
  
Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu.  Malezi yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi.  Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari.  Alisimamia mipango  mikubwa ya upandaji miti, alichimba visima vya maji vyingi tu na kujenga nyumba nyingi ambazo zilitosha mamia ya wageni.  

 Sultan alitambua wageni watakaa na kujiliwaza katika Oasisi.  Na alijua kwamba biashara itakuwa na kufanyika katika eneo hili ikiwa litaimarishwa kwa vitu na mambo mengine pamoja na usalama.  Vile vile alitarajia na kutambua kwamba angelipata asilimia fulani inayotokana na shughuli za kibiashara zitakazo endeshwa Visiwani kama ni malipo ya kuviimarisha visiwa hivyi.  Aliwakaribisha na kuwaomba wafanyabiashara kutoka India kufungua matawi ya ofisi zao ndani ya Zanzibar ili kuimarisha biashara.  Wafanyabishara hawa wengi kutoka India walikuwa ni raia wa kiingereza hii ilikuwa ni kwa sababu ya kutekwa India na Uingereza.  

 Kwa maana hiyo, alianza kuwakaribisha maofisa wa kiingereza visiwani ili kuwakilisha maslahi ya raia hawa wahindi wa kiingereza.  Mara tu tena baadae alianza kuingia katika mikataba rasmi ya kibiashara na Serikali ya kiingereza na Serikali nyengine za Magharibi.

Majengo ya biashara yalijengwa ndani ya Mji Mkongwe na Kampuni za Kimarekani, Kijerumani, Ufaransa na na Kiingereza.  Bandari ya Zanzibar ilitoa huduma za fueli na kufanyia matengenezo Meli za kivita na vyombo vya usafiri vya wafanyabiashara.  Meli hizi zilileta mapote ya ziada ya watu wa magharibi ndani ya Zanzibar.  Kama ni makaribisho mema ya wageni wengi katika Oasisi yake.  Sultani aliruhusu watu wa imani zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda.

Akiwa Muislamu mwenye imani kamili, Sultani alionyesha mfano bora wa uvumilivu juu ya mahitajio  ya kidini ya watu wengine.  Wakati huo huo akijenga furaha na imani katika dini ya mababu zake, kwa bidii zote.  Warithi wake alifuata utaratibu wa Sultani Seyyid, wakiruhusu kuanzishwa mahekalu mengi tu ya kihindi, makanisa mawili, moja la kikatoliki na kiprostanti, sehemu za kimazishi za zoroastriani na misikiti kwa kila dhehebu kuu au dogo la kiislamu ndani ya mji mmoja.



1800 – 1900
WAKATOLIKI, MAKUNDI YA WAKIRISTO WASIOPENDA MIKUTANO ASMI, VITA AU GHASIA (QUAKERS) NA UJUMBE WA VYUO VIKUU KWA AFRIKA YA KATI ( UMCA)

Baada ya Wareno kurudi nyuma Wakiristo kidogo tu Wakigoa ndio waliobakia Zanzibar.  Wakiristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia Ibada lakini waliweza kuifanya hai jumuia yao kwa kwa kuifanya ibada zao kibinafsi.  Baadae katika miaka 1800 makundi ya watu wa wamagharibi yalianza kujumuisha wamisionari na wachungaji wamisionari waliokuwa wakipita pita mara chache na wachungaji katika meli bandarini.   

Katika mwaka 1844 wamisionari wa kikiristo zaidi wa kudumu waliwasili Afrika mashariki kwa kupitia mchungaji wa kilutheri Joseph Krapf na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili wa Jumuia ya kimisheni ya kanisa la kiingereza (English Church Missionary Society).  Wakifanyakazi, Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache mbeleni walitoa kamusi bora kabisa la Kiswahili lakini hawakuwahi kuanzisha kanisa ndani ya visiwa hivyi.

Ukuwaji wa harakati dhidi ya utumwa ndani ya Uingereza ulishajiisha raghba ya wamisionari wakiristo, ikikuzwa na hotuba ya David Livingstone aliyoitoa mwaka 1857 akiomba Uingereza kupeleka wamisionari na wafanyakazi Afrika.  David Livingstone alilingania kwamba mwisho wa utumwa utakuwepo tu kupitia “ biashara na ukiristo”.  Baadae Livingstone alitumia siku nyingi tu Zanzibar ambao alipatiwa nafasi ya kutumia nyumba ya Sultani.

Hotuba zake zilipelekea kuundwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu  kwa Afrika ya Kati (UMCA).  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati ulikuwa ni mashirikiano baina ya kitivo na wanafunzi waliopitia vyuo vikuu vya Oxford and Cambridge, ambao baadae tu waliungana na mashabiki kutoka vyuo vikuu vya Durham na Dublin.  Katika mwaka 1860 walimchagua Charles Mackenzie kama ni “Askofu wa Afrika ya kati” na ilipofikia mwezi wa Oktoba wa 1860 alikuwa njiani kuelekea huko Afrika ya Kati.

Lengo la ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) lilikuwa ni kufikisha dini ya kikiristo kwa watu wengi sana waliokuwa Afrika ya Kati, kuzunguka ziwa Nyasa, ambalo Livingstone alilizungumzia kwa ufanisi.  Kwa ajili hiyo, baada ya kufika Afrika Kusini Askofu Mackenzie na wafuasi aliokuwa nao walisafiri kwa boti mpaka mto Zambezi na baadae hadi mto shire kuasisi ujumbe wa mwanzo wa ujumbe wa vyuo vikuu kwa Afrika ya Kati katika Afrika katika sehemu iliyojulikana kama Magomero.




Wakati ujumbe huu na eneo lake ulichukuana na jina na ari ya jumuia mama, Ujumbe huu ulishuhudia   kushindwa kwa aina yake kutekeleza malengo yake.  Maradhi na njaa na ukame uliwakumba wamisionari wa mwanzo na kupelekea kufa kwa askofu.  Kundi hili lililazimika kuondoka katika eneo hilo ndani ya kipindi

cha miaka mitatu kwa sababu eneo hilo lilikuwepo mbali sana na upatikanaji wa bidhaa kutoka nje na vituo vya mawasiliano, eneo hilo halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya kwa wale ambao hawana uzoefu na mazoea na hali ya hewa ya hapo na pia eneo halikuwa na utulivu wa kisiasa.  Askofu mpya, George Tozer, kwanza alijaribu kuupeleka ujumbe maili 200 mafikio ya mtiririko wa mto kuelekea eneo la muanuko lakini hata hivyo eneo hilo mara tu  liligundulika kuwa halikuwa na mazingira mazuri ya kiafya na kwa hiyo lilihamwa kwa miezi hivi tu.

Wakichukua bidii za makusudi, ili kutorejea makosa yaliyopita viongozi wa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) waliangalia uwezekano wa kituo au eneo jengine ambalo litatumika kuweza kufika kati kati ya Afrika.  Maeneo mbali mbali yalifikiriwa kutumika kama Kisiwa cha Johanna,  maeneo katika mwambao wa Afrika Kusini lakini kwa bahati Zanzibar ilikubalika kutumika kutokana na muundo mzuri wa njia za mawasiliano, upatikanaji mzuri wa bidhaa za chakula na wingi wa upatikanaji nguvu kazi bora.  Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) uliobakia uliwasili Zanzibar tarehe 31/08/1864.



Ujumbe huu ulipowasili ulipokewa na wamisionari wakatoliki wa Kifaransa.  Wamisionari wa kikatoliki waliwasili mwanzo Zanzibar kwa kiasi ya miaka minne kabla ya wamisionari wa kiingereza.  Katika mwezi Septemba mwaka 1860 Abbe Favat ambaye alikuwa Mfaransa mdini  maarufu mwenye nguvu alitiliana mkataba na Seyyid Said kumruhusu yeye Abbe Favat kuhamishia Makao Makuu yake katika Kisiwa cha Reunion na kuwa Zanzibar kufikia mwezi Disemba kikundi chake cha “mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika makaazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani.  

 Jengo hili la watawa linasemekana na lilijengwa katika mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla.  Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200.

Ruhusa iliyotolewa na Sultan Majid kwa Wafaransa hawa kuanzisha duka ndani ya Zanzibar ilitafsiriwa kama ni juhudi za Sultani za kuweka “ uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nao Waingereza Zanzibar kwa kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa kizungu.”  

 Ikiwa ushindani wa kisiasa ndio uliompelekea Sultan Majid za kukaribisha pamoja matawi tofauti ya wamisionari wakiristo hata hivyo matokeo hayakuwa hayo kwani kwa upande wa wamisionari hawa hakukuwa na msuguano wowote.  Mahusiano yao mazuri makundi hayo mawili ya wamisionari ulitokana na ukweli kwamba Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati wa kianglikana (UMCA Anglicans) ulikuwa ni ujumbe wa watu watukufu ambao wenye mafunzo ya kikatoliki ya kiengereza (Anglon Catholic Learnings)



Wamisionari wakifaransa walikuwa makini kuepuka matatizo yoyote Zanzibar “kwa kutambua uhalisia wa maisha ulivyo ndani ya nchi ya kiislamu ya Zanzibar, Wafaransa kuanzia 1862 wafuasi wa Holy Ghost Order, waliamua kujikita katika maeneo maalum kama ya elimu, shughuli za uchungaji kwa jumuia ndogo ya mjini ya magoa wakatoliki na huduma za afifu na walifungua hospitali ya mwanzo iliyopendekezwa na Sultani ya kizungu.  Kwa hili waliojenga maoni mazuri kwa warabu.

Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibar hawa kidogo hawakuwa na azma yoyote kufuata imani ya wageni hawa wapya.  Wamisionari wa kikatoliki walilielewa hili lakini waliamini kwamba kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya kikiristo litaweza kupatikana masafa machache kuvuka mlango bahari wa Zanzibar huko Tanzania Bara.  Walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo katika mwambao wa Tanzania Bara katika mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao Tanzania Bara.  Harakati hizi ikiwemo ujenzi wa “ Hospitali ya Kifaransa”  ndani ya Bagamoyo.

“ Hospitali ya Kifaransa”  ndani ya Zanzibar ilijengwa mkabala na jengo la watawa.  Hospitali ilimalizwa kujengwa na kuanza kazi kufikia mwaka 1890.  Kipindi hicho wakatoliki walien delea kutumia uhusiano mzuri na majirani zao wa Zanzibar, wakipata ruhusa ya kujenga kanisa la mtakatifu Joseph katika mwaka 1894. (Cathedral of Saint Joseph in 1894).  Jiwe la msingi la kanisa hili kuu liliekwa tarehe 10 Julai 1896.  Misa ya mwanzo katika kanisa hili kuu jipya iliendeshwa na Askofu Allegeyer katika usiku wa krismas 1898.

Kadri ya wakati ulivyokuwa ukienda, hospitali hii ya Zanzibar ilipungua umuhimu wake na jengo hilo likafanywa kuwa ni skuli.  Hii ilikuwa ni skuli ya kitawa ya mtakatifu Joseph (St. Joseph Convent School).

Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) hawakuzubaa katika kipindi hichi.  Akianzia kwanza kuishi katika nyumba Mambo Msiige, katika eneo la Shangani, ambapo haikuwa mbali na ujumbe wa Kifaransa, Muingereza mchapa kazi shupavu alianzisha ustawi wa majengo ya ukubwa wa kuvutia na ya aina tofauti.  Kwanza walinunua sehemu ya ardhi ya kilimo Kiungani pembezoni mwa mji wa Zanzibar Kaskazini.  Ujenzi wa “bweni kwa ajili ya vijana watumwa walioachiwa huru” uliendelea katika eneo hilo kufikia mwaka 1866.  Karibu ya hapo mava sehemu ya kuzikia ilianzishwa, na hadi leo mava hii inayo baadhi ya mabaki ya wakiristo wa mwanzo wa Zanzibar.

Baadae ilinunuliwa ardhi nyengine katika mwaka 1873, ardhi hii ilikuwa karibu na kitovu cha mji ambalo ni jengo kubwa zima la mjini ambalo liliwahi kuwa uwanja wa soko kongwe, ambapo watumwa walikuwa wakiuzwa,  Mara wito ulitolewa wa fedha kusaidia ujenzi wa kanisa katika eneo hilo ambao uovu huo wa biashara ya utumwa ulifanyika.  Huu ulikuwa mwanzo kanisa kuu la kristo (Christ Church Cathedral).

Mwaka uliofuata Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA) walinunua ardhi ya kilimo Mbweni kusini mwa mji karibu na bahari.

Wamisionari wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya kati (UMCA) walipanga kujaza milki zao kwa majengo ya kidini na yasiyokuwa ya kidini.  Katika mwaka 1882 walianzisha ujenzi wa kanisa la parokia la mtakatifu John (St. John’s Parrish Church) huko Mbweni.  Karibu ya kanisa hilo walijenga kijiji na shamba dogo kwa ajili ya waliokuwa watumwa zamani na pia walijenga “Makaazi ya watoto wadogo wa kiume wa kilimani”,  ambayo baadae iligeuzwa  skuli ya wasichana.  Huko Mbweni walijenga karakana nyingi tu za elimu amali kwa ajili ya kuwafunza wafuasi wapya wa dini stadi muhimu na baadae kuwa Chuo cha kidini cha Mtukufu Mark,  ambacho baadae kilihamishiwa kiungani.

Jiwe la msingi la kanisa kuu la ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati (UMCA Cathedral) liliekwa mwaka 1873 katika siku ya siku kuu ya krismas katika eneo la mjini.  Uwanja wa soko kongwe ulianza kujazwa majengo ya ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati.

“Jumba la Mkunazini” lilijengwa katika mwaka 1875 na kanisa mara baada ya kujengwa jumba la kunazini lilihamisha makao makuu yake kutoka Mambo Msiige na kuwa Mkunazini.  Zahanati ilijengwa katika mwaka 1877, hatimae iligeuzwa kuwa hospitali yenye kutoa huduma kamili katika mwaka 1893. Skuli ya Mtakatifu Mon`ica, nyumba ya kasisi mkuu na Askofu ilijengwa katika uwanja wa soko kongwe.  Jengo hilo la skuli ya Mtakatifu Monica bado mpaka leo linatumika kama ni hostel/dahalia Mtukufu Monica.

Mwenye kustahiki sifa ya mafanikio haya ilikuwa hakika ni kanisa kuu la kristo. Mradi usio wa kibiashara ambao ulisimamiwa binafsi na Askofu wa tatu wa Ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati Edward Steere, utabakia kuwa moja ya mifano ya kuvutia na bora wa usanifu majengo ndani ya Afrika uliofanywa na wakiristo wa mwanzo.

Wakati eneo lake lilijazwa na haiba nzuri ya shinikizo la kidini, ukaribu wake na kijito kidogo chenye manukato ilisababisha baadhi ya watu kutia wasiwasi juu ya athari zake kwa afya za wamisionari.  Kijito hicho kidogo ambacho kilitambulika kama ni mfano wa mfereji wa venice huko Italy (Venetian Canal) kwa maelezo ya kikanisa kilikuwa kiukweli hasa ni topetope zenye kunuka wakati wa kupwa kwa maji.  Eneo hili liliacha kutoa moshi wenye kunuka na kudhuru katika miaka ya 30 (30’s) baada ya kijito hicho kufunikwa na barabara, moshi ambao uliendelea kujitokeza kwa masiku wakati wa kujaa  na kupwa maji.

Haiba binafsi ya ushiriki katika ujenzi wa Daktari Steer unaweza kuonekana na wengi juu ya mabadiliko aliyoyafanya kwa ramani zilizoletwa kutoka Uingereza na juu ya majaaliwa ya nguzo za mawe ambazo husimamishwa karibu na nyuma ya ukumbi wa kanisa.  Nguzo hizi zilitiwa kipindi ambacho Askofu alikuwa safarini Tanzania Bara kwa kazi za kanisa.  Kwa hivyo, utiaji huo wa nguzo hizo ulikosa usimamizi wake.  Wafanyakazi hao walizitia nguzo hizo kwa kusimamisha wima kama alivyoelekeza Askofu lakini kwa bahati mbaya walizigeuza juu chini juu.  Baada kurejea Askofu alizichunguza na kuamua zibakie kama zilivyo,kama zinavyoonekana leo.  Hii ilitokana na azma yake ya kushindikiza kazi iendelee bila ya kurudi nyuma.

Thamani hasa kubwa ya juhudi zake za usanifu majengo ni Paa la kanisa kuu.  Akikumbuka matokeo  yasiopendeza wakati akijaribu kufanya matengenezo la paa lililooza la kanisa lake kongwe la Kiingereza, Askofu Steer alidhamiria kujenga paa kwa kutumia muda mrefu.



Aliamua kujenga paa la zege badala ya kutumia mbao kwa sababu ya kuhofia mbao hizo kuharibiwa na mchwa na hatari ya moto na hakuweza kujenga paa hilo kwa kutumia vifaa vya chuma kwasababu hakuwa na fedha ya kugharimia.Alitumia vifaa vya kienyeji katika ujenzi, alichanganya saruji na kokoto katika juhudi zake za kujenga paa kubwa lenye upana wa futi 28.5.  Ilikuikamilisha kazi hii alitumia mbea moja ya chombo kilichotengenezwa Uingereza mbacho kililetwa hali ya kuwa hakijaunganishwa pamoja.   

Mashine hii iliekwa kwenye eneo la ujenzi ikiwa na viringi vilivyotiwa ili kuweza “kuzungushwa zungushwa kutoka sehemu moja kwenda nyengine pale ambapo kipande kimoja cha paa kinapomalizika kutiwa”.   Pale ambapo muhimili unapotaka kuondoshwa kundi kubwa la watu ilibidi kukusanyika pamoja.  Mkusanyiko huu wa watu unakuwa unatweta wakati vifaa vya kujengea jukwaa vinabomolewa, na huachwa kushangaa na kidogo na kukata tamaa pakiwa hapakutokea lolote.  Paa ambalo watu wote  hawakutegemea kuchukua muda bila ya kuanguka sasa limeweza kubakia zaidi ya karne moja/miaka 100.

Mfalme ambae kwa wakati huo alikuwa Seyyid Barghash alivutiwa sana na aliamua kutoa saa kubwa, ili kuupamba mnara wa kengele ambao uliwekwa pembe ya kusini magharibi ya jengo.  Kwa bahati mbaya haikuwepo saa katika ramani ya mwanzo.  Uamuzi wa busara wa kisiasa kupokea na kuiweka zawadi ya Sultani ulipelekea marekebisho kufanywa juu ya mnara na kuufanya mwembamba na mrefu zaidi.  Uamuzi huo kwa upande mwengine uliathiri pia zawadi zawadi nyengine ya seti nzuri ya kengele 25, seti za mlio wa saa ambazo ziliweza kupiga milio mirefu.  Hata hivyo ukubwa  na uzito wa seti hizo ulikuwa hauwezi kubebwa na mnara huo mwembamba.  Kengele 13 tu zilitiwa kwenye mnara huo na kengele  zilizobakia zilitawanywa kwa makanisa mengine na maskuli.

Wakati shughuli zote hizi zikiendelea katika kisiwa mama, wamisionari kutoka jumuia ya kirafiki ya kidini, the Quakers walianzisha makaazi karibu kabisa na kisiwa cha Pemba.  Quakers walifika Zanzibar mapema kufikia mwaka 1865, wakati huo walikuja kama ni waajiriwa wa kampuni za kibiashara za watu wa Magharibi.  Lakini Juu ya hivyo, mpaka ilipofikia  tarehe 20/Januari/1897 ndipo ujumbe wa kudumu wa Quaker ulianza mahala panapoitwa Banani ambapo ni karibu na kitivu cha ghuba ya Chake Chake mwambao wa Magharibi ya Pemba.

Kama  vile ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya Kati, kichocheo cha fedha kwa ajili ya ujumbe wa Pemba zilitokana na raghba za vita dhidi ya utumwa alizokuwa nazo kila Quaker.   Kuanza hapo tena baadae utumwa ulipigwa marufuku rasmi katika visiwa hivyi ingawa maisha ya wengi waliokuwa watumwa kabla hayakubadilika.Kwa wale watumwa waliohama katika maeneo ya wale waliokuwa wakiwamiliki walikosa makaazi ya kuishi na hofu kubwa ilienea juu ya kuwepo vikundi visivyofuata utawala wa sheria vikizunguka zunguka sehemu za ma shambani.

Ujumbe wa Quaker, kwa maana hio ilibidi uwe ujumbe “Chapakazi” ili watumwa walioachiwa huru waweze kupata kazi na kusoma biashara.  Kiongozi wa ujumbe huu Theodore Bartt bila hata ya kufika Pemba, alisema katika ukumbi wa mkutano ndani ya Uingereza “Ni jambo mwafaka na sahihi kwake yeye mtu alieachiwa huru kumiliki shamba kubwa ndani ya Kisiwa hichi na kuonyesha dunia/ulimwengu kwamba watu walioachiwa huru watafanya kazi kwa bidii na uaminifu na kuwa wastahamilivu na kujitahidi kujenga maisha yao."

Theodore Buft aliamini kwamba biashara na ukiristo ilikuwa ndio njia ya uongofu na kuweza kuweza kuelimika.


Watumwa na Waliobadili Dini

Ujumbe wa Quaker kwa Pemba ulikuwa ni mlolongo wa karibu zaidi wa wakiristo wa uasisi wa “Mji huru”  ndani ya Afrika ya Mashariki kwa ajili ya makaazi ya watumwa walioachiwa huru.  Kwa miaka, jeshi la majini la kifalme walileta makundi kwa makundi watumwa kwa kwa ujumbe wa Vyuo Vikuu kwa Afrika ya waliowakamata kutoka bahari kuu.  Watu hawa walioachiwa huru walikuwa rahisi kwao kugeuzwa na kuwa wakiristo na kwa kweli wengi katika wao waligeuka kuwa wafuasi wa dini ya kikiristo.

Lakini juu ya hivyo, wingi wa wakiristo hawa wapya na mahitaji yao maku bwa yalikuwa ni changamoto kwa raslimali na subira ya wafadhili wao.  Wakiangalia demografia wamisionari waliona njia pekee ya kuwahudumikia wakiristo wapya ni kuanzisha chimbuko la Padri wa kiafrika.

Kwa hivyo wote wakatoliki na waprotestanti walifanya bidii kuwajumuisha makundi ya kienyeji shughuli na mambo ya kanisa na hii yote ilipelekea kujua na kufunza mtumishi bora kwa ajili ya kuendesha shughuli za kidini.

                                           

Kwa Zanzibar harakati zote hizi zilikuwa katika eneo la Kiungani ambapo kwanza ilianzishwa “dahalia kwa watumwa vijana walioachiwa huru”, na baadae “Chuo cha Mafunzo ya ualimu cha Mtakatifu Andrew” na baadae “Chuo cha kidini/theolojia” kila moja kati ya hivyo kilijaribu kuwafunza na kutathmini matokeo ya vijana wa kiafrika.  Kiasi cha wanafunzi 50 kwa kipindi kimoja cha wakati waliishi na kusoma Kiungani.  Mitaala ilisisitiza heshima, elimu, imani na michezo.  Wanafunzi wazuri walifanywa kuwa walimu na wanafunzi bora kuliko wote walifanywa kuwa mapadri.

Jambo moja la kuvutia juu ya michezo iliyoanzishwa kwa ajili ya wanafunzi wa Kiungani ni kwamba ilifanya baadhi ya mashindano ya kwanza ya timu mjumuisho ndani ya Afrika.  Timu hiyo ya skuli mara walicheza dhidi ya makundi ya mabaharia wazungu.  Mchezo wa Kriketi ulianzishwa mwanzo katika mpira wa miguu lakini hata hivyo mchezo wa mpira wa miguu ulipendwa zaidi kwani makundi kwa makundi ya watu walikuwa wakikusanyika kuangalia mpira wa miguu.  Inaaminika kwamba kanisa iliendeleza michezo kusaidia kuwafunza waafrika maadili mapya ya jumuia, ufuataji wa sheria, kuweka wakati, kufanyakazi kwa pamoja na mashirikiano na maofisa husika.  Wanafunzi wa kizanzibari walicheza mechi/michezo hii kwa hamu na raghba na umahiri wao wa mchezo wa mpira ulijenga mshangao na fadhaa kwa wapinzani wao.  Lakini lisilosahaulika zaidi walilojifunza ni kwamba wao wanaweza kufanikiwa katika mchezo wowote na sio mpira wa miguu tu.
Source: http://www.zanzibarhistory.org

TINDIKALI TANZANIA KWA SASA NI JANGA LA KITAIFA


Na Chiwambo Ausi,


Zengwe la kumwagia Tindikali watu wa aina Mbalimbali Tanzania sasa limekuwa janga la kitaifa na ni wimbo wa Taifa kwa sasa. Huko nyuma tulitumia kwa shughuli za Kimaabara na mahospitalini lakini leo matumizi ya tindikali yamegeuzwa na kuwa silaha ya kuwaalibu watu sura zao, kuua kwa kutumia tindikali au kumwagia tindikali. Kwa sasa tindikali Tanzania imegeuzwa kuwa silaha dhidi ya watu fulani.

Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania tumeshudia namna watu wa aina Mbalimbali walivyomwagiwa Tindikali pasipo kukamatwa mtu yeyote yule. Kwa mfano, hivi majuzi Wazungu wawili kutoka Wiingereza wamemwagiwa tindikali na watu wasiofahamika. Pia katika chaguzi mbalimbali nchini ikiwemo ule wa Igunga ulitawaliwa na mada ya Tindikali.

Pia Waandishi wawili wa Gazeti la Kila wiki la Mwanahalisi (Lililofungiwa na serikali) akiwemo Saed Kubenea na mwenzake mmoja walimwagiwa Tindikali wakiwa ofisini. Watanzania Tujiulize, kwanini haya yanatokea? Kwanini wahalifu hao hawakamatwi? Je huu ni uzembe wa nani? Serikali haina budi kutafuta chanzo cha tatizo na kuzuia moja kwa moja.

Kwa miaka michache iliyopita Tindikali ilikuwa ni suala la kitaifa tu, ila kwa sasa wamevuka mipaka na kuwamwagia Tindikali hadi Wageni waliofika Tanzania kutoka nchi nyingine. Watanzania tulaani Vikali sana sulala hili kwani ni aibu ya kitaifa.
Mwandishi wa RFI Kiswahili Ndugu Emmanuel Richard Makundi alilipoti taarifa ifuatayo; Raia hao wawili wasichana wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 wanaaminika kuwa walikuwa wakifanya kazi za kujitolea visiwani humo na kwamba tukio hili ni la kwanza kufanywa kwa raia wa Kigeni.

Kaimu kamanda wa Polisi Visiwani Zanzibar, Mkadam Khamis amewaambia waandishi wa habari visiwani humo kuwa watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki waliwakaribia wasichana hao na kisha kuwamwagia tindi kali.
Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imekiri kuwa na taarifa hizo na kwamba wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia hao wanapatiwa matibabu ya haraka kuwanusuru na madhara zaidi ya acid hiyo.

Polisi wanasema bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba mpaka sasa watu waliohusika na shambulio hilo hawajafahamika ila uchunguzi bado unaendelea na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahusika.
Wizara ya mambo ya nje imesema kuwa zaidi ya raia elfu 75 wa Uingereza ambao huetembeala Tanzania kila mwaka, hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi yakuwalenga raia wakigeni jambo ambalo linahatarisha usalama wao.

Wizara hiyo imeongeza kuwa kumekuwa na matukio ya uporaji wa mizigo ya raia wa kigeni hasa kwenye baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine hali ambayo hivi sasa inaonekana kuota mizizi.

Hivi Karibuni watu wasiofahamika walimwagia tindi kali mufti msaidizi wa Zanzibar pamoja na kumpiga risasi padri wa kanisa Katoliki.”
Ni matumaini yangu kuwa serikali itasikiliza kilio hiki na kuchukua hatua stahiki ili lisije kujirudia na uwe wimbo uliopita na muda “The Song of the past”.

LEO WAISLAM WOTE DUNIANI WANASHEREHEKEA SIKUKUU YA EID MUBARAK. NAWATAKIA SIKUKUU NJEMA.


Saturday, August 3, 2013

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AZIMIO HUKO TUNDURU WASOMEA CHINI YA MITI NA OFISI YA KIJIJI

 Hili ni Moja ya Darasa linalotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Azimio kufundishwa na kujisomea. Jengo la Mbele katika kuta zake ni majengo ya shule yaliyojengwa Miaka ya 1970. Majengo hayo hayatumiki kwa sababu hayana paa na yalikuwa na nyufa kubwa kuweza kuhatarisha maisha ya wanafunzi wa shule hiyo iliyopo Kata ya Mtina Tarafa ya Lukumbule.
 Huu ni mwonekano Mwingine wa jengo hilo na darasa moja la wanafunzi wa darasa la Tatu wanaosomea nje ya majengo ya darasa kwa kuwa shule hiyo ina madarasa manne tu huku idadi ya wanafunzi ni kubwa na kukiwa na madarasa 7





Mbeya ya picha ni Jengo la madarasa mawili yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi kijiji hapo na hadi leo halijakamilika ujenzi wake.
Upande wa kulia ni Vyumba vya madarasa mawili yaliyojengwa na TASAF na nyuma kabisa ya picha ni Tanuli la Matofali yanayogeuka kuwa kichuguu ile hali wananchi waliandaa tofali hizo miaka mitatu iliyopita

Haya ni majengo yaliyohalibika kutokana na kuchakaa kwa kuta zake ambapo shule hiyo ilianzia na majengo haya miaka ya 1970




NA CHIWAMBO AUSI
Hayo ndiyo majengo ya shule ya msingi Azimio yakionyesha madarasa manne tu ya kusomea wanafunzi na vyumba vya nje yaani chini ya miti. Wananchi walijitolea kufyatua tofali ila hadi sasa zinaota kichuguu kwani hada sasa zina miaka Mitatu huku zikiwa zinaharibika. Tofali nyingi zimehariika na kutokana na asili ya udongo wa sehemu hiyo, matofali hudumu kwa muda wa miaka miwili tu kabla halijajengewa.

Ni hatari sana kuona wanafunzi kusomea chini ya miti ambako wanafunzi huzagaa kila mahali na kuleta picha mbaya katika suala zima la Elimu. Ni miaka zaidi ya 50 ya uhuru. Jengo linaloonekana kuwa zuri ni la Tasaf lenye madarasa mawili na ofisi moja tu na jengo lingine ni nguvu za wananchi ambalo lina vyumba viwili tu na ofisi moja.

Serikali ya Wilaya ya tunduru ichunguze suala hili la Elimu shuleni hapo na ichukue hatua haraka iwezekanavyo. Kutokana na muda wa kuwepo Wilayani hapo kuwa mchache nilishindwa kufanya mahojiano na Afisa Elimu wa wilaya hiyo. Taarifa ya mahojiano yangu na viongozi wahusika nitaiweka mwezi September baada ya kufanya mahojiano na viongozi wahusika. 

achiwambo@yahoo.com

Thursday, July 4, 2013

RAIS WA MISRI AMENG'OLEWA NA JESHI LA NCHI HIYO

BREAKING NEWS: Rais wa Misri Mohamed Morsi Amepinduliwa na jeshi la nchi hiyo. Source: The New York Times Newspaper