Wednesday, December 24, 2014

Kesi ya IPTL yapigwa kalenda hadi mwisho wa mwaka


Dar es Salaam. Kesi ya kupinga maazimio ya Bunge iliyokuwa ianze kusikilizwa leo imeahirishwa hadi siku ya kufunga mwaka Desemba 31, 2014.

Wiki iliyopita za kampuni za IPTL na Pan Africa Power Solutions (T) Limited  (PAP) kwa kushirikiana na Harbinder Sighn Sethi zilifungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kuomba zuio la muda la utekelezaji wa maazimio manane ya Bunge kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow.

Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu ambao ni Augustina Mwarija, Gadi Mjemas na Stella Mugasha jana ilipaswa kuanza kusikilizwa lakini iliahirishwa baada ya mawakili wa upende wa Jamhuri kuomba ahirisho ili waweze kujipanga.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo kwa madai kuwa wao walichelewa kupata maombi ya kampuni hizo hivyo walishindwa kuyasoma na kujibu.

Hivyo aliiomba mahakama kuiaihirisha kesi hiyo jana  ili waweze kusoma na leo wawasilishe majibu yao na kama upande wa pili na wenyewe utakuwa na cha kujibu  watajibu ili Desemba 31,2014 isikilizwe.


Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo,majaji wanaoisikiliza kesi hiyo walikubaliana na maelezo hayo na kuiahirisha hadi siku hiyo ya Desemba 31,2014.

Chanzo: Mwananchi

No comments: