Saturday, February 2, 2013
Friday, February 1, 2013
AJALI YAUA WATANO YAJERUHI 130 MBARALI MBEYA NI VIBARUA WA KAMPUNGA
WATU watano wamepoteza maisha na
wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori
walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha
Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30
asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga
Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji
huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha
Kapunga.
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema
kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa
madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu
kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda
kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa
katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi
ya majeruhi katika ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na
wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza
kufahamika kwa haraka.
Pcha Mbeya yetu na Kamanga
Source: http://francisgodwin.blogspot.com
Monday, January 28, 2013
“MAGAZETI YA UDAKU NI JANGA LA TANZANIA”
JOHN F. KENNEDY (1917-1963)
“There
is a traffic disadvantage in not having the abrasive quality of the press
applied to you daily. Even though we never like it, and even though we wish
they didn’t it, and even though we disapprove, there isn’t any doubt that we
could not do the job at all in a free society without a very, very active press”.
John F.
Kennedy (1917-1963).
MAKALA
YA CHIWAMBO
“MAGAZETI
YA UDAKU NI JANGA LA TANZANIA”
Nakubaliana sana na maneno ya
President J. F. Kennedy aliposema “kuna hasara kubwa sana kwa kutokuwa na
vyombo vya habari vye ubora. Do you know why? Vyombo vingi vya habari nchini
vinapotoa zaidi habari za udaku inachangia mawazo ya watu kudumaa na kushindwa
kufikiri nini tufanye ili kujiletea maendeleo ya mtu binafsi. Hizi gazeti au tv
zenye ubora kwa kawaida hazipedwi. Kwa mfano Nchiya Tanzania kuna gazeti la
Raia Mwema, Mwananchi, The citizen, The Gudian, Nipashe na hata lile
lililofungiwa na serikali Gazeti la Mwanahalisi, ni watu wachache ndio wanaosoma gazeti
hizi.
Pia hata Wasomi wetu vyuoni
wahasomi. Walio wengi wanasoma magazeti ya udaku na yale ya sport. Pamefikia
mwanafunzi unamuuliza hivi leo kuja jambo gani limefunika sana vyombo vya
habari mbalimbali. Atakujibu do you know what? Muda sina.
Huyu mwanafunzi wa chuo kikuu anasema
muda wa kusoma gazeti ambazoni quality News anasema hana time ila kwenye
michezo hata akiliona la juzi au mwakajana anatamani liwe lake asome. Ninyi kama
tegemeo letu la taifa mnadhani tutafika kweli.
Mara nyingi utasikia “RAIS AFANYA MAUAJI
YA KUFURU”, CHIWAMBO ZE DOCTOR KAFUMANIWA LIVE, WAZIRI AUSI KAKUTWA NA PEMBE ZA
TEMBO”. Mmmmmmmmh!!!! Ingia humo ndani usomo uone utumbo uliopo. Hauendani na
kitu wanachozungumzia. Eti Rais wanayemzungumzia ni Yule wa wajinga Chikaje
street.
Kwanini waandishi kama hawa wasifungiwe
tu. Je elimu yake ina faida gani. Kama ana “LAW DEFORMATION” kwanini anashindwa
kuandika kitu kinachoendana na hali halisi. Ama kweli “KILIO CHA SAMAKI MACHOZI
HUISHIA MAJINI”. Huwezi kuona watanzania wanatesekaje huko chini. Wewe mwandishi
wetu taifa linakutegemea sana.
Kulaumu wanafunzi nao sio zuri bali
tuangalie zaidi kwa hawa waandishi uchwara wa magazeti yetu. Pamefikia mahali
mtu uachoka hata kusoma gazeti husika kwa sababu mwandishi anaonekana
anapendelea sana chama Fulani, au sehemu Fulani.
Kwa mfano Tv zilizonyingi Tanzania kama
vile Cloud Tv pia wanaangalia zaidi taarifa za majijini na mikoani. Hivi jiulize
mara ngapi wanaripoti habari za vijijini. Hikinacho kinachangia kupoteza ubora
wa tv zetu. Hata hizi tv media nyingine nazo ni vile vile wanaangalia zaidi Dar
es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya. Hivi kule Kigoma, Rukwa na Mikoa ya kusini
mbona hawalipoti matukio kama kule mijini.
Ukweli ni kwamba vijijini watu
walio wengi wanateseka; hawana huduma za jamii. Umeme kwao ni ndoto. Wanauona wakiwa
mjini tu. Kwa msingi huo serikali inataka kufungia matumizi ya analogia bila
kuangalia hawa wanakijiji ambao ni asilimia 80% ya Watanzania kweli wataweza
kutumia digitari. Kama chakula tu ni shida je mtu alipie king’amuzi ataweza.
Watanzania vijijini wamekata tamaa. Hawana wa kumweleza shida zao,sauti
yao imefunikwa na waandishi uchwara ambao wamenunuliwa. Nakumbuka kwamba
kipindi nasoma St. Augustine university of Tanzania 2011 katika kozi ya NEWS
REPORTING chini ya Mwalimu wangu Madam Mushi,
alinifundisha namna ya kwenda kupata taarifa vijijini. Hapo ndipo
aliponikalilisha kuwa maana ya Jonalist “Is the voice of the voiceless”. Hatu
Lecture wangu Denis Mpagaze pia alikuwa analizungumzia sana neon hili.
Mimi naweza kujiita ni mwanafunzi
wa Danis Mpagaze kwa kuwa amenifundisha. Huyu ni Msomi nan i Mwandishi ya
jarida la “Physiognomy” pia ni Lecture st. Augistine University-Mwanza.
Nilifurahia sana na Documentary zake ambapo alituonyesha mwanga juu ya Uandishi
wa habari kwa kutuonyesha documentary ya “Mto tigite” namna watu walivyopalika
ngozi na kugeuka kuwa rangi tofauti na walizonazo.
Ukiangalia documentary hiyo utaona
namna watanzania vijijini walivyokata tama. Hawana imani na hata viongozi wao
kwa kukosa kuwatetea. Haya nimeyathibitisha baada ya kutembelea kijiji kimoja
cha wilaya ya Newala kijiji cha Kitangali A, pia hata maeneo mengine ya kusini
kama vile kijiji cha Mtama (Masasi), Namakambale B, Azimio,(Tunduru).
Hivyo somo langu la bure kwa
waandishi wa habari ni kwamba mutembelee vijijini kuliko mijini.
AUSI CHIWAMBO
TEKU UNIVERSITY
MBEYA
ausichiwambor@gmail.com
PICHA HALISI ZINAZOONESHA KUANZA KWA MAANDAMANO MTWARA SIKU YA KWANZA MWISHONI MWA MWAKA 2012 HADI SASA
Mwanzoni mwa maandamano yaliyotokea Mtwara yalipambwa na Mabango ya aina hii. Hii ni siku ya kwanza ya maandamano.
Haya ni mabango mengine
Hizi ni nyaraka za serikali zikiungua moto mjini Masasi Juzi
Wauguzi wa Hospitali ya Ndanda wakisubili majeruhi
Nyumba ya Mbunge wa Jimbo la Masasi,Mariam Masembe ambayo ilichomwa moto juzi na watu wenye hasira. Vitu mbalimbali viliharibiwa.Picha na Mpiga Picha Maalum-Mwananchi
HILI NI GARI LILILOCHOMWA MOTO IKISEMEKANA GARI HILO LILIKWENDA KUMFUATA BIBI (Upande wa kulia) ALIYESEMA KUWA WAKIAMISHA GESI KWENDA DAR ES SALAAM ITAGEUKA KUWA MAJI
Hili ni gali la kubebea wagonjwa
Huu ni siku ya kwanza maandamano yalianza kama inavyoonekana wakiwa na mabango yao yaliyoonesha madai yao
Hii picha imechukuliwa kutoka Masasi
Nyumba ya Mbunge wa Jimbo la Masasi,Mariam Masembe ambayo ilichomwa moto juzi na watu wenye hasira. Vitu mbalimbali viliharibiwa.Picha na Mpiga Picha Maalum-Mwananchi
Subscribe to:
Posts (Atom)

















































