Sunday, January 27, 2013

MAGAZETINI LEO 27-01-2013












Friday, January 25, 2013

st.johns university walipoandamana Mjini Dodoma










Wanachuo wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa hii ni kushinikiza ulinzi kwa sababu ya matukio ambayo yanaendelea kutokea maana juzi alifariki mwanachuo na usiku wa kuamkia leo wanachuo walivamiwa vyumbani  baada ya kukata nondo ya dirisha na kuiba Laptop tatu na simu tano na baada ya kuchukua vitu hivyo waliacha wamewafanyia vitendo vibaya na pia waliachwa wamefungwa ili wasipige kelele.
Kwa hali hii  imesababisha maandamano ili kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John kilichopo Dodoma mjini.

Source:www.mjengwablog.co.tz

MAGAZETI LEO25-01-2013












FUJO ZILIZOTOKEA MKOANI PWANI, KIBITI, RUFIJI ZITAFUTIWE UFUMBUZI

HAWA NI WANANCHI WA KIBITI JANA MCHANA WAKIVAMIA KITUO CHA POLISI KWA LENGO LA KUKICHOMA MOTO

Source: michuzi.blogsppot.com

Kwa sasa imeonekana ni hali ya kawaida watu kujichukulia uamuzi mikononi. Mwizi akikamatwa kuchomwa moto au kupiga hadi kuua. Maandamano kila kukicha Tanzania hadi inaleta shaka sana kuhusu uwajibikaji wa vionozi wetu. je wananchi wanasikilizwa kweli shida zao?

Wednesday, January 23, 2013

TANGAZO LA MMILIKI WA BLOG YA TEKU-BASO'BLOG

TANGAZO: KUANZIA LEO BLOG YA sociologist-baso.blogspot.com haitafanya kazi badala yake Munaombwa kuitumia hii blog ya Chiwambo.blogspot.com. bLOG YA MWANZO ITAKUWA KAMA SEHEMU YA HISTORIA. Ila kwa wasomaji wa maswali ya Baso munaruhusiwa ila hakutakuwa na habari mpya kama ilivyozoeleka na unaweza kupata maswali yako kupitia blog hii. kwa sasa tunapatikana kupitia

Chiwambo.blogspot.com

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA

By Chiwambo

VITUKO VYA WAKUBWA HII NDIYO MOJA YA HOTUBA MBAYA ZA P. w. BOTHA



Ƙ Akiri kuwaua kwa weusi kwa sumu
Ƙ Mweusi ni malighafi ya mweupe

HABARI KAMILI
Hii ni hotuba ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, p. w. Botha alipohutubia baraza lake la mawaziri wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo. Katika hotuba hiyo iliyochapishwa na gazeti la “SUNDAY TIMES” la nchini humo toleo la Agosti 18, 1985, Botha anapojigamba eti ardhi hiyo ni mali yao na haipaswi kuingiliwa.

Ikumbukwe kuwa katika utawala huo, mtu mweusi aliteswa na kunyimwa haki zake za msingi na alifanywa kuwa kiumbe dhaifu kisichostahili kuishi kwa raha katika nchi hiyo.


“Kaka zangu na dada zangu, Pretoria imetengenezwa na watu weupe kwa ajili ya watu weupe na hatuna haja ya kuuthibitisha umma au mtu mweusi kuwa sisi ni watu bora, tumekuwa tukiwaambia  watu weusi jambo hili kwa njia elfu.

Africa kusini ya leo haikutengenezwa katika mawazo ya kawaida, tumeitengeneza kwa kutumia akili nyingi, jasho na damu. Mnaposema kuwa tunawabagua weusi sielewi.

Hivi ni Afrikaners ndio waliojaribu kusitisha kizazi cha Aborigines wa Australia? Je ni Africaners waliotenga na kuwanyanyasa watu weusi Marekani kasikazini kwa kuwaita niggaz?

Je, ni Africaners waliowatenga na kuwanyanyasa watu weusi huko England kwa kuwatungia sheria ya kuwakandamiza? Canada, Ufarasa , Russia, na Japan nao wana njia zao za kibaguzi. Hivi kwanini hasa kuna kelele nyingi dhidi yetu? Huu ni uendawazimu! Kwanini wanatukaba koo kiasi hiki? Hawatundendei haki hata kidogo.

Nataka kuwaeleza kuwa hakuna kibaya tunachokitenda hapa ambacho hao wanaojihita wako katika dunia ya ustaarabu wameacha kufanya. Sisi ni watu wema tusio na hatia na ambao tumeweka wazi mfumo wa maisha ya tunayotaka tuishi kama watu weupe.

Sisi sio wanafiki kama wazungu wenzetu wafanyavyo kwamba wanapenda watu weusi.

Ukweli kuwa weusi wanaofanana na binadamu na kutenda mambo kama binadamu hayawahalalishi kuwa wao ni watu wenye akili timamu au binadamu aliyetimia. Kanunguyeye si nungunungu na mijusi hawawezi kuwa mamba kwa sababu eti wanafanana.

Kama mungu alitaka tufannane na weusi angetufanya wote tuwe na rangi moja na fikra sawa. Lakini alituumba tofauti, weupe, weusi, wanjano, watawala na watawaliwa. Katika upeo sisi ni bora kuliko weusi na hilo halina ubishi kwani limejidhihilisha kwa miaka mingi iliyopita.

Naamini kuwa Africaner ni mtu safi, mwenye hofu na mungu. Ni mtu mbaye ameonyesha kwa vitendo njia sahihi ya utu. Hata hivyo inafurahisha kuona Ulaya, America, Canada, Australia na wengine wengi wako nyuma yetu achilia mbali maeneo yao.

Kuhusu uhusiano wa kidemokrasia, sote tunafahamu lugha inayotakiwa kutumika. Na kwa ushaidi ulio wazi hivi kuna mtu hapa asiyejua kuwa nchi nyingi za Ulaya zina tamani kuwekeza Afika kusini.

Nani anayenunua dhahabu yetu, nani anayenunua almasi yetu? Nani anafanya bihashara nasi? Nani anatusaidia katika kuendesha siraha za nyukilia? Ukweli ni kwamba sisi ni watu wao na wao ni watu wetu. Hii ni siri kubwa. Nguvu ya uchumi wetu inajengwa kwa kiasi kikubwa na America, Uingereza, na Ujerumani. Ni jambo kubwa sana hili na kwa maana hiyo, mweusi ni malighafi kwa mweupe.

Hivyo basi, kaka na dada zangu hebu tuungane kumpiga vita huyu mweusi. Napiga mbiu kwa Africaners wote kujitokeza kwa hali na mali kupigana vita hii. Kwa hakika mungu hawezi kuwatupa watu wake ambao ni sisi. Hadi sasa imeonekana kwa vitendo kuwa weusi hawawezi kujitawala. Wape bunduki kama hawataanza kuuana.

Hawana lolote jema isipokuwa mashujaa wa kupiga kelele, kucheza ngoma, kuoa wanawake wengi na kupenda sana ngono. Hebu sasa tukubali kuwa mtu mweusi ni alama ya umskini, udumavu wa akili, uvivu na aliyekosa ushindani. Hivi hapo je, si kweli kwamba mtu mweupe aliumbwa ili kumtawala mtu mweusi? Hivi utajisikiaje unaamka asubuhi unakuta Kaff*ir amekaria kiti cha utawala? Hivi unajua kitakachotokea kwa wanawake wetu? Hivi kuna mtu anaweza kwamba mweusi ataitawala nchi hii.
                         
Kwa hiyo tuna sababu nzuri ya kuwapeleka akina Mandela jela waozee huko na katika hili nadhani upo umuhimu wa kupewa pongezi kwani tungekuwa na uwezo wa kuwaangamiza lakini sasa wanaishi.

Napenda kuwatangazia mikakati mipya ya kuwaangamiza hawa weusi. Tutumie sumu kuwamaliza.

Kamwe tusirushusi idadi ya watu weusi iendeleekukua vinginevyo tutakwisha. Tayari nimeshawaleta wanasayansi ambao wamekuja na sehemu kubwa ya mzigo wa sumu na ninawasaka watafiti wengine zaidi waangalie sehemu murua za kuitumia sumu hiyo kwa lengo la kuwaangamiza weusi.

Sehemu nzuri za kuwaangamiza kwa sumu ni hospitali na pia katika usambazaji wa chakula inaweza kutumika. Tumetengeneza sumu inayoua taratibu na kupunguza uwezo wa uzazi. Lakini hofu yetu ni kwamba itakuwaje kama sumu hiyo itaangukia mikono yao.

Hata hivi tunafanya kila yuwezalo kuhakikisha kuwa sumu hiyo inabaki katika himaya yetu. Pili, watu weusi wanapenda sana pesa kwa hiyo tunaweza kuwatenga kwa njia hiyo. Wataalamu wetu wanalifanyia kazi suala hilo ili mtu mweusi amchukie mweusi mwenzake.

Hawana upeo wa kufikiri na huyo ndiye kiumbe dhaifu kisicho na akili ya kuona mbali.

Kuna umuhimu mkubwa wa kupanga mambo hayo yaendelee kwa muda mrefu ili wasibaini kuwaua. Kwa kawaida mtu mweusi hapangi mikakati inayozidi mwaka mmoja. Na hapa napenda niwaombe kina mama wa ki Afrikaner wazae kwa fujo kuongeza idadi.

Litakuwa jambo la maana pia kama kutatengwa vituo maalumu ambako vijana wa kike na kiume watakaa na serikali kuwawezesha ili wazae kwa idadi kubwa iwezekanavyo ili kuongeza idadi yetu. Wakati hilo likiendelea, lazima tuwabane watu weusi waachane na wake zao.

Ninayo kamati inayoratibu na inayoangalia njia nzuri ya kuwafanya watu hawa wachukiane na wauane wenyewe kwa wenyewe. Adhabu kwa mweusi aliyemuua mweusi iwe ndogo ili kuwapa hamasa ya kuendelea na mauaji.

Wanasayansi wangu wameshauri pia kuna ulazima wa kuwawekea sumu kwenye pombe, sumu ambayo itakuwa inawaua taratibu na kumaliza uwezo wa kuzaa pia. Njia kama hii na nyingine zifananazo na hii itawarahisisha kuwapunguza idadi.

Rekodi zinaonyesha pia kuwa mtu mweusi anapenda sana mwanamke mweupe. Hii ni nafasi nzuri kwetu. Wanawake wetu warembo wanaotumika katika mbinu za kuwaangamiza wapinzani wetu watatumika kuwaua hao wanaopinga ubaguzi wa rangi.

Hili jeshi letu la mwituni la mapenzi huku tukiwa na jeshi kama hilo kwa upande wa wanaume ambao watatafuta wanawake weusi. Pia serikali imeagiza Malaya kutoka Marekani na ulaya kwa ajili ya kukidhi haja yao.

Ombi langu la mwisho ni kwamba wajawazito wanapozaa hospitalini, watoto lazima wauwawe pindi tu wanapotoka tumboni. Hatuwalipi wale wauguzi kwa ajili ya kutuletea watoto weusi katika dunia hii bali kuwaangamiza.

Serikali yangu imetenga fungu maalumu la pesa kwa ajili ya kufanikisha mpango huo. Pesa inafanya lolote na kwa vile tunazo tuzitumie ipasavyo.

Kwa muda huu ndugu zangu weupe, msiyaweke moyoni wala msione aibu kuitwa wabaguzi na wala sijali mhandisi wa Mfalme wa ubaguzi.

Siwezi kugeuka nyani eti kwa sababu mtu kaniita nyani. Nitabaki kuwa nyota inayong’aa ….mtukufu Botha.

Leo naondoa mawingu; kesho nitajalibu mlima”.

HABARI HII ILIWAI KUTOLEWA NA GAZETI LA RAI, OKTOBA 19-25, 2006. UK. 17.

IMELETWA KWENU NA CHIWAMBO AUSI R (TEOFILO KISANJI UNIVERSITY-TEKU, BA SOCIOLOGY AND SOCIAL WORK) 18, March, 2012.

MAWASILIANO:-



MCHAKATO WA UCHAGUZI 2015 USIWE MBEBWE KIASI CHA KUSHINDWA KUFANYA KAZI ZENYE MASLAHI KWA UMMA.



 MAKALA YA CHIWAMBO
Katika Makala ya Chiwambo leo inazungumzia zaidi juu ya utendaji kazi wa watumishi wa umma, wanasiasa, na namna vyombo vya habari vinavyotumika visivyo ili kutetea maslahi ya wachache. Hili linajitokeza kila uchaguzi hasa kuanzia Mwaka 2005, 2010, na inavyoonekana 2015 nayo ipo vivyo hivyo. Wananchi hugawanywa vipande vipande katika makundi mbalimbali huku makundi hayo yote husimamia maslahi ya kundi husika.

Katika nchi yetu kwa bahati mzuri hatuna Ukabila kama kule Nchini Kenya ambapo nchi hiyo katika kila chaguzi utawala suala la ukabila. Lakini huku kwetu Tanzania makundi ndiyo tatizo kubwa ambayo lengo kuu ni kushika hatamu ya kuongoza nchi. Wakati huu karibu kila chama kinazunguzia zaidi kuhusu uchaguzi 2015. Nani atakuwa Rais ajaye sio kwa chama tawala tu bali hata chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Viongozi wetu inavyoelekea hasa wale wanaohitaji Urais 2015 wameanza kujisahau. Wamesahau wapiga kura wao na kuzungumzia zaidi suala la uchaguzi mwaka 2015. Swali la kujiuliza ni kwamba je wananchi munawatumikia kweli? Panafikia mahali mtu unapata mashaka juu ya utendaji wao wa kazi. Magazeti wameyatawala kwa kuandika zaidi habari zao za uchaguzi 2015 na nani atakuwa mbabe katika uchaguzi huo.

Ukweli ni kwamba wananchi hatupendi kuona nchi inalumbana juu ya nani atakuwa Rais ajaye Mwaka 2015 badala yake muwatendee haki hawa Wananchi waliowafanya muingie hapo Mjengoni. Katika tafsiri ya mwandishi wa habari inasema kwamba ni “The voice of the voiceless” au Watch dog of the Government”. Hii inamaana kwamba mwandishi wa habari ni mtu anayewasemea wananchi ambao hawana pa kusemea.

Wananchi walio wengi Tanzania hasa wale wa vijijini hawana wasemaji licha ya kuwa na wabunge ambao huwakilisha wilaya hizo na wanaonekana kwao uchaguzi hadi uchaguzi. Sasa huyu mwandishi anatakiwa kuwa msemaji na mfichuaji wa maovu na mazuri yote yanayofanywa na Wananchi, kikundi cha watu, pamoja na kuikosoa serikali iliyopo madarakani kwa kuonesha kwamba hapa bwana mkuu hujafanya vizuri na hapa umefanya vizuri.

Lakini kwa sasa waandishi wa habari wetu wamewageuka wananchi. Na wamebadilisha maana halisi ya Mwandishi wa habari ambapo wameifanya kuwa “Journalist is a person who deal with the viceveser of the voice of the voiceless”. Inamaanisha wanajadili zaidi suala la kwamba mwandishi wa habari na kazi yake ni kuweka kinyume cha tafsili halisi ya kuwasemea wale wasio na sauti na badala yake kusimama upande Fulani wa kundi analoliamini yeye ili kutetea maslahi ya mtu binafsi kunyakua kiti cha uraisi 2015.

Hili ni balaa nan i janga kwa taifa la leo na kesho. Matokeo ya vyombo vya habari kuwa wapiga debe kwa viongozi wa aina Fulani ni bomu ambalo litakuja kuwalipukia wenyewe hapo baadaye. Waandishi wenzangu mulio wengi mumekuwa ndumila kuwili na watawaliwa wa fikra zenu. Inaonesha namna gani elimu muliyonaye haisaidii Taifa letu badala yake unafuata matakwa ya wachahce wenye fedha na wanasiasa.

Wewe mtaaluma wa masuala ya uandishi wa Habari, iweje ufundishwe nini cha kuandika na mtu ambaye hata taaluma yenyewe ya uandishi wa habari hana na hajawai kuisoma. Na wengine hata tafsiri ya neon lenyewe Journalism halijui. Sasa inakuwaje kikundi hiki cha watu kitawale sanaa ya uandishi wa habari. Kwa msingi huu mutaendelea kununuliwa siku hadi siku, maisha hadi kiama. 

Kwa mabo kama haya munakaa vikao na kusema hatuna uhuru wa Habari nchi. Kama unakubali kununuliwa na ukanunulika unadhani uhuru utakuwepo kweli? Tumezichoka habari za kusikia hatuna uhuru wa vyombo vya habari nchini huku ninyi wenyewe mkiwa mstari wa mbele kuwasaliti wananchi. Munategemea nini? Fedha za leo zitawatawala ninyi wenyewe hapo kesho. Mara nyingi ninyi munakuwa mstari wa mbele baadaye kusema kiongozi huyu ni mbaya, hafai na kumwangika vichwa vya habari vya kumkejeli baada ya kupata madaraka.

Kama mimi ningekuwa ndiye Rais wan chi hii ningemshinikiza waziri anayehusika na masuala ya vyombo vya habari andaye mswada mpya zaidi wa kuvinyonga vyombo vya habari ili wakose uhuru zaidi. Kwani kiasi cha uhuru uliopo wameshindwa kukitumia. Mambo ya kuzungumzia yapo mengi ten asana kila kona. Hivi swali lenu ni hili, je umewai kutembelea vijijini kule na kuona nyakati za mvua wanaishije? Wanakula nini? Adha gani wanayokutana nayo?

Hivi ni kweli vitu vya kuzungumzia kwenye vyombo vyenu vya habari (Media) vimekwisha kabaisa? Au munataka wananchi waandamane pamoja na kuwalamba mboko ili muandike habari zao na muwatumikie vyema? Hivi munadhani hiyo elimu yenu bila wananchi mungeza kuipa? Utitili wa magazeti sasa unathibitisha usemi wangu kuwa wanaripoti habari mbalimbali ili kulinda maslahi ya watu wachache badala ya umma.

Mutazame maeneo ya Ngorongoro watu wanavyoteseka na Njaa, Tunduru hadi leo korosho hazinunuliwi na wananchi hawajui lini zitanunuliwa huku watu binafsi wakinunua kangomba za korosho kwa bei ya shilingi 500 kwa kilo. Ninyi waandishi muko wapi? Kwanini musiripoti habari kama hizi zinazooneka ni za ulanguzi. Maisha ya wanatunduru msimu huu wa mvua yanakuwa hali tete? Chakula chao kikuu ni ugali wa muhogo wa wa kuloweka kwenye maji na kukausha ambao hauna virutubisho mwilini. Na mvua zinapochanganya watu hushindwa kula na wengine hushindia miogo ya kupika au uji.

Nakumbuka mwalimu wangu Mama Mushi wa somo la NEWS REPORTING Chuo kikuu MT. Augustine Mwanza alinifundisha kwamba Greater The Name Greater The News, And Greater the Event Greater the New”. Ila hili neon lisitumike visivyo ili kuweza kuwanyima na kuwafunga midomo wananchi. Pamefikia mahari mtu unahamua kuaghahilisha kununua Gazeti Fulani kisa linapendelea sana upande Fulani wa chama au kundi la watu wataka Madaraka badala ya kuwazungumzia wananchi na shida zao zinazozidi kuongezeka siku hadi siku na zitazidi kuongezeka siku hadi siku.

Inawezeka waandishi wetu wanafanya haya kwa sababu vyombo vya habari vilivyo vingi nchini vinamilikiwa na wenye fedha na wanasiasa hivyo wanalazimika kuandika au kuripoti kile basi wao anachohitaji. kwa mfano kama mimi ningekuwa namiliki vyombo vya habari basi nikilala nikiamka natoa amri kesho magazeti au media zangu zote munilipoti kwamba nimetoa msaada huu ili nionekana nafanya mema kwa wananchi kumbe moyoni ni danganya toto.

 HivyoViongozi wetu tunawaomba muwatumikie wananchi vilivyo ili kuweza kuleta ufanisi zaidi na kupunguza lindi la umaskini linaloikabili nchi yetu. Masuala ya uchaguzi 2015 yasiwe ndio kikwazo kwa maendeleo ya nchi yetu Tanzania. CCM na CDM na vyama vingine muwatumikie wananchi kwanza na sio kulumbana juu ya uchaguzi 2015 na badala yake mufanye kama mulivoagizwa na wananchi. Je ukifika mwaka 2015 utawaeleza nini hao wananchi waliokuchagua kuwa kiongozi wao? 

Makala hii Imeandikwa na Chiwambo Ausi
TEOFILO KISANJI UNIVERSITY (TEKU)
E-Mail: Ausichiwambor@hotmail.com